Meli mbili za ufilipino na china zagongana Manila watajwa kuhusika

Meli mbili za ufilipino na china zagongana Manila watajwa kuhusika

jjackline

Senior Member
Joined
Jul 25, 2024
Posts
111
Reaction score
274
Meli zinazopeperusha bendera za China na Ufilipino zimegongana leo Jumatatu, Agosti 19, 2024 karibu na mwamba unaogombaniwa katika Bahari ya Kusini ya China.

Kulingana na vyombo vya habari vya Serikali ya Beijing, China inaishutumu Manila kwa kusababisha ajali hiyo kwa makusudi.

Msemaji wa walinzi wa Pwani ya China, Gan Yu amesema:“Meli ya walinzi wa Pwani ya China ilijaribu kuzuia meli ya Ufilipino kufika Sabina Shoal.”

Meli ya Ufilipino inadaiwa kwenda njia isiyo ya kitaalamu na ya hatari, hivyo kusababisha mgongano.

Katika shutuma zake hizo, Yu amesisitiza hatua ya meli hizo kugongana ilikuwa ya makusudi na kwamba Ufilipino ndio inayohusika zaidi.
Snapinsta.app_456083868_1436252360384690_5042593791131761242_n_1080.jpg
 
Mtu akiwa na nguvu lazima aanze ukurofi. Imagine China anasema bahari yote ya South China ni yake!!?
 
Back
Top Bottom