Meli ya mizigo ya Tanzania imepinduka Kusini mwa Iran

Frumence M Kyauke

JF-Expert Member
Joined
Aug 30, 2021
Posts
630
Reaction score
1,262
81C58465-67FE-45C9-9A32-55BCF356C013.jpeg

Meli ya mizigo ya Tanzania iitwayo Anil imepinduka katika bandari ya Assaluyeh Kusini mwa Iran Siku ya Jumanne, Januari 24 kutokana na mpangilio mbaya wa Makontena kwenye bodi.

Ajali hiyo imetokea katika Bandari inayohusika na kemikali za petroli na gesi zinazozalishwa nchini Iran iliyopo kilomita 950 kusini mwa Tehran.

Katika taarifa iliyotolewa na IRNA, tovuti rasmi ya habari ya Iran, ilifichuka kuwa wafanyakazi wa Meli waliokolewa na kupelekwa kwenye eneo salama na timu ya uokoaji. Maelezo zaidi bado hayajatolewa.

Biashara ya Shehena ya kila mwaka kati ya Tanzania na Iran ni chini ya dola milioni 100 lakini mauzo ya nje na uangizaji umepungua tangu tangu Marekani ilipoweka vikwazo kwenye mafuta na benki ya Iran.
 
View attachment 2496054

tuombe mizigo iwe imekatiwa bima
 
Mna uhakika kuwa ni ajali na si hujuma itokanayo na vikwazo vilvyowekwa na Marekani?
 
ANIL arrived at Asaloyeh from Bandar Abbas. Container ship ANIL, IMO 8822143 built 1989, flag Tanzania, manager unknown

Wanatabia ya kusajir meli Tanzania ila mmiliki anakuwa mtu wa nnje
Ni kawaida kusajili chini ya bendera za nchi tofauti na wenye mali kwa sababu ya ushuru na tozo kwa nchi zingine zipo juu sana, kwa hiyo wakisajili kwenye nchi zingine wanapunguza gharama sana
 
Usajili huo hua wanapitia Zanzibar na ziko meli nyingi sana Za Bara Asia ambazo hutembea na bendera ya Tanzania
 
... ni simba wa bahari au nani hawa? Pole zao.
 
Back
Top Bottom