Meli inaanza kuingiza maji wahudumu wanamwambia nahodha:
“Captain, kuna uvujaji mkubwa upande wa chini!”
Lakini nahodha anajibu:
“Msipige kelele. Meli hii imekuwa ikisafiri miaka 20 bila kuzama. Endeleeni na ratiba kama kawaida.”
Maji yanaendelea kuingia.
Mhandisi anasema:
“Tunapaswa kupunguza mzigo na kuziba sehemu hii mara moja.”
Nahodha:
“Hapana. Tukikubali kuna tatizo, abiria wataingiwa na hofu. Waambieni kila kitu kiko sawa.”
Baadhi ya wafanyakazi wanaona tatizo ni kubwa, lakini wanaogopa kumwambia ukweli kwa sababu wale waliowahi kumkosoa nahodha walifukuzwa.