Uchaguzi 2020 Membe afurahishwa na uteuzi wa Wagombea Ubunge wa CCM, awakaribisha ACT-Wazalendo wale waliokatwa

Uchaguzi 2020 Membe afurahishwa na uteuzi wa Wagombea Ubunge wa CCM, awakaribisha ACT-Wazalendo wale waliokatwa

johnthebaptist

JF-Expert Member
Joined
May 27, 2014
Posts
97,869
Reaction score
171,716
Mgombea urais wa ACT-Wazalendo Bernard Membe amesema amefurahishwa sana na uteuzi wa wagombea Ubunge wa CCM na kuwapa pole wote waliokatwa kwa sababu walikuwa karibu naye.

Membe amewakaribisha wale waliokatwa kujiunga na ACT-Wazalendo ili safari iendelee.

Ameandika katika akaunti yake ya Twitter.

Maendeleo hayana vyama!

1597993614569.png
 
Anaandika Bernad Membe baada ya baadhi ya watia nia wa Ubunge kupitia CCM kukatwa na kamati kuu ya chama hicho licha ya kuongoza kura za maoni.

"Uteuzi wa CCM uliofanywa leo umenifurahisha sana! Nawapongeza wote waliobahatika kuteuliwa, lakini kubwa zaidi nawapa pole wale wote waliokatwa kwa sababu ya kuwa karibu nami. Hiyo ni baraka siyo balaa. Karibuni mjiunge na ACT- Wazalendo haraka ili safari iendelee!"
Screenshot_20200821-092312.png

MY TAKE; Membe anataka kutuaminisha nguvu yake aliyo nayo ndani ya CCM.
Wapo tayari kuwapokea kina Chenge kuifanya ACT kuwa CCM B rasmi?
 
Mshauri Mkuu wa Chama cha ACT-Wazalendo na Mgombea Urais wa chama hicho, Bernard Membe amewakaribisha wale waliokatwa katika uteuzi wa kuwania ubunge kupitia CCM kujiunga na ACT Wazalendo


Ameandika kwenye ukurasa wake wa mtandao wa kijamii ‘Uteuzi wa CCM uliofanywa leo umenifurahisha sana! ... nawapa pole wale wote waliokatwa kwa sababu ya kuwa karibu nami’

Amesema kukatwa kwao CCM ni baraka sio balaa kwa kuwa sasa wanaweza kujiunga na ACT-Wazalendo, ili safari iendelee, aidha amewapongeza wale wote walioteuliwa

2020-08-21.png
 
Kumbe moyo wake bado uko CCM; yaani bado anaiwaza CCM muda wote? Uzoefu unaonyesha kuwa ni asilimia ndogo tu ya waliowahi kukatwa CCM wakahamia upinzani na kushinda: Slaa, Wassira na Shibuda. Bulaya hakukatwa bali alihama kabla ya mchakato.
 
Your idea is good but time isn't in our side Mr. Membe!! I think they did this purposely, to caught us in a box.
 
Back
Top Bottom