Membe amwaga siri Hayati Magufuli alivyomfitini na kumkosesha Ukatibu Mkuu wa Jumuiya ya Madola

Taifa hili lina ma "sadists" wengi sana na ni jambo la kutisha wanaweza kupata nafasi kubwa za maamuzi siku yoyote huku tukiwa na katiba ya sasa.
Hivi hii inatokana na nini?
 
Unamaanisha nini?
Hata kama ukijaribu huwezi kumridhisha kila mtu. Kiongozi ni kama mzazi, kwa baadhi ya watoto atakuwa kama mkali, kwa wengi mpole, kwa wengine kama adui na kwa wengine kama rafiki. Hata ufanye nini huwezi kumridhisha kila mtu. Kwa sababu mtazamo wake juu yako hauhusiani kwa vyovyote na wewe. Ni maamuzi yake binafsi.
 
Dr Salon Ahmed Salon aliungwa Mkono na Raisi wake na pia OAU lakini alishindwa kuwa UN secretary General, hivyo hata kama JPM angemuunga mkono n.k kulikuwa hakuna uhakika wa Yeye kupata.
Na hizo hela anazozungumzia alizopata, alizipata/ tulizipata kwa kuwa wanachoma wa Jumuiya ya Madola na sio kwa sababu ya Yeye kutaka kuwa/ au kuwa Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Madola . Au kusema kwamba Basi angekuwa katibu Mkuu Angeles hizo hela nyingi Tanzania kwa "upendeleo" angekuwa ana kwenda kinyume cha mkataba wa kazi yake kuwa mtenda haki.
Kuna Ntu tena Mbongo alifanya hivyo UHabitat Nairobi , matokeo yake mkataba wake ulivyoisha hakupata mkataba mwingine.
 
Pamoja na mazuri ya Mwendazake ila utawala wake ulikuwa na makandokando mengi sana, kubwa zaidi ni chuki zake binafsi.

Tunaomba Polepole na Bashiru nanyi mjibu kwa upande wenu na kwa niaba ya Mwendazake.
Wakijibu unitag
 

..magufuli unayemtetea alikuwa na mahusiano mabaya na viongozi wenzake ktk EAC, na alihudhuria kikao kimoja tu cha wakuu wa nchi za AU.

..kuna umuhimu wa nchi za afrika kuwa na uwakilishi ktk taasisi mbalimbali za kimataifa kama un, commonwealth secretariat, etc etc ili tuweze kutetea hoja na maslahi ya nchi zetu.
 
Ubaya huo ulihusiana na nini? Kama alikuwa ana uhusiano mbaya alipofanya ule mkutano wa SADEC Tanzania aliongelea nini? Kwahiyo wewe hukuona jinsi nchi hizo zilivyogeuka kuwa agents wa mataifa ya nje kwa faida ya hizo nchi?

Mara ngapi adui yako amekuita wewe mbaya je unakubali kuwa wewe ni mbaya kwasababu tu asiyekupenda kakupa hilo jina? Grow up man...Hii ni 21st century, vizazi vyetu havitakubali haya...watch and see....Mandela hakuitwa mbaya ti bali gaidi....Mnatirudisha nyuma mno na mawazo yenu haya ya ancestor mangungo, wenzenu tulisha toka huko zamani...Tuache uvivu tufanye kazi, mahusiano yanajengwa kwakuheshimiana siyo kwa mmona kukubali kuwa mtumwa ili apate vya dezo ambavyo havijasaidia kwa centuries...Tutaendelea kuwakataa manabii wetu mpaka lini? Wake up guys!
 
Tumepita katika ombwe kubwa, na nasikia walipanga mipanga mipango ovu mikubwa huko mbeleni na akina bashiru na polepole
Utaendelea kusikia mabaya tu usipofundisha masikio yako vitu vya kusikiliza...Majungu tu ndiyo people are good at...
 
Nimependa idea yako ya self reliance LAKINI ni nani ambaye atakubali umuuzie vitu wakati hamna ushirikiano mzuri, wewe umejifungia haushiriki katika matatizo na furaha za jamii (misiba na harusi) then unataka ukipata harusi watu waje kwako, watakuja kweli?

Mfano ni namna majirani walivyokataa mahindi yetu wakidai yana sumu kuvu baada ya trip moja ya mother kwa jirani mahindi yakaisha sumu kuvu ghafla.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…