Membe amwaga siri Hayati Magufuli alivyomfitini na kumkosesha Ukatibu Mkuu wa Jumuiya ya Madola

Membe amwaga siri Hayati Magufuli alivyomfitini na kumkosesha Ukatibu Mkuu wa Jumuiya ya Madola

Ok, naona Membe ameamua kufunguka ila ajue wengine aliowasema bado wako hai, hapa naona vita ya maneno itaenda kuanza very soon huko CCM, na zaidi zile kelele za "hawa wa kanda hii" na "wale wa kanda ile" zitazidi kushika kasi na hili litakuwa kikwazo kwenye serikali ya Samia hasa baada ya Rais kusikika akisema hamtumbui mtu kutokana na kabila lake.

Membe anachofanya kwa kifupi ni kuonesha zamu yao ya kujidai imerudi, ndio maana juzi amesikika Mzee Makamba akisema Mungu halishwi ugali analishwa maombi na akayasikia, leo Membe anakuja na hili, Kinana nae aliwahi ku tweet siku za nyuma akionesha sasa mambo yao safi, na Makamba mdogo karudishwa serikalini, kwao ni mwendo wa kucheka cheka tu huku wakitudanganya wanatibu majeraha.

Katiba Mpya ndio suluhu yetu, ije kutuondoa kwenye haya makundi yanayojiona yana hati miliki ya kututawala, waroho wa madaraka wasioshiba, Membe alitaka kubebwa na Kikwete mambo yakagoma baada ya Lowassa kutemwa, ile vita ndio ikamzaa Magufuli, lakini japo alionekana "neutral" wakati ule, bahati mbaya nae akaja kutengeneza kundi lake.

Tuache kuishi kwa kutegemea fadhila za hawa walafi wanaojidai kutupenda, ni waongo na wanafiki wanaoyapenda zaidi matumbo yao.

Kumbe Membe alitaka kwenda kuwa KM Common wealth ili apate paundi bilion 7 wakati bado hajatuambia zile za Gaddaffi ilikuwaje. Basi Magufuli alimkataa kwasababu alizijua tabia zao hawa wapenda pesa, huu sio muda wao wa kutoka mafichoni na kuanza kupiga kelele kama wanavyodhani kwani bado ni wachafu kwa matendo waliyofanya siku za nyuma, Kinana pembe za ndovu....

Wacha niendelee kufuatilia kesi ya Mbowe naamini yule wanayelazimisha kumfunga mdomo ndie mwenye threat kwao, na wote kwa pamoja bila kujali makundi yao chamani huungana kumpiga vita ili waendelee kuitafuna nchi yetu kama ni mali ya baba yao, naamini iko siku taifa hili litaupata ukombozi wa kweli.
jpm alikuwa Rais wa mfano kwa africa na Dunia mzima.Membe huwezi mchafua bado anaishi kwe mioyo ya Watz.RIP baba yetu.
 
Mtu kihiyo pekee atamuamini huyo zoba Membe. Tangu lini hawa wapuuzi wakawa na uchungu na watu wa nchi hii zaidi ya kutanguliza maslahi yao. Mi naona kaongea utumbo wa kuku.

@Rutagwerera,
Mkuu hata utumbo wa kuku ni chakula kwa baadhi ya watu.
Akae atulie Kwa sababu ni kiazi, kilaza na hajielewi.
kwa nafasi alizowahi kuwa nazo hapaswi kuwa mtu wa kulialia na kulalama kama sie machinga huku mitaani.

Tena, kumsema marehemu(Mhe. Hayati Magufuli) anaonesha alivyoishiwa hekima na busara za kitanzania.
 
  • Thanks
Reactions: Ame
Sanaaa. Huyu baba ni mwehu. Anaongea uharo. Anaji-contradict yeye mwenyewe ukimsoma between the line. Aache uwongo wake kwa CV gani mpaka aukwae ukatibu wa Jumuiya ya Madola.
Ana sifa ya uchafu wa miongoni mwa majitu maroho na yanayoitafuna ya nchi hii kwa maslahi ya familia na mitandao ya madhalimu wenzao. Hawaridhiki kuiba kote huko.
Kwani watafika wapi? Hana miaka zaidi ya 30 hapa duniani hata akiwa mzima akili itakuwa imeisha isha uwezo....Atakumbana na hukumu yake ashukuru Mungu iwapo itakuwa ahera...
 
nilicho note hapa ni "mimi nimetoka katika intelligence na nina Network". mtu kama huyu kumuangusha ni vigumu
 
Soviet ilianguka kwa kujifanya mlinzi na mlezi wa kila nchi ya kijamaa!!
====
Sasa na Kenyatta alikuwa anamuogopa Hayati JPM kiasi cha kumuomba Kinana amfikishie ujumbe? Hii ni kweli? Hivi ikijakugundulika si kweli hali itakuwaje?
- - - -
Ukiwa na mentality ya utegemezi ni vigumu kulivusha taifa. Eti kule kuna fedha nyingi za kusomesha, nakadhalika,...kwa nini usifikirie kucreat bidhaa na huduma za kuuza huko jumuiya ya madola ili upate fedha za kusomesha watu wako na kufanya miradi ya maendeleo? Unawaza kupata hela za "bure" huko kwenye madola. Hii ni aibu kwangu mimi.
*****
Sasa kamati itaundwa, ukatibu wa madola utapatikana.
Kenyata sio kwamba alimuogopa jiwe lakini unapokuwa Rais wa nchi nyingine hupaswi kuingilia mambo ya nchi jirani pia hawa viongozi huwa wana urafiki fulani so inabidi waangalie nani anaelewana na nani
nakupa mfano, Idd amin aliwahi kuwateka waandishi habari fulani wa ulaya,rais wa hiyo nchi aliangalia nani ni rafiki wa Idd amin ndipo ikaoneka ni Mobutu hivo Mobutu akaombwa ambembeleze Idd Amin
hii ni mfano wa mambo yanavoenda hata sasa,wewe ukiwa Rais wa nchi nyingine na huna uhusiano wa karibu na Rais fulani unamtumia kiongozi aliyekuwa karibu naye
 
Huku Membe,kule Assad na Vicky
JPM naona ilikua kazi kupiga watu na vitu vizito kichwani😅

Poleni sana jmn
 
Ilikuwa iwe sifa kwa Tanzania kutoa katibu mkuu wa jumuia ya madola kwa maana ya Bernard Membe. Enzi zile Tanzania tulipewa heshima kubwa sana kimataifa kwa ajili ya kina Dr Salim Ahmed Salim, Kachero Dr Mahiga, kina Mwakawago, Getrude Mongella, Dr Asha Rose Migiro, Amb.Nyakhi Anthony nk. Kipindi cha JPM Ilikuwa sifa kupata watanzania wenzetu hawa kina Membe huko commonwealth , Likwelike na Dr Mulamula huko African union nk lakini kwa weusi wa roho ya JPM aliona ni afadhali hizo nafasi zidumbukie kina kirefu gizani au chooni kuliko mtanzania mwenzake na nchi yake ipate! Kiongozi wa ajabu mnooo! No wonder dakika ya 89 utabiri wa Membe na Lema ukatimia. Membe sio wa kubezwa. .
 
Membe hasione tumenyamaza,
1:Candle la Ushoga na msaada wa Uingereza Enzi ukiwa waziri wa Mambo ya Nje
2: Kuna mwingine analopokalopoka ,tunakumbuka alipokuwa waziri wa utalii 1992 aliuza mbuga ( Otterlo Business Corporation) Km 15000M^2 loliondo corridor!

Mmeingiza nchi katika migogoro mikubwa na kwakuwa wakuwasema hayupo mnalopoka tu.
Hii inatupa picha hiki kibibi kinalinda masilahi yenu, sio kwa ulopokaji huuu, kamilisheni Mambo yenu tu, utawala utarudi kanda ya ziwa mtaona
Hee Sukuma Gang bado mnapumua kumbe🤣🤣🤣
 
Kwanini usiwaze kwamba alikuwa hataki atumiwe kuhujumu taifa letu wenyewe kwa kipande cha pesa?

Umeelewa maelezo yake lakini? Kama bado hizo pesa kazi yake ni ipi na thamani yake ukilinganisha na watakayochukua kupitia hiyo diplomasia?

Kwanini unadhani hawakunichagua mimi au wewe? Can't you see what was needed from him? Ebu tuweni basi na critical analysis japo kidogo!
JPM alikuwa mzalendo lakini alikuwa binadamu mwenye udhaifu mwingi wenye kuhitaji mijadala mirefu. Ameshaondoka juu ya uso wa dunia, hawezi kujitetea hivyo sio suala jema kumuongelea kwa mabaya.
 
Mimi sijamuelewa aliposema kuwa ilikuwa akabidhiwe paundi bilioni saba baada ya kuwa Katibu Mkuu wa Commonwealth. Hizo pesa alikuwa apewe ili awape watanzania au azitumie kwa faida ya wanajumuia wote? Kama alishaanza kupigia hesabu hizo pesa ili ziwafaidie watanzania wenzake tu basi angepwaya kwenye ile nafasi.

Amandla...
 
Kwanini usiwaze kwamba alikuwa hataki atumiwe kuhujumu taifa letu wenyewe kwa kipande cha pesa?

Umeelewa maelezo yake lakini? Kama bado hizo pesa kazi yake ni ipi na thamani yake ukilinganisha na watakayochukua kupitia hiyo diplomasia?

Kwanini unadhani hawakunichagua mimi au wewe? Can't you see what was needed from him? Ebu tuweni basi na critical analysis japo kidogo!

..membe alikuwa anazungumzia nafasi ya katibu mkuu wa jumuiya ya madola.

..taasisi kubwa kama hiyo kuongozwa na Mtz kuna faida zake kwa nchi yetu na watu wake.

..mwalimu nyerere alimpigania salim ahmed salim awe katibu mkuu wa Umoja wa mataifa.

..kulikoni rais magufuli akatae kumuunga mkono Mtz mwenzake kwa nafasi ya katibu mkuu wa jumuiya ya madola.

..hata kama alikuwa hamtaki membe kwanini hawakupendekeza Mtz mwingine ambaye waliona anafaa?
 
Mimi sijamuelewa aliposema kuwa ilikuwa akabidhiwe paundi bilioni saba baada ya kuwa Katibu Mkuu wa Commonwealth. Hizo pesa alikuwa apewe ili awape watanzania au azitumie kwa faida ya wanajumuia wote? Kama alishaanza kupigia hesabu hizo pesa ili ziwafaidie watanzania wenzake tu basi angepwaya kwenye ile nafasi.

Amandla...

..siyo fedha kwa ajili ya kudumbukiza kwenye mifuko yake au ya Watz.

..hiyo ni bajeti ya commonwealth secretariat ambayo inaongozwa na katibu mkuu wa jumuiya.

..sehemu ya fedha hizo ni kwa ajili ya MIRADI mbalimbali ktk nchi wanachama wa jumuiya.
 
..membe alikuwa anazungumzia nafasi ya katibu mkuu wa jumuiya ya madola.

..taasisi kubwa kama hiyo kuongozwa na Mtz kuna faida zake kwa nchi yetu na watu wake.

..mwalimu nyerere alimpigania salim ahmed salim awe katibu mkuu wa Umoja wa mataifa.

..kulikoni rais magufuli akatae kumuunga mkono Mtz mwenzake kwa nafasi ya katibu mkuu wa jumuiya ya madola.

..hata kama alikuwa hamtaki membe kwanini hawakupendekeza Mtz mwingine ambaye waliona anafaa?
Thank you
True story
 
Back
Top Bottom