Membe anaweza saidia sana katika mchakato wa kudai Tume Huru ya Uchaguzi

mkamanga original

JF-Expert Member
Joined
Jan 21, 2015
Posts
637
Reaction score
663
Vyama vya siasa vinavyo jitambua ambavyo vimeanzisha mchakato wa kudai Tume Huru ya uchaguzi vinaweza kucheza vizuri karata kama watamtumia Bernard Membe.

Namshauri Membe kutojiunga na chama chochote cha siasa ili kile anachokiamini kiweze kufanikiwa, apigane hii vita akiwa kama mwanaharakati huru. Akifanikiwa atakuwa amejijengea heshima kubwa wananchi wanaojitambua

Ninaamini kwamba Membe anaweza kuwa msaada katika hili kutokana na uzoefu wake Wa ushawishi wa kukaa wizara ya mambo ya nje kwa takribani miaka 10. Kwa hiyo atatumia uzoefu Huo kujenga ushawishi kwa mataifa ya nje kama China na maeneo mengineyo.

Akishafanikiwa hilo ndio sasa anaweza kufikiria hatua nyingine ya mbele.

Hii nchi bila Tume Huru ya Uchaguzi, chaguzi zinazofanyika zinakuwa hazina maana kwa nchi.

Tujadiliane hapa namna bora ya kupata tume huru na muundo wake uweje, kwa wanaojitambua tu wanaruhusiwa kuweka neno.
 
Tuyaache Hayo kwanza,tuangalie lililopo kwanza mbele yetu la corona . Membe ni CCM damu sio wa kumwamini Sana yasije yakawa kama Yale ya 2015
 
naafikiana nawe isipokuwa hapo kwenye "China".
 
Vyama vya siasa vinavyo jitambua ambavyo vimeanzisha mchakato wa kudai Tume Huru ya uchaguzi vinaweza kucheza vizuri karata kama watamtumia Bernard Membe.

Namshauri Membe kutojiunga na chama chochote cha siasa ili kile anachokiamini kiweze kufanikiwa, apigane hii vita akiwa kama mwanaharakati huru. Akifanikiwa atakuwa amejijengea heshima kubwa wananchi wanaojitambua

Ninaamini kwamba Membe anaweza kuwa msaada katika hili kutokana na uzoefu wake Wa ushawishi wa kukaa wizara ya mambo ya nje kwa takribani miaka 10. Kwa hiyo atatumia uzoefu Huo kujenga ushawishi kwa mataifa ya nje kama China na maeneo mengineyo.

Akishafanikiwa hilo ndio sasa anaweza kufikiria hatua nyingine ya mbele.

Hii nchi bila Tume Huru ya Uchaguzi, chaguzi zinazofanyika zinakuwa hazina maana kwa nchi.

Tujadiliane hapa namna bora ya kupata tume huru na muundo wake uweje, kwa wanaojitambua tu wanaruhusiwa kuweka neno.
Mi nashauri anaweza akasaidia sana kwenye hili kama akiwa kiongozi wa chama kikuu cha upinzani. Hii itamsaidia kuwa na platform ya kusemea na kuungwa mkono. Hivyo, aingie Chadema. Mbowe ajiuzulu uwenyekiti na mara moja Membe apewe uwenyekiti. Kwa kuwa Mwenyekiti wa Chadema na kwa kutumia ubobezi wake kwenye ukachero na diplomasia za kimataifa ni rahisi sana kuipata Tume Huru ya Uchaguzi. Baada ya kuipata, agombee urais kupitia Chadema kama ilivyokuwa kwa Lowassa mwaka 2015!
 
Back
Top Bottom