Membe arejeshewa kadi yake ya CCM

Membe arejeshewa kadi yake ya CCM

Aliyewahi kuwa Waziri wa Mambo ya Nje Bernard Membe, leo amekabidhiwa kadi ya CCM na Katibu wa Itikadi na Uenezi wa chama hicho Shaka Hamdu Shaka, makabidhiano hayo yamefanyika Chiponda mkoani Lindi..

Awali Membe alifukuzwa uanachama na chama chake na kisha kujiunga na chama cha ACT Wazalendo na aligombea kiti cha Urais katika uchaguzi wa mwaka 2020. ambapo kupitia kikao cha Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM kupitia Mwenyekiti wake Samia Suluhu Hassan, mnamo Machi 31 mwaka huu kilitangaza kumsamehe na kumrudishia uanachama wake baada ya kuandika barua ya kuomba msamaha.

Membe amerejea Chama cha Mapinduzi (CCM) sambamba na wanachama wengine zaidi ya 1,000 wa vyama vya upinzani waliorejesha kadi katika mkutano huo.
View attachment 2243583

Hivi kadi ya ACT karejesha? Na ya CCM lini aliirudisha ? Na mbona anayorejeshewa ni mpya sana? Au kadi mupya? We call it publicity! Ofisi ya mwenezi haina usmart….si kuna kadi za ki electronic ziliishiwa wapi na mbwembwe zile. Hapo ndio palikua pakufanyia publicity
 
Back
Top Bottom