Tetesi: Membe awakatalia Kardinali Pengo na Askofu Malasusa kumsamehe Musiba

Hahahahah sawa bwana, sasa wewe kafungue mashataka kuhusu ufisadi uliokithiri kisha tutaona jinsi hizo mahakama zita respond juu ya malalamiko yako.
 
Mimi ni mkatoliki Niliacha kusali sababu ya huyu mzee. Ndiye kiongozi mkuu wa kanisa lenye waumini wengi Tanzania na duniani kote.

Cha ajabu hata Watz 1000 wakafa au kuuawa kwa siku moja huwezi kusikia salamu za rambi rambi za huyu Bwana.
Alikuwa swahiba wa wauaji kama hakina Bashite nk.
 
Huenda familia nia yao sio kurudisha heshima Bali wanataka kurudisha zile zilipunguzwa wakati wa Jiwe😁😁anyway.. Kama angetaka Heshima irudi... Angemsamehe Musiba... Maana anaesamehe ndio mtu strong, maana anakana matakwa yake, na kutanguliza furaha ya mwingine... Lazima abarikiwe... Ila kama anangangania kisasi... Na yeye ajihoji ameumiza wa ngapi.... Na je aliumiza kama atalipa kisasi.. Hiyo pesa na kisasi chake vitampa furaha?
 
Mahakama inatoa hukumu haitoi kisasi😅😅
 
Sahihi
 
Mimi ni mkatoliki Niliacha kusali sababu ya huyu mzee. Ndiye kiongozi mkuu wa kanisa lenye waumini wengi Tanzania na duniani kote.

Cha ajabu hata Watz 1000 wakafa au kuuawa kwa siku moja huwezi kusikia salamu za rambi rambi za huyu Bwana.
Sali tu mkuu kama mimi, ila mambo zake na hata nikimuona tu Pengo moyo wangu unarudi nyuma sana. Natamani angekaa tu kimya.
 
Mh Membe hakuna kumsamehe huyo muhuni musiba piga mnada kila kitu ,ulitoa fursa ya kuomba msamaha lakini alijifanya mbabe na kuendelea kukudhalilisha....Piga mnada hadi makobazi yake najua mali zake hazifikii hizo 9.9B ,kufidia pia mfunge mpaka ndugu zake walipe ndiyo atoke ,hii utaweka precedent kwa wahuni wajao.
 

Sure huyo Muhuni MUSIBA inabidi awe funzo kwa WAHUNI wengine.

Membe hakuna kumsamehe kabisa.
 
Ni aibu sana mahakama kufuata mikumbo ya mihemko ya kisiasa.. Uko wapi uhuru wa kutoa maoni wa mtu?
 
Ni aibu sana mahakama kufuata mikumbo ya mihemko ya kisiasa.. Uko wapi uhuru wa kutoa maoni wa mtu?
Yaani ni mambo ya kushangaza, fidia ya bilioni 9 kuamuriwa kulipwa kwenye nchi maskini ambayo wastani wa kipato cha mwananchi kwa mwaka hakifiki hata laki 5 na zaidi ya asilimia 80 ya watu wakiishi chini ya mstari wa kima cha umaskini.​
 
Ili Iwe fundisho kwa waandishi makamjanja na chawa,huu upuuzi unawasumbua chawa wengi Sana.

Mahakama ikitekeleza Hali atayokuwa nayo musiba baada ya kuuzwa Kila kitu chake na Bado hata robo haifiki,waliobaki wakimua galia musiba hawatakubali kamwe kutumika
 
Ni aibu sana mahakama kufuata mikumbo ya mihemko ya kisiasa.. Uko wapi uhuru wa kutoa maoni wa mtu?

Mkuu ulifuatilia mwanzo wa kesi hadi mwisho? Ukimdhalilisha mtu bila ushahidi ni kosa ,Musiba alimsema vibaya sana Membe ,Membe alimsihi Musiba afute kauli na kumwambia aombe radhi aotherwise atapeleka kesi mahakamani na yeye apate haki yake ,Musiba kwa jeuri hakumsikiliza Membe kisa alikuwa analindwa na "STATE".

Umeangalia kwa upande wa Musiba ila wa Membe haukuangalia kabisa ,Uhuru gani wa kutoa maoni kwa kumkashifu mtu kwa tuhuma za Uongo? Huyo Mpuuzi mwache apate fundisho ili wahuni wenzake waje kujifunzo in the future.
 
Wakati dalali wa Mahakama kampuni ya Yono (vijana wa kazi) ikihesabu siku zilizobaki katika 14 (siku za kazi) alizolewa mtukanaji Cyprian Majura Musiba kumlipa fidia Kachero Bernard Membe jumla ya shilingi 9.2 Bilioni, Bwana Musiba amewaangukia viongozi wa dini Askofu Alex Malasusa (KKKT Diyosisi ya Pwani) na Kardinali Porlycarp Pengo kumwombea msamaha kwa Membe asipige mnada mali zake.

Taarifa kutoka ndani ya familia ya Membe nyumbani kwake Mikocheni zinaeleza kwamba Jumatatu ya tarehe 24/4/2023 majira ya saa 10 alasiri mjumbe kutoka kwa Pengo alifika kwa Membe kumpa ujumbe wa Pengo kumsihi amsamehe Musiba.

"Alikuja hapa padre wa moja ya makanisa yetu kuleta ujumbe huo lakini naona Mzee alimkatalia na kumwambia 'namheshimu sana baba Askofu Pengo lakini kwenye hili anisamehe yeye (Pengo) huyu kijana lazima alipe gharama ya matusi yake' " anasema mwanafamilia aliyetajwa kwa jina la Colleta na kuongeza:

"Lakini jioni yake ya saa moja Askofu Malasusa naye alimpigia simu Mzee kuongelea suala hilo hilo lakini naye Mzee alimpa majibu yale yale aliyompa mjumbe wa Pengo." Hata hivyo kwa maelezo ya Colleta ni kwamba si tu ni msimamo wa Mwanadiplomasia huyo Bali ni msimamo pia wa familia.

Hii inakuja baada ya jitihada za Askofu Mwamakula pia kugonga mwamba baada ya kumwandikia barua Membe ya msamaha kwa Musiba.

Wakati hayo yakijiri hapa Mikocheni, tayari kampuni ya Yono imeshatua jijini Dodoma itakapoanzia kazi ya mnada kwa kuanza na apartments za Musiba zilizoko Ihumwa, nyumba yake ya Chamwino, guest house yake ya Msalato na shamba la hekari 10 njia ya Singida.

Baada ya hapo Yono atatimba apartment ya Kigamboni, shamba la hekari 5 Bagamoyo kabla ya kugeukia mitambo yake ya uchapaji iliyoko jengo la Exim ghorofa ya 8 jirani na Makao Makuu ya Polisi jijini Dar es salaam.

My take: Vijana tujifunze kitu katika sakata hili la Musiba na Membe kwamba tuwe na akiba ya maneno. Lakini pia akili ya kupewa changanya na zako. Waliokuwa wakimpa akili karibia wote wamemkimbia tena ndio wamekuwa jirani na Membe. Amtegemeae mwanadamu mwisho huwa kama hivi. Musiba kwishney!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…