Membe: Tuwashirikishe UNESCO katika kukuza Kiswahili

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Joined
Feb 24, 2012
Posts
5,108
Reaction score
10,191
Mwanadiplomasia Bernard Membe ameshauri serikali kukuza kiswahili ili kiweze kuwa lugha inayotumika Afrika, kwa kuwa ushahidi upo kuwa lugha ya kiswahili inaweza kutumika bara zima.

Amesema UNESCO wanahela wanaweza kusaidia kukuza lugha hiyo kwa kuanzisha chuo kikuu cha kiswahili ili watu waweze kujifunza.

Amesema jambo hili serikali haiwezi kufanya yenyewe, bali tuwashirikishe UNESCO ambao ndio wana hela na ni wadau wa jambo.

Amesema hayo katika siku ya mchango wa lugha ya kiswahili katika ukombozi wa bara la afrika
 
Legacy ya Membe ni ipi hapa Tanzania?

Anachokijua ni kuombaomba tu
 
Legacy ya Membe ni ipi hapa Tanzania?

Anachokijua ni kuombaomba tu
Ni mwanadiplomasia alietukuka. Akiwa waziri wa mambo ya nje wa awamu ya nne, nchi yetu ilishirikiana na mataifa mbalimbali na ilikuwa na jina ZURI. Kila sikunviongozi wa nchi kubwa duniani na arabuni na Afrika walikuwa wanakuja hapa, nakumbuka kuna siku Obama akiwa Rais alikutana na Bush ambae alikuwa mtangulizi wake hapa Tanzania.

Zile ziara tu za viongozi wakubwa kufika hapa kwetu ilikuwa ni FURSA kubwa sana kwa nchi.Ni wakati wa Membe nchi yetu ilijulikana na kupata wawekezaji wakubwa kutoka nje. Uchumi wa mwananchi mmojammoja uliimarika.

Jiulize baada ya Membe kuondoka, ulimwona kiongozi gani mkubwa akija hapa Zaid ya kagame, Burundi mseven na kinyata??

KAMA MTAWALA ALIEFUATIA ANGERIDHIA NGULI HUYU ANGEKUWA KATIBU MKUU WA JUMUIYA YA NCHI ZA MADOLA. NA HAKIKA KAMA ANGEKUWA KATIBU WA MADOLA, KUNA FAIDA KUBWA SANA NCHI INGEPATA.
 
Unatetea mtu ambaye hata tu kuandika makala kupitia magazeti kutoa mchango wake kwa yale anayofahamu na mafanikio yake kwenye nyanza za siasa, usalama na utengamano..hawezi, unamsifia kwa lipi hasa..he s a dead wood..
 
Back
Top Bottom