Ni mwanadiplomasia alietukuka. Akiwa waziri wa mambo ya nje wa awamu ya nne, nchi yetu ilishirikiana na mataifa mbalimbali na ilikuwa na jina ZURI. Kila sikunviongozi wa nchi kubwa duniani na arabuni na Afrika walikuwa wanakuja hapa, nakumbuka kuna siku Obama akiwa Rais alikutana na Bush ambae alikuwa mtangulizi wake hapa Tanzania.
Zile ziara tu za viongozi wakubwa kufika hapa kwetu ilikuwa ni FURSA kubwa sana kwa nchi.Ni wakati wa Membe nchi yetu ilijulikana na kupata wawekezaji wakubwa kutoka nje. Uchumi wa mwananchi mmojammoja uliimarika.
Jiulize baada ya Membe kuondoka, ulimwona kiongozi gani mkubwa akija hapa Zaid ya kagame, Burundi mseven na kinyata??
KAMA MTAWALA ALIEFUATIA ANGERIDHIA NGULI HUYU ANGEKUWA KATIBU MKUU WA JUMUIYA YA NCHI ZA MADOLA. NA HAKIKA KAMA ANGEKUWA KATIBU WA MADOLA, KUNA FAIDA KUBWA SANA NCHI INGEPATA.