Membe Ubalozi karibia utafungwa kule Brussels

I think it can be very serious kama ubalozi utafungwa for not having heating system halafu bado tukadhani Membe na JK hawapaswi kujua .Ufike mahali ufunge ubalozi kwamba baridi imezidi ndani watu wakose huduma bado wadhani ni utani huu ?

JK na Membe ni muhimu kujua uzembe unaofanywa na huo ubalozi lakini JK au Membe asitupiwe lawama kwa uzembe wa kushindwa kutatua tatizo dogo kama la heating system hapo ubalozini.
Lawama hizo abebe balozi na timu yake.
 

Still attached to old vision of fear...and the politics of kidumu chama cha mapinduzi hata kama kikivurunda namna gani!!..I think we have reached a time when we need to say no to these types of politics and allow new ideas to flow in and develop our nation...By the way we are very behind compared to other nation around us .Its time to adapt new vision,new leadership and develop our country.
 
- Kama ubalozi una tatizo la heating system hili ni tatizo la HOC wa ubalozi, na wala sio la balozi, unless ubalozi wetu Brussels wanatumia system tofauti ya uongozi as opposed na balozi zetu zingine,

- Kwa kawaida ubalozi unatakiwa kuendeshwa kwa hela za viza, hata bila ya kusubiri hela kutoka Foreign sasa kama hapo Brussels hakuna heat, ina maana moja tu nayo ni kwamba kuna HOC mzembe, au ana majungu na balozi.

Waziri hawezi kuhusika na heating za ofisi za balozi zetu, kuna wakuu wengi sana in the process kabla ya kumfikia waziri, unless kuna more than haya ya heating system, basi wekeni wazi hapa tuchambue!
 


Hapana, hapa unapotosha ukweli na kupiga propaganda kwa niaba ya CCM kwa kusambaza hofu zisizokuwa na msingi miongoni mwa wananchi wasiiangushe CCM.

(1) CCM ni kikundi cha watu tu, siyo mashine fulani. Hakuna ushahidi wowote kuonyesha kuwa kikundi cha walioko CCM ndio wanaojua kuongoza tu, hasa tukizingatia kuwa imeshindwa kuikwamua nchi hii kutoka katika umaskini kiasi kuwa hata jirani zetu wa Rwanda waliokuwa wanachinjana wenyewe kwa wenyewe miaka michache iliyopita, leo hii wana uchumi imara kuliko wetu licha ya raslimali nyingi tulizonazo. CCM inaendelea kuwapo madarakani kwa kutumia hizo mbinu za kutisha na kutumia naivity ya wananchi wetu.

(2) Kuhusu uwezo wa sisi kutumia kompyuta siyo kwa sababu ya CCM kabisa. Dunia nzima inatumia kompyuta leo, na sisi bado tuko nyuma sana katika matumizi ya kompyuta kwa vile hatuna miundombinu inayotakiwa kutokana na kuongozwa na CCM. Ikumbukwe pia kuwa watu walioongoza nchi hii kupata uhuru walisoma wakati wa Ukoloni. Kama watu hao wangesema kuwa wamesomesha chini ya mfumo wa ukoloni basi wasiupige vita, basi hata hiyo CCM isingekuwapo. Dunia hii inaendelea kwa kutumia megezui, kwa hiyo ni wazi kuwa wakati umefika kufanya mageuzi na kuiondoa CCM madarakani kuweka chama kingine ili tuzidi kusonga mbele.


(3) Kama kweli Kenya wangekuwa wanaililia KANU, basi wangeichagua wakati wa uchaguzi mkuu uliopita, lakini hiyo KANU haikufikisha hata robo ya wabunge. Vile vile UNIP ingekuwa inakumbukwa huko Zambia kama unjavyodai, ni dhahiri kuwa ingekuwa imesharudi madarakani katika chaguzi zilizofuata lakini haijenda popote. Kwa upande wa Zambia, ingawa kweli Chiluba alikuja geuka kuwa fisadi, utakumbuka kuwa Marahemu Mwanawasa alirudisha imani ya wanachi kwa kupiga vita ufisadi ikiwa ni pamoja na kumwadhibu huyu Chiluba, kama tunavyotaka Mkapa naye aadhibiwe.

(4) ZAPU iliyokuwa ikiongozwa na Joshua Nkomo huko Zimbabwe haikumbukwi na wananchi wa Zimbabwe wote bali inakumbukuwa na Wandebele kwa vile ilikuwa ya wandebele zaidi, wakati ZANU ikiwa ya washona zaidi. Kwa vile washona ni wengi kuliko wandebele, basi ZAPU ilishindwa uchaguzi kwa msingi wa ukabila na siasa za Zimbabwe ziliendelea kwa mtindo huo hadi pale walipoamua kuungansiha ZANU na ZAPU na kuuundwa ZANU-PF ambapo Joshua Nkopmo alifanywa makamu wa Rais. Historia hiyo ya Zimbabwe haina uhusiano kabisa na sisi kuiondoa CCM madarakani kwa vile ZAPU haikuondolewa madarakani na wananchi.
 
Nadhani Membe ndie kiranja wa Mabalozi, bila shaka anajua umuhimu wa ubalozi huo, sasa inakuwaje ukawa hivyo?????????? Labda ni kwa sababu wenyewe walioko huko hawafanyi chochote hivyo wamesahaulika, methali husema "kulichoko machoni na rohoni kipo".
na wachumi husema "return on investment" kama ni zero basi kwa nini mwekezaji aendelee kuwekeza???? sijui Membe angalia hapo Bruxell wanafanya nini?
 
ndugu yangu, uwajibikaji ni wa mkuu wa kituo, hivyo wakuu hao ndio wanawajibika sasa ni nani kafanya mbhona hajamwajibisha maana anaiona baribi hiyo, nnnnnnnn
 
Hivi ni kweli tunaendesha balozi kwa hela za viza? Mimi naamini kuwa huu ni mfano mwingine wa priorities zetu zilivyokuwa warped! Leo ukisikia mkubwa anatembelea nchi hiyo basi utashangaa uwezo wetu wa kuhakikisha kuwa matatizo madogo madogo hayamsumbui. Hizo hela nazo zinatokana na viza?
 


Sidhani kama balozi huwa zinaendeshwa kwa hela ya visa.Sasa balozi ambazo hazipati visa applicants wa kutosha zitajiendeshaje?
 
Kwani hata hivyo pesa za Visa ni kiasi gani ?Balozi zina endeshwa kwa pesa toka Wizarani na zinapitia Bungeni kwenye bajeti .
 
Right. Pesa zinatengwa kwenye bajeti ya serikali. Swali la kujiuliza hapa ni Je balozi zinatengewa pesa ya kutosha kwa mwaka? Inawezekana tunamlaumu balozi bure. Na kwa utaratibu wa serikali yetu, pesa kutengwa kwenye bajeti na kuipata pesa iliyokwishatengwa kwenye bajeti ili kutekeleza kazi iliyokusudiwa ni mambo mawili tofauti. Departments nyingi za serikali huishia kupata chini ya asilimia 70% ya pesa zilizotengwa kwenye bajeti na si kwa wakati. There is a lot of institutional problems within the government system.
 
- Kama ubalozi wetu wa Brussels, hauna hela za viza wakati KLM kila siku imejaa watalii mpaka kuipelekea kusimama Kilimanjaro, basi huo ubalozi unatakiwa kufungwa,

- Wakuu vipi naona ya ofisi za balozi zetu nje hasa majuu yanawapita kwa pembeni, off course hela za viza huendesha ubalozi hulipia local bills na ni hela zinazokuwa at hand kwa ofisi zetu katika nchi kama Belgium, UK, France, US, Holland, Luxemburg, I mean Tanzania tunapokea watalii wangapi toka hizi nchi kwa mwaka?

- Kama ubalozi wa Brussels hauna hela za kulipia bills za heating system, ina maana moja tu kuna mtu anakula hela za viza na zinazotoka bongo, vituo vyetu vya ubalozi katika nchi kama Belgium vinapata hela nyingi sana kutokana na viza, maana hawa watalii wanaojaa kwenye ndege zao hawaji bila viza na viza hazitolewi bure na balozi zetu, labda mtafute vizuri habari za Professor Mbilinyi alipokuwa pale ndio mtaelewa ninachosema,

viongozi wetu siku zote hufanya madudu kwa kutegemea wananchi wasioelewa that is all lakini sio kwamba wana uchawi wa kutuloga ili tuwachague kila wakati, huwa tunajifanya tunajua wakati ukweli ni kwamba hatujui kitu and they love it.
wakuu kama hamyaelewi haya ni kuuliza tu mpewe darasa, ndio balozi zetu nyingi huko majuu hutegemea hela za viza kwa ajili ya kulipia bills ndogo ndogo kama za heating system, na hata sometimes kulipia mishahara ya local staff, kama ubalozi wetu Brussels umekwama kulipia hizo bills basi kuna mtu hapaoa anakula hizo hela, atafutwe na ashugulikiwe mara moja hakuna any hadithi hapo.
 
Watalii wengi kwa mfano wanaoshukia JNIA wanalipia visa hapo Airport Dar es Salaam. Hawachukui visa ubalozini.
 
- Sio kweli mkuu, ni watalii kutoka nchi ambazo Tanzania hatuna ubalozi kama Spain ndio wanaruhusiwa bila ubishi kwenda kuchukua viza bongo,

- Ingawa sio crime kwenda kuchukua viza bongo kwa watalii wa kutoka nchi ambazo tuna balozi zetu, bado ni asilimia 15% wanaokwenda kuchukulia bongo, 80% wanachukulia majuu huko huko,

- Pia kuna nchi fulani ambazo serikali yetu imeamua kua wasiruhusiwe kupewa viza na balozi zetu za nje, ni mpaka applications zao zitumwe bongo Immigration kwa uchambuzi wa kina ndio watumiwe kutokea bongo.

Again, watalii wanaochukulia viza bongo ni asilimia ndogo sana, ubalozi wetu kama wa Brussels unatakiwa kua na hela za kutosha kutokana na viza na hata kuweza kujiendesha kwa matumizi madogo madogo ya kiofisi bila kutegemea hela kutoka bongo, wala hakuna excuse hapo!
 
Leo ukisikia mkubwa anatembelea nchi hiyo basi utashangaa uwezo wetu wa kuhakikisha kuwa matatizo madogo madogo hayamsumbui. Hizo hela nazo zinatokana na viza?

- Wakubwa wakubwa hasa husafiri na cash toka bongo hata siku moja hawategemei hela toka ubalozini, never!, mawaziri na level za chini mara nyingi safari zao huwa zinalipiwa na wenyeji waliowaalika, sometimes wanaweza hata kuwepo kwenye nchi na wasifike kabisa kwenye ofisi zetu za ubalozi, hata siku moja ubalozi wetu nje huwa hauna anything to do na kulipa kwa ajili ya viongozi walioko safarini pale, kama ni wakubwa sana huwa wanakuwa na watu wa protocol ndio hasa moja ya kazi zao hizi za kulipa gharama za wakubwa sio ubalozi.
 
Ubalozi hautakiwi kamwe kuendeshwa kwa hela za viza. Kufanya hivyo ni kwenda kinyume na utaratibu wa matumizi ya fedha za serikali. Matumizi ya Balozi yanatakiwa kulipiwa kutokana na pesa zilizotengwa kwa ajili hiyo na si vinginevyo. Pesa za serikali zinatumika kutokana na "vote" husika. Makusanyo yote, viza n.k. yanapaswa kuwasilishwa hazina. Ndio taratibu.

Wizara husika inapoandaa bajeti yake inapaswa kujua mahitaji halisi ya kila balozi yake ili zitengwe fedha zitakazokidhi mahitaji yake. Ukweli ni kuwa hatufanyi hivyo. Bajeti hazitayarishwi kwa umakini na pesa zinazotengwa haziendani na mahitaji ya kiuendeshaji ya balozi. Matokeo mara nyingi ni huu ukiukaji wa taratibu wa kukopa hela za viza! Kama ilivyoulizwa, je huko ambako si watu wengi wanasafiri kuja Tanzania wataishije? Pamoja na kuwa watu wengi wanasafiri kwa KLM kuja Tanzania lakini si wote wanaotokea katika nchi za Benelux. Na hata hao, sio wote wanaoombea viza zao ubalozini. Hawalazimiki kufanya hivyo. Sheria inawaruhusu kuchukua viza zao Airport au sehemu yeyote watakapoingilia tanzania kama ni more convenient kwao. Hata kama tuna ubalozi kwao.

Matumizi yanayotumika kugharamia safari za wakubwa na yenyewe yanapaswa kulipwa kutokana na pesa zilizotengwa kwa ajili ya shughuli hiyo. Sasa kama pesa hizi zinapatikana (bila kujali wapi, ubalozini au wizarani) bila matatizo lakini za kuhudumia ofisi ya balozi inakuwa mbinde, basi tuna matatizo. Unless kama pesa zilizotengwa kwa ajili hiyo hazikutumiwa ipasavyo na wizara inataka kujua kulikoni kabla ya kutuma nyingine. Hii nayo inawezekana. Haitakuwa mara ya kwanza.

Sijawahi kufanya kazi ubalozini lakini siamini kuwa gharama zote zinazotokana na ujio wa wakubwa zinalipwa na wao wenyewe. Lazima kuna gharama ambazo ubalozi una-incur kutokana na ujio huo. Hizi ni pamoja na safari za balozi, malipo ya ziada ya madereva na wafanyakazi wengine, kukodi kumbi n.k. I stand to be corrected.

Amandla......
 
1.
- Serikali yetu hutoa hela kwa balozi zetu kwa mafungu, sio zote kwa wakati mmoja maana hatuna hizo hela, sasa hakuna sheria inayosema kuwa ni lazima hela za viza zitumike, ila HOC au AAA wanakuwa na discretion ya kutumia hizo hela in case hela za kutoka kwenye mgawo wa serikali zimechelewa au hazipo, lakini ubalozi hauwezi kukosa kabisa hela za kulipia gharama ndogo ndogo kama za heating ina maana moja tu kua kuna mtu anakula hizo hela.

2.
- Kama viongozi ni wengi katika ubaloiz mmoja kwa wakati mmoja na sio wakubwa kuliko mawaziri, hapo ubalozi unaweza kwenda nje ya mstari kuwakodishia magari, lakini only kama wananzo hizo hela, ama sivyo wote watabanana kwenye magari machache yaliyopo hapo ubalozini, lakini la ofisi zetu kuliwalipia huwa ni la mwisho sana, wanapokwenda wakubwa wakubwa zaidi ya mawaziri, huwa ni gharama zao wenyewe maana wanapewa pesa za namna hiyo through watu wao wa protocol.

- Kukodi ukumbi inaweza kufanyika kwa kiongozi kuanzia level ya Waziri Mkuu tu kwenda juu, na siku zote hela hizo za ukumbi hulipwa na wao wenyewe yaani through watu wao wa protocol na hata magari ya ziada inapobidi, ubalozi utalipa wafanyakazi wake tu ambao watahitajika kwa muda wa ziada.
 
 

Hivi bado mpo mnaoamini hii longolongo ya enzi na enzi? Mara ya mwisho nilisikia ujinga huu plae mlimani wakai ZERO (our ex-PM) alipodai kuwa kuwep kwetu hapo kulitokana na juhudi za CCM kama vile kungekuwa na chama kingine hilo lisingeliwezekana... Sasa huyu anakuja na matumizi ya Computer akihusisha na uwepo wa CCM.

Inawezekana bado ndugu yangu unashindwa kutofautisha kati ya TANU na CCM...

Tanzanianjema
 

Kaka makusanyo ya visa yanatofautiana nchi na nchi. Siamini kama Brussles kuna flow ya wageni kiasi cha kuweza kuwezesha kukusanya kiasi cha kutosha kwa matumizi kama hayo. Wengi wanaoingia na KLM ni wa connctions kutoka US/CANADA/germany/Nordic/Scandnavian countries ambazo kuna balozi tofauti. Vilevile kama sijakosea mapato yote huwa yanaingizwa kwenye account halafu kupelekwa Hazina. Hazina ndio wanaotoa fedha/idhini za matumizi kufuatana na bajeti.

Kuhusu wizara ya mambo ya nje inaelekea kuna tatizo kubwa la disbursement kutoka hazina maana mambo mengi yamesimama. Nadhani hii inatokana na tatizo la kuwa na hati isiyo ya kuridhisha kwa muda mrefu sasa. Hili ni tatizo linalochangiwa sana na matumizi yanayokiuka taratibu katika balozi zetu na pia tabia ya baadhi ya watumishi/maofisa wa wizara hii kushindwa kurudisha mahesabu mara watokapo safarini.

Ningelikuwa karibu na mikoba yangu ningeweza kujua kama ubalozi wa Brussels ulikuwa na hati gani kwa mujibu ya ripoti ya mdhibiti wa mahesabu wetu ambayo hutumika sana katika uaandaji na upitishaji wa bajeti ya kila wizara.

Hivyo katika hili kila mmoja anaweza kuwa na hatia.

Waziri kwa kushindwa kudhibiti nidhamu ya matumizi ktk wizara yake, mabalozi na maofisa wa balozi zetu pamoja na hazina ambao wakati mwengine hutokana na redtepism inayokwaza ufanisi lakini muhimu kupunguza ulaji katika serikali yetu.

Tanzanianjema
 
Mzee ES nimesha shuhudi wageni wengi sana wana chukulia VISA hapa hapa Dar .Kuna shida ya Balozi ama ofisi za balozi kukaa majumbani mwa wa watu.Kwa mgano kule Holland jamaa mzungu ni rafiki yake JK for the last 14yrs wanajuana na hata JK akipita pale lazima wanaitana na wanadanya shopping wote , leo ofisi yake iko porini hjata Public transport ni shida hadi uchukue taxi.Wa Dutch they got no time for that wanachukulia airport Dar wanamaliza fitina .Unasemaje ?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…