Mie sikubaliani nawe mpendwa Mshiiri;
CCM is a political party with a common sense as well as common vision.
Kuwepo kwa CCM madarakani kumekuwezesha kuwa kama ulivyo sasa hata kuweza kutumia kompyuta.
Kuwepo kwa CCM madarakani kumekuwezesha kuwa na amani uliyo nayo na uhuru ulionao sasa.
CCM ikianguka leo, wewe na wengineo mnaoiponda mtaikumbuka kama watani wetu wa jadi (Kenya) wanavyoikumbuka KANU, pia kama marafiki zetu Zambia wanapoikumbuka UNIP; Vile vile kama waZimbabwe wanavyo ikumbuka ZAPU-PF iliyokuwa ikiongozwa na Joshua Nkomo (RIP).
Hapana, hapa unapotosha ukweli na kupiga propaganda kwa niaba ya CCM kwa kusambaza hofu zisizokuwa na msingi miongoni mwa wananchi wasiiangushe CCM.
(1) CCM ni kikundi cha watu tu, siyo mashine fulani. Hakuna ushahidi wowote kuonyesha kuwa kikundi cha walioko CCM ndio wanaojua kuongoza tu, hasa tukizingatia kuwa imeshindwa kuikwamua nchi hii kutoka katika umaskini kiasi kuwa hata jirani zetu wa Rwanda waliokuwa wanachinjana wenyewe kwa wenyewe miaka michache iliyopita, leo hii wana uchumi imara kuliko wetu licha ya raslimali nyingi tulizonazo. CCM inaendelea kuwapo madarakani kwa kutumia hizo mbinu za kutisha na kutumia naivity ya wananchi wetu.
(2) Kuhusu uwezo wa sisi kutumia kompyuta siyo kwa sababu ya CCM kabisa. Dunia nzima inatumia kompyuta leo, na sisi bado tuko nyuma sana katika matumizi ya kompyuta kwa vile hatuna miundombinu inayotakiwa kutokana na kuongozwa na CCM. Ikumbukwe pia kuwa watu walioongoza nchi hii kupata uhuru walisoma wakati wa Ukoloni. Kama watu hao wangesema kuwa wamesomesha chini ya mfumo wa ukoloni basi wasiupige vita, basi hata hiyo CCM isingekuwapo. Dunia hii inaendelea kwa kutumia megezui, kwa hiyo ni wazi kuwa wakati umefika kufanya mageuzi na kuiondoa CCM madarakani kuweka chama kingine ili tuzidi kusonga mbele.
(3) Kama kweli Kenya wangekuwa wanaililia KANU, basi wangeichagua wakati wa uchaguzi mkuu uliopita, lakini hiyo KANU haikufikisha hata robo ya wabunge. Vile vile UNIP ingekuwa inakumbukwa huko Zambia kama unjavyodai, ni dhahiri kuwa ingekuwa imesharudi madarakani katika chaguzi zilizofuata lakini haijenda popote. Kwa upande wa Zambia, ingawa kweli Chiluba alikuja geuka kuwa fisadi, utakumbuka kuwa Marahemu Mwanawasa alirudisha imani ya wanachi kwa kupiga vita ufisadi ikiwa ni pamoja na kumwadhibu huyu Chiluba, kama tunavyotaka Mkapa naye aadhibiwe.
(4) ZAPU iliyokuwa ikiongozwa na Joshua Nkomo huko Zimbabwe haikumbukwi na wananchi wa Zimbabwe wote bali inakumbukuwa na Wandebele kwa vile ilikuwa ya wandebele zaidi, wakati ZANU ikiwa ya washona zaidi. Kwa vile washona ni wengi kuliko wandebele, basi ZAPU ilishindwa uchaguzi kwa msingi wa ukabila na siasa za Zimbabwe ziliendelea kwa mtindo huo hadi pale walipoamua kuungansiha ZANU na ZAPU na kuuundwa ZANU-PF ambapo Joshua Nkopmo alifanywa makamu wa Rais. Historia hiyo ya Zimbabwe haina uhusiano kabisa na sisi kuiondoa CCM madarakani kwa vile ZAPU haikuondolewa madarakani na wananchi.