Members wa JF waliojiunga 2007 njooni tusemezane

Members wa JF waliojiunga 2007 njooni tusemezane

MLAU

JF-Expert Member
Joined
Aug 23, 2007
Posts
4,726
Reaction score
3,363
Najua ni mwaka 11 sasa tangu tujiunge na Jamii Forum enzi hizo inaitwa Jambo forum iliyoanzishwa na vijana wawili na kubadilishwa jina baadaye na kuitwa Jamii Forum.

Najua ni mengi tumejifunza humu ndani kupitia mada mbalimbali na hata kujua kama familia.

Nadhani kwa sisi tuliojiunga 2007 ni muhimu kutoa maoni,mawazo,ushauri kwa wengine pia kuhusu namna Jamii Forum inavyosaidia jamii kwa ujumla wake hasa hasa katika kujua haki za binadamu,taarifa kuhusu mwenendo wa Taifa letu na fursa mbalimbali zinazopatika nchini na nje ya nchi.

Ni muhimu kuondokana na tabia ambayo ilianza kujitokeza ya lugha chafu na hata kuonekana kama JF ina makundi katika mada kiasi cha kuanza kuonekana ni cha chanzo cha watz kutengana kwasababu tu tofauti za kiitikadi wakati sisi wote tunalipigania Taifa letu katika ustawi wa watu wake na usawa wa haki kwa kila mmoja.

Nawatakia kila la heri members wote wa JF lakini kwa sisi wa mwaka 2007 tuwe mfano katika mijadala na mada mbalimbali kwasababu ya uzoefu wetu ndani ya Jamii Forum.

Karibuni wote tuifanye JF kuwa kimbilio lakila mmoja katika kutaka kujua mambo mengi na taarifa mbalimbali za nchi yetu na dunia kwa ujumla.
 
Hashima kwako MLAU na kwa wengine wa enzi na enzi toka miaka hiyo,
Kila nisomapo posts na comments mbali mbali za wadau enzi hizo mlikuwa mkitoa hoja zenye mashiko sana.

Bahati nzuri ya sasa hivi members wamekuwa wengi, ila bahati mbaya iliyopo kwa wingi huu wa members ni kila iletwapo thread ya maana basi asilimia kubwa ya wachangiaji ni kutema pumba na mashudu tu wachache ndio huchangia points, hakuna tena kubishana kwa hoja kama zamani.
 
nyie ndo mnadai jf imepoteza msisimko wakati enz zenu mlikuwa mnapost thread za kitoto..!
 
Me nilikuwa bado nuko Bwisya huko visiwani Ukerewe.
 
Umri wako sio type yetu,,, katafute vibabu/vibibi wenzako mitaani.

2007 kwanza jamiiforums ilikuwa haipo. Nenda zako jamboforums
Naona kuna watu unataka kuwatusi hapo hata waanzilishi wa huu mtandao naona huwaoi heshima yao na hilo ndiyo tatizo la kizazi cha nchi hii.
 
Me nilikuwa bado nuko Bwisya huko visiwani Ukerewe.
Karibu sana ila tukumbe tulikotoka visiwani siku hizi usafiri mzuri tu mpaka Ukara unafika powa tu
 
nyie ndo mnadai jf imepoteza msisimko wakati enz zenu mlikuwa mnapost thread za kitoto..!
Ok powa wewe wa sasa iboreshe kwa kupost mada za maana sasa
 
Hashima kwako MLAU na kwa wengine wa enzi na enzi toka miaka hiyo,
Kila nisomapo posts na comments mbali mbali za wadau enzi hizo mlikuwa mkitoa hoja zenye mashiko sana.

Bahati nzuri ya sasa hivi members wamekuwa wengi, ila bahati mbaya iliyopo kwa wingi huu wa members ni kila iletwapo thread ya maana basi asilimia kubwa ya wachangiaji ni kutema pumba na mashudu tu wachache ndio huchangia points, hakuna tena kubishana kwa hoja kama zamani.
tyc ...umeongea cha maana sana na hiyo ndiyo ilikuwa Jambo Forum 2006 na hatimaye Jamii Forum 2008 ni kweli mada zilikuwa na mashiko sana na mengi tulijifunza na hata mabishano yalikuwa hoja kwa hoja.

Kwasasa nadhani members ni wengi na wengi wanataka kusema ilimradi amesema lakini ni muhimu sana kuchangia jambo kwa hoja inasaidia sana.Kuna umuhimu wa kuwa na reference ya mambo tunayoyatoa au hata uhakika wa jambo lenyewe na sio tu kuandika kwasababu watu wanasema mtaani wakati huna uhakika na jambo lenyewe.
 
Kwa hiyo Mzee umeamua kuongea na madingi wenzio wa JF wa longi; ubaguz
Hakuna ubaguzi kabisa ndugu ndiyo maana na wewe umechangia hapo
 
May be lakini hawawezi kuwa wote
Sie tuliojiunga mwaka 2008 turuhusiwa kuchangia au mpk ifike 2019?

Kila la kheri wakubwa zetu. Tunaithamini michango yenu ya enzi hizo
 
Back
Top Bottom