Men in black + Polisi wa kutosha kwenye msiba wa Kadinali Pengo, Je alikuwa mserikali?

Men in black + Polisi wa kutosha kwenye msiba wa Kadinali Pengo, Je alikuwa mserikali?

TBC wanarusharusha memorizing, huenda baada ya yule waziri kum appreciate kule arusha na kuomba mkutano usimame na ukae kimya kwa daikika moja kumkumbuka kwa mambo mengi aliyolifanyia taifa. Inajulikana kabisa kwamba hawa viongozi wakubwa wa dini/madhehebu ni sehemu ya dola, ndio maana wakiaga dunia serikali hufika fasta msibani kufanya coverage kumzika mwenzao!
 
Sio dini tu hata msanii wa bongo fleva, bongo muvi, muuza madafu, mcheza bao/drafti, mzee wa kijiwe cha kahawa na huko kwenye pombe za mataptapu wakifa serikali huenda kuzika watu wao. Hawa watu huzikwa na serikali kwa heshima zote kulingana na hadhi zao. Kama mtu hajulikani anasali wapi atazikwa tu kwa heshima zote na serikali. Wakijua aliwahi kuwa mkristo watamzika kwa nyimbo na mapambio ya kikristo, hatazikwa kibudu. Kuna watu hujitokeza kuwa wanajua maandika na huchukua jukumu la mchungaji au katekista mradi tu mtu azikwe kwa heshima zote
 
Kuna wachungaji/maaskofu na masheikh wakifa huwa tunaona ushiriki mkubwa wa serikali mpaka tunashangaa kulikoni? Ipo siku hawa mitume na manabii watakapoaga dunia huko nako tutashangaa serikali kujitokeza kwa wingi kuzika mtu wao! Hawa viongozi wa dini ndio wale wamisionari wa ulaya waliotumwa na serikali zao kuja afrika kwa manufaa ya mataifa yao. Sasa hawa ni wamisionari wazalendo, wanatumika na serikali yao kama wale wa ulaya enzi za ukoloni. Kwa hiyo tuna wamisionari wa kizalendo, watu wa serikali. Yale makundi matatu ya kikoloni tunayo, ila ya sasa ni ya kizalendo. Tuna wapelelezi, wafanyabiashara na wamisionari, hawa ni ajenti wa serikali yao kama wale maajenti wa ukoloni
 
Back
Top Bottom