Sio dini tu hata msanii wa bongo fleva, bongo muvi, muuza madafu, mcheza bao/drafti, mzee wa kijiwe cha kahawa na huko kwenye pombe za mataptapu wakifa serikali huenda kuzika watu wao. Hawa watu huzikwa na serikali kwa heshima zote kulingana na hadhi zao. Kama mtu hajulikani anasali wapi atazikwa tu kwa heshima zote na serikali. Wakijua aliwahi kuwa mkristo watamzika kwa nyimbo na mapambio ya kikristo, hatazikwa kibudu. Kuna watu hujitokeza kuwa wanajua maandika na huchukua jukumu la mchungaji au katekista mradi tu mtu azikwe kwa heshima zote