Mende ,Panya na wengineo: Kiumbe gani kikiingia nyumbani/ghetoni kwako unakosa amani kabisa?? Am

I am Groot

JF-Expert Member
Joined
Jul 20, 2018
Posts
3,929
Reaction score
10,747
Salamu kwenu.

Kurudi katika mada; Kusema kweli hakuna mavitu yanayonipa shida akibahatika kuingia ghetoni kwangu kama panya. Yaani nakosa amani kabisa hasa usiku haka kadudu(panya) hakajuagi kutulia kabisa sijui kanamatatizo gani.
 
kwa nguvu nilizonazo ntakuwa mpole kama ataingia simba wa yuda.
 
Panya mbona ni burudani kabisa na usingizi unakuja, aingie nyoka aisee au uvamiwe na kunguni, utageuka mlinzi.
 
Kuna vile vimjusi vyeupe.
Halooo huwa najisikia hadi kichefuchefu.
Hahahaha hao mi nawaona kama mashetani yaani mpaka utumbo unauona
Sikipenda hicho kimyama ingawa hana madhara ila akiingia chumbani ama zake ama zangu
 
Mimi naviogopa hata kuviua sidhubutu yani. Natamani ningepata ujasiri kama wako.
Nilimmalizia dawa ya mbu mpaka nikaanza kukohoa akawa anatambaa kama anacheza break dance lakini alikufa mwisho
Aliingia chini ya kitanda nikasema huyu akiingia kwenye shuka sijui ntatokea wapi.

Kwa kweli ni phobia yangu huyu mdudu
Napenda majoka na wanyama na wadudu ila huyu hapana
Kwnye nyumba au mimi au yeye
 
Haha halafu kikishajua unakiogopa kukibonda kinakuzoea .
Mimi nikikitishia wala hakijigusi yaani.
 
Panya namuogopa
Kunasiku nililala ugenini kushtuka usiku panya huyu ndani ya neti tumelala pamoja
Wew niliruka kama ngedere juu ya mti
Ila sikupata usingizi tena maana mawazo yalienda mbali
Nikijiuliza huyu panya ameingiaje ndani ya net wakat nilichomeka vizur
Asubuh ilipofika jambo lakwanza ilinibid niulize kama humo ndani wanaishi panya watu pia
 
Haha halafu kikishajua unakiogopa kukibonda kinakuzoea .
Mimi nikikitishia wala hakijigusi yaani.
Hahahahaha yaani nyumbani nakumbuka tangu wadogo tulitokea kukiogopa mpaka leo
Naona wanekuzoea kwa upole + uoga haha
 
πŸ˜€πŸ˜€πŸ˜€ unahatari sana mkuu
 
Panya mbona ni burudani kabisa na usingizi unakuja, aingie nyoka aisee au uvamiwe na kunguni, utageuka mlinzi.
Kunguni nae waajabu mno hafagi kizembe zembe watukutu sijawahi kuona. ukiwa nao ndani siku upate ugeni utaiona nyumba chungu. Wanajitokeza kama vile uliwaomba wajitambulishe kwa wageni.
 
Kunguni nae waajabu mno hafagi kizembe zembe watukutu sijawahi kuona. ukiwa nao ndani siku upate ugeni utaiona nyumba chungu. Wanajitokeza kama vile uliwaomba wajitambulishe kwa wageni.
Hahahahahaha eti wajitambulishe
Kama namuona katibu kata kimbelembele na balozi wa nyumba
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…