Mene, Mene, Tekeli na Peresi": Maandishi Ukutani Kuhusu Nyufa na Ugomvi wa Ndani ya CCM

Ni jambo Jema, na huenda limechelewa saaaana.

Mpasuko ndiyo maendeleo halisi.

Hofu yangu, je mapapa nguli na mafisadi yatakubali kuachia rasilimali zetu au yataendelea kuuwa na kuteka ili kulinda walivyopora kwa nguvu ????? !!!!!
 
Kuendelea kumshikilia Lissu mtima nyongo utawasambaratisha wale makada wa chama tawala, ni bora wamuachie ili mjuba Lissu akiwa nje wanakuwa pamoja kumkabili. Sasa hawana pa kuelekeza nguvu zao inabidi zitumike kusambaratishana wao kwa wao. Tena ni wakati wa kuelekea kupata mgombea mpya watatifuana sana wale, Lissu atawaunganisha wakitetee chama chao kwa pamoja
 
Hata humu Jf, Mwashambwa=Nvhimbi!
Tlaatlaah=Nchemba!
 
Mbogamboga wanaogopa sana baridi ya nje ya mfumo tawala. Hata wapige kelele vipi chinichini, at the end of the day, hakuna mwenye ubavu wa kuanzisha CCM B au kukimbilia upinzani. Wote watarudi mstari mmoja!
 
Mimi ni mwana CCM wa siku nyingi , lakini sasa hivi CCM ni chama cha maslahi binafsi.
Chama ambacho sasa ni sehemu ya dola.
Hata ndani ya CCM hakuna demokrasia.
 
Ntachelewa sanaaa sanaaa kuamini kua mvutano huu utakua na chochote cha maaana kwenye mkwamo huu wa kisiasa,kiuchumi na kijamii tulionao.

Mboga mboga linapokuja swala la chama cha kushika dora, huwa tofauti zao wanaziweka pembeni. Huwa hawajali nani atakua rais.kitu pekee wanajali ni chama kushika hatamu.
 
Tena ni wakati wa kuelekea kupata mgombea mpya watatifuana sana wale, Lissu atawaunganisha wakitetee chama chao kwa pamoja✍🏿
 
Naunga mkono hoja Je, kesho ndio siku "Mene Mene Tekeli na Peresi!" ya CCM?
P
 
Bado mnayo matumaini ya wao kufika 2030?
Kweli watu mnayo imani ya kushangaza sana!

Ni muujiza wa kipekee sana utakaomfikisha Samia 2030.
 
Ni jambo Jema, na huenda limechelewa saaaana.

Mpasuko ndiyo maendeleo halisi.

Hofu yangu, je mapapa nguli na mafisadi yatakubali kuachia rasilimali zetu au yataendelea kuuwa na kuteka ili kulinda walivyopora kwa nguvu ????? !!!!!
Kwani yataendelea kumiliki DOLA?

Watainunua DOLA na kuendelea kuitumia vile vile kama ilivyokuwa inaendeshwa kwa niaba yao na kundi la Samia?

Siamini kuwa hao mafisadi yatahamishia uteja wao kwa timu mpya itakapoingia. Inachukuwa muda kujenga uhusiano huo, hiyo siyo kazi ya haraka mara moja!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…