Meneja Afrika Mashariki: Bolt inaweza kusitisha huduma Tanzania

Hiki unachofanya ni spamming na haijawahi kuwa njia ya marketing. Badala liwe tangazo sasa linakuwa kero, unarudiarudia
 
Ndio mkuu....
Hii serikali ni ya kinyonyaji mnoo, kila sehemu wanapiga pini, na hii yote ni kwa sababu wao wanakula kiubua hawajui gharama ya mafuta wala vyakula. Wao vitu vingi free, bado mshahara mkubwa, posho kede kede, nyumba za serikali.

Kama sisi tusipofanya jambo basi tumekwisha.
 
Jitangaze mkuu, upate wateja.
Napenda kuwasapoti wazawa.
 

Uber na bolt hawataki 15% wanataka 20-25% ambayo madereva wanaipinga tusubiri kuona yajayo
 
Kwa hiyo anayeumia bado ni mlaji.
Ukiwa na app ya Uber au bolt hata ukienda nje ya nchi huhitaji kuwa na account nyingine. Kwa kuwa hizi kampuni zipo nchi nyingi ndio maana wanakuwa na nguvu.
Athari itakuwa kwa wageni wanaoingia nchini maana itabidi wapakue app za mskampuni ya nyumbani.
 
Hizi sheria ziliachwa na yule jamaa, mama kaachiwa jumba bovu, naamini anasikiliza ataondoa hio makato ili atengeneze ajira
Kama alivyoachiwa Jumba Bovu la Kuunganishwa umeme Laki Tatu yeye akashusha mpaka 27,000/=
 
Sahihi kabisa, Madereva kazi yao pia ni kuangalia mashahi yao, vp kuhusiana na maslahi ya mteja ambayo bolt ameamua kuyalinda kwa kuhakikisha nauli haziwi ghali?
 
Umeangalia pia na kipato cha mlaji au mnaangalia tu maslahi binafsi?
 
Sahihi kabisa, Madereva kazi yao pia ni kuangalia mashahi yao, vp kuhusiana na maslahi ya mteja ambayo bolt ameamua kuyalinda kwa kuhakikisha nauli haziwi ghali?

Yaah tatizo pia bolt hataki kushusha commission yake to 15%
 
25 wanaokula hao mabeberu ni ya kichonyaji haswa 15 sahii kbsa hawataki linkii ipo au serekali ianziehe udumu yake au latra wenyewe waanzishe site yao
 
Yaah tatizo pia bolt hataki kushusha commission yake to 15%
Pengine akishusha chini ya hiyo percentage anaweza shindwa lipa wafanyakazi wake pamoja na kumudu gharama mbalimbali za kiuendeshaji, na mwisho wa siku aweze kupata decent profit ambayo ni malipo ya efforts zake- Tatizo bongo tunataka slope sana- Katuachia zaidi ya 85 percent lakini bado serikali na madereva wanataka yote- Investor lazima aondoke hata kama ingekuwa mm 🤣 🤣
 
Nina wazo: Kama serikali inawapenda sana madereva na inataka kuwasaidia basi watengeneze na ku-manage Application kama ya Bolt ambayo madereva wote wataitumia kwa bei wanayoona ni rafiki hata ikiwezekana iwe bure. Au madereva wajiunge watengeneze app yao na wapange management fee wanayodhani itawafaa.
 
Wamezoea dezo.... walipe kodi stahiki...
 
Sasa Latra anaingiliaje wakati hayo ni makubaliano baina ya makampuni na wenye magari? Kama mwenye gari anaona hapati kitu si anaacha makampuni yanaendelea na wenye magari walio tayari!
 

Bolt hajaacha iyo percentage iyo percentage ndio amegomea bolt anachukua 20 na uber alikua anachukua 25
 
BADO NI BIASHARA HURIA ILA LAZIMA KUWE NA REGULATORS WA BEI HAKUNA UHURU BILA SHERIA, UHURU LAZIMA UJUE UNAANZIA WAPI NA UNAISHIA WAPI. INGEKUWA HIVYO HATA DALADALA WANGEKUWA WANAJIAMULIA TU NAULI ZAO SABABU NI BIASHARA HURIA MKUU.
Sikia Watanzania ambao bado mnawaza kijamaa. Kama hiyo bei ni realistic kwa nini wasiwaache wanaoweza washushe ili abiria na madereva wahamie kule?

Tanzania tungekuwa tunatoa incentives kwa locals tungekuwa na makampuni strong area hiyo na yangeshusha bei kama hio rate ni reasonable na haya makampuni automatically yangefunga bila kelele au yangeshusha pia.

Unaweza ku control sheria bila kuweka mkono moja kwa moja!
 
Kabisa homeboy haujakosea. Kuna watu wa ajabu sana serikalini.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…