Meneja Afrika Mashariki: Bolt inaweza kusitisha huduma Tanzania

LATRA wako sahihi, asilimia 20 anayochajiwa dereva ni nyingi, angalau hiyo 15 inakua fair kiasi. Labda iwe asilimia 20 na nauli itabidi ipande zaidi.
Unajua mambo mengi ni upuuzi na kukosa shukrani.

Hao bolt na Uber ni makampuni binafsi ambayo waanzilishi wake walikuja na idea ya watu binafsi kutumia magari yao binafsi kujipatia passive income na sio kuajiri madereva tax na kuwapa mishahara. Hata ukisoma utambulisho wa wamiliki wa hizi apps utaona wanakuelezea idea yao ni very simple,haijakaa kimambi mengi. Ni simply a hobby thing na sio Career au fulltime job or occupation ingawa wewe ukitama iwe hivyo ni sawa but according to u personally sio according to them.

Haya mashirika si mashirika ya uma au ya serikali kusema hawa madereva wana haki ya kuwacontrol kwa lolote lile.

Its a free economy and tuna expect forces of Demand and Supply ndizo zitafanya kazi yake. Inasikitisha sana tena sana mamlaka ya kiserikali kama Latra kuamua kuyapangia haya mashirika ambayo kimsingi serikali nadhani walitakiwa kuyapa kila aina ya support sababu yamesaidia serikali kuwapatia raia kipato cha ziada katika uchumi huu wa ajira chache na mishahara finyu.

Hivi haya makampuni yakifunga biashara na kuondoka serikali na hawa madereva wa hizo gari watapata nini zaidi ya kurudi nyuma mara dufu maana hizo gari hazitakuwa na kazi tena kibiashara na mapato yaliyokuwa yakipatikana yatatoweka.

Kwann serikali huwa inaingilia mambo na kuyaharibu kisha wanajifanya wao ndio wanakuja kutoa msaada wakati wao ndio chanzo.

Sasa unalalamika bolt au uber kuchukua hiyo 20% hivi kubabako wewe na hiyo serikali yako ya CCM mlishawahi kuja na wazo gani ambalo linaweza kuwapatia kipato cha 80% kama hicho mnacholalamikia.

Shida hapa sio Uber na Bolt bali shida ni serikali na hawa madereva wasiojua mchawi ni nani.

Mtu anakupa deal halafu yeye katika kipato anachukua 20% anakuachia 80% then unasema anakunyonya. Aisee hivi mtu unatakiwa kuwa selfish kiasi gani. Hii 80% inatafunwa na serikali ndio maana haonekani kuwa ina faida. Hebu wazia bei za mafuta, gharama za vipuri, service za gari, vibali, tiketi za matrafiki, bima ya gari, hela ya m'miliki wa gari. Hivi vyote ndivyo vinakamua faida ya huyu dereva na si hawa makampuni.

Mbona watu ambao wanamiliki magari yao binafsi na wanafanya hizi vitu huwezi sikia wanalalamika sana sababu hawana mahesabu kama ya hawa madereva wanaopewa magari kimkataba na wamiliki.

Sasa leo watu wachache wasiokuwa na shukurani wala akili wanaona bora kampuni ifungwe kila mtu akose kulikoni wangeacha kampuni zifanye biashara kwa mujibu wa kanuni za soko huria.

Kama mtu hautaki au unaona unanyonywa simply futa tu hiyo app achana nayo weka app ya CCM wakupe abiria na wakukate hiyo 15% maana wao ndio wanajua sana biashara na si Uber na bolt.

Kila kukicha mnalalamikia uwekezaji mzuri Tanzania ambao hauwagharimu rasilimali zenu , mnaupata kama huu mnaleta ufala. Ila wakija wawekezaji wanapiga madini, mawe mafuta gesi wala hatuoni kama hapo tunanyonywa. Ila huyu ambaye anakupa mchongo kwa kutumia technology mnamuona mnyonyaji.

Aiseeeeeee hii inchi ina ufala mwingi sana. Wacha jamaa wakimbilie nchi zingine wanazojielewa. Mtu anakupa lift unampangia ruti ya kupita.
 

Njia muafaka ya kusuluhisha haya mambo ni kuwa na ushindani kwenye hizi apps.
 
Hivi Uber na Bolt nao ni wawekezaji? Wamewekeza nink Tanzania? Hawa ni kama madalali tu.

Hawa ni wanyonyaji. Hebu fikiria, huna gari, hulipi dereva, hununui mafuta, hulipii matengezo ya gari, halafu uchukue 25% kwenye nauli...siyo faida ila nauli ghafi.

Operational cost zao zikoje?
 
Bolt na Uber wanaigomea vip Gvt kwa commmissions ya 15% kila trip wao ni wamiliki wa software tu gharama zote kodi Bima ya laki 7 tozo mafuta repair and maintenance mshahara wa dereva zinakwenda kwa mmiliki wa gari .
Mod unganisha huu uzi wa Bolt na Uber
 
Hizo list ya gharama umetaja hapo ni regulations za serikali yako. Hizo ndizo zinakula faida na malengo ya watu wanaojihusisha na Uber na bolt. Wasingeweka ma regulation cost ya kipuuzi hiyo kitu ingewafaa sana vijana kupunguza makali ya maisha.

Uber sio biashara rasmi kama TAXI. Uber ni passive income gig app.

Serikai ya Tanzania sababu ya kukosa ubunifu na uwezo wa kuwatengenezea mifumo ya ajira vijana wake wanageuza vitu ambavyo sio official kuwa official employment.

Ni aibu. Ndio maana juzi Lema akawachana kuwa umachinga, bajaji na bodaboda si jambo la serikali kuhesabia kama ni ajira ramsi kwa taifa sababu hakutakuwa na future nzuri kwa vijana wetu.

Hizi ni shughuli za kufanya kujipatia passive income na sio ajira rasmi.
 
BADO NI BIASHARA HURIA ILA LAZIMA KUWE NA REGULATORS WA BEI HAKUNA UHURU BILA SHERIA, UHURU LAZIMA UJUE UNAANZIA WAPI NA UNAISHIA WAPI. INGEKUWA HIVYO HATA DALADALA WANGEKUWA WANAJIAMULIA TU NAULI ZAO SABABU NI BIASHARA HURIA MKUU.
Uhuru upo. Nani ana regulate bei ya ndizi, n.k.? Sema tu kwenye suala la vyakula suppliers wapo wengi.
 
LATRA wako sahihi, asilimia 20 anayochajiwa dereva ni nyingi, angalau hiyo 15 inakua fair kiasi. Labda iwe asilimia 20 na nauli itabidi ipande zaidi.
Mi sijaifahqmu vizuri hii habari. Wana regulate commissions ama wanataka ku regulate fares? Yaani tusema wao wanataka kufanya kilakilomita pengine ni elfu 1?
 
Uhuru upo. Nani ana regulate bei ya ndizi, n.k.? Sema tu kwenye suala la vyakula suppliers wapo wengi.
Kwani mafuta suppier ni mmoja, usafiri je ? lakini hao wote wanapangiwa bei elekezi mkuu hata kwa Bolt na Uber lazima wawekewe bei elekezi
 
Uhuru upo. Nani ana regulate bei ya ndizi, n.k.? Sema tu kwenye suala la vyakula suppliers wapo wengi.
Kwani mafuta suppier ni mmoja, usafiri je ? lakini hao wote wanapangiwa bei elekezi mkuu hata kwa Bolt na Uber lazima wawekewe bei elekezi
 
Sahihi kabisa hasa ukichukulia bei za mafuta vipuli na hata atitude za baadi yetu a abiria utakuta mtu anaita bolt inafika anamuweka mtu mpk dk 20 afu hio haiesabiwi au anarequest unafika anacancel umbali iluotoka mafuta uliotumia vyote havina maana kwa bolt hawakucompesate kwa lolote shida ni nyingi na jamaa wamepiga hela kinoma unakuta gari mpya mpk inachoka huna lolote hawa latra pamoja na udhaifu wao mwingi wapo sahihi ktk hili
 
Na hii spamming hapa jf ndio marketing strategy yenu?
 

Uber katoka, bolt nae akitoka hakuna kampuni itakayo survive hapa Tz , unless iwe ni mpango wa kigogo fulani kashakula hela sasa anataka kuleta app yake ifanye kazi bila competitor yoyote!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…