Meneja Mawasiliano MWAUWASA katoa taarifa ya uongo kuhusu kutokuwepo tatizo la maji jijini Mwanza

Meneja Mawasiliano MWAUWASA katoa taarifa ya uongo kuhusu kutokuwepo tatizo la maji jijini Mwanza

Ruhuta

New Member
Joined
Jul 2, 2024
Posts
3
Reaction score
1
Wananchi wa mkoa wa Mwanza hususani wilaya ya Ilemela na Nyamagana tunapitia katika kipindi kigumu cha upatikanaji wa huduma ya maji licha ya mradi mkubwa wa uzalishaji maji kata ya Butimba kukamilika na kuanza kutoa huduma.

Baada ya malalamiko kua makubwa amejitokeza meneja wa mawasiliano wa Mwauwasa na kueleza Mwanza hakuna tatizo la maji,taarifa aliyotoa imejaa uongo,unafiki,kujipendekeza na kuficha tatizo ambalo linazidi kua sugu.

Mimi ni mkazi wa Ilemela kata ya Buswelu jirani kabisa lilipojengwa tank kubwa linalopokea maji kutoka mradi wa Butimba, wakazi wa Buswelu yapata wiki na nusu sasa hatupati maji licha ya kuishi jirani na tank achilia mbali ziwa victoria.

Baada ya kufatilia tatizo hili, mamlaka ya maji Mwanza walidai kua shida hiyo inasababishwa na myumbo wa umeme uliopo eneo la buswelu na baada ya majibu hayo tulifanya ufatiliaji Tanesco kujua shida ya myumbo wa umeme buswelu inatokana na nini hadi kutufanya tukose maji.

Hata hivyo Tanesco wamekana tatizo hilo na kudai umeme wao upo stable hawana shida yoyote ya myumbo wa umeme eneo la Buswelu.

Kwa hivyo Mwauwasa umeme wanao, maji ya ziwa victoria wanayo,mitambo mipya na ya kisasa ya kusukuma maji wanayo, matank ya kupokea maji wanayo lakini wameamua kutunyima maji wanachi ili tuteseke.

Meneja mawasiliano Mwauwasa tuombe radhi wakazi wa Mwanza na mtoe huduma.
 
Labda alimaanisha kwake.
Kwakuwa kwake anaona maji yapo anadhani jiji lote la Mwanza Lina maji
 
Nahitaji kujua ni maeneo yapi hapa Mwanza iwe Wilaya/Kata au kijiki/mtaa ambalo hawajafikiwa kabisa na huduma ya maji ya mamlaka na watu/wakazi wake wanatumia maji ya kisima, mito au maziwa. Nahitaji hii Kwa ajili ya utafiti wa kielimu.
 
Back
Top Bottom