Waufukweni
JF-Expert Member
- May 16, 2024
- 5,383
- 18,776
Kamati ya Mpira wa Miguu wa Wanawake ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) katika kikao chake kilichopita taarifa za mechi za Ligi Kuu ya Wanawake imemfungia Meneja wa Simba Queens, Selemani Makanya kwa miezi 6 na kumpiga faini ya TSh 1.5 Milioni kwa kosa la kuwashambulia Waamuzi baada ya mchezo wa Ligi Kuu Wanawake uliochezwa kwenye uwanja wa Meja Jenerali Isamuyo kati ya Simba Queens dhidi ya Mashujaa Queens ulioisha kwa sare ya 2-2.
Soma, Pia:
www.jamiiforums.com
Uamuzi huo umezingatia Kanuni ya 47(3) ya Ligi za Wanawake.
Pia, Kocha Msaidizi wa Simba Queens, Mussa Mgosi amefungiwa mechi tatu na kutakiwa kulipa faini ya TSh. 1,500,000 (milioni moja na nusu) kwa kuzingatia Kanuni ya 46(2) (1) ya Ligi za Wanawake.
Soma, Pia:
√ - Tukio la viongozi wa Simba Queens kuwashambulia waamuzi baada ya Sare na Mashujaa Queens halivumiliki, mamlaka zichukue hatua
Wakuu! Hii haikubaliki Mechi ya Ligi Kuu ya Wanawake kati ya Simba Queens na Mashujaa Queens hapo jana (Mei 12) ilizua taharuki baada ya kumalizika kwa sare ya mabao 2-2. Baadhi ya Viongozi wa benchi la ufundi, Simba Queens walianzisha vurugu na kuwavamia waamuzi, wakipinga baadhi ya maamuzi...