Meneja TANESCO Arusha kazi imekushinda

Gerad2008

JF-Expert Member
Joined
Jun 9, 2009
Posts
583
Reaction score
287
Tangu Jumapili tarehe 10/7/2011 hadi leo Jumatano jioni TANESCO Arusha imeshindwa kuwapatia umeme wakazi walioko maeneo ya Kijenge yote(chini na juu), Kimandolu na maeneo yaliyoko barabara ya Moshi yaani Tengeru, Usa river, Maji ya Chai, Kikatiti, KIA hadi Mererani.

Katika mgawo wa umeme unaoendelea mkoani hapa TANESCO imekuwa ikikata umeme masaa zaidi ya 20 na wanarudishiwa kwa masaa 3, au saa 1 au dakika 5 na kukatwa tena kana kwamba tayari zamu yao ya kupata umeme imepita:

Kwa mfano:

Jumapili 10/7/2011

Maeneo ya Kimandolu tulikuwa tupate umeme kuanzia saa 2 asubuhi hadi saa 12 jioni lakini umeme ulirudi kama ifuatayo:
Kuanzia saa 2:15 asubuhi hadi saa 4:50 na ulikatwa ukarudi saa 7;15 na ukakatwa baada ya dakika 5 then ukarudi saa 9 na ukakatika tena na kurudi saa 10 na ilipofika saa 12 kamili TANESCO walikata umeme rasmi na kuhesabu kuwa zamu ya eneo hilo imepita.

Jumatatu 11/7/2011

Umeme ulirudi saa 9 Usiku na kukatika saa 2 asubuhi: TANESCO ilirudisha umeme saa 12 jioni na kuukata saa 4:30 usiku hadi asubuhi.


Jumanne 12/7/2011

Siku ya jumanne tulikuwa tupate umeme mchana kutwa kuanzia saa 2 asubuhi lakini TANESCO iliwasha umeme saa 2 asubuhi na ikakata umeme saa 3 asubuhi (yaani Kimandolu ilipata umeme saa 1 tu kwa siku nzima kati ya masaa 12).

Jumatano 13/7/2011

Leo Jumatano umeme ulirudishwa saa 9 usiku na ukakatwa saa 2 asubuhi. Kutokana na ratiba leo jioni siku ya Jumatano Kimandolu na maeneo ya hapo juu yalitakiwa yapate umeme kuanzia saa 12 jioni lakini TANESCO imerudisha umeme kwa dakika 5 tu na kuukata (yaani kuanzia saa 12:15 hadi saa 12;20). Hadi ninapoandika haya malalamiko ya umeme hauna mwelekeo wa kurudi.

Nataka Meneja wa TANESCO aelewe kwamba tangu jumapili huku Kimandolu na Kijenge watu hawasagi mahindi, hawakoboi mahindi, hawapasui mbao na wala hakuna grill zimetengenezwa. Cha ajabu maeneo mengine yanapewa umeme kwa upendeleo kama mjini , uzunguni na maeneo wanayoishi hawa jamaa wa TANESCO.

Hivi inakuwaje TANESCO inarudisha umeme kwa saa 1 au dakika 5 tu na kuukata tena kwa masaa 12 bila compensation au kueleza kulikoni wakati maeneo mengine umeme ukiwashwa unakaa masaa 8 hadi 10?. Kwa maelezo hayo hapo juu na tathmini ya kawaida tu inaonyesha MENEJA WA TANESCO ARUSHA AMESHINDWA KAZI NA awe tu muungwana asalimu amri kwa sababu ni dhahiri kazi imemshinda.

Nimwulize swali rahisi tu" HIVI UNAPORUDISHA UMEME SAA 8-10 USIKU NA KUUKATA ASUBUHI WAKATI WATU WAMELALA UNAMSAIDIA NANI?
KWA NINI TANESCO ISIRUDISHE UMEME KUANZIA SAA 1 ASUBUHI THEN WAUKATE SAA 6 MCHANA ILI WATU ANGALAU WAUTUMIE KUFANYA SHUGHULI ZAO ZA UZALISHAJI?

Huyu Meneja akiendelea kuwepo kuna uwezekano wa Kimandolu ,Kijenge na maeneo niliyoyataja kukosa umeme hata wiki nzima bila yeye kujisikia vibaya .
 
kweli mkuu wife yupo njiro jtatu walikata wakarudisha jtano usiku. nchi hii uozo mtupu hapa navyoandika niko gizani
 
Ndg yangu! Hakika ni kwmb cna mamlaka kwani huyu asingekuwepo ofisini. Ila hakika hawa wote walioko ngazi yote ya juu watashukaga tu.
 
Meneja wa TANESCO Arusha ameshindwa kusimamia mgawo wa umeme kwa haki badala yake kutoa umeme kwa kuwapendelea maswahiba wake. Mimi nashukuru gerad kuwa umefafanua vema ni kweli huku hali ni mbaya tangu jumapili watu wenye mashine tangu jumapili hawajaweza kuingiza kitu. Mbaya zaidi mtu anaogopa kuwasha hata mashine kwani umeme unawashwa kwa dakika chache then unazimwa na hapo inakuwa imetoka na wao TANESCO wanahesabu wamewapatia umeme.
 
kweli mkuu wife yupo njiro jtatu walikata wakarudisha jtano usiku. nchi hii uozo mtupu hapa navyoandika niko gizani

Bora wangekuwa na ratiba inayoeleweka ila tatizo TANESCO hapa Arusha wanafanya mambo ya Kijiweni kwani ratinba inabadilika kila siku na hata pale umeme unarudishwa ni kama suna. Hivi umeme ulikokatwa kwa siku nzima ukarudishwa kwa dakika 5 au saa 1 unasaidia kitu gani. huyu meneja inawezekana ni mtu wa kinywaji na jioni anakuwa amelewa kwani katika hali ya kawaida na kwa mtu ambaye ana akili timamu hawezi ku abuse binadamu wenzake kwa kiwango cha hali ya juu namna hii. Huku ni kudharau wateja na ni kukosa huruma na utu.
 
haya maandishi hayasaidii hapa kama wananchi wamechoshwa basi waingie mtaani. Hii ni haki yao ya msingi.
 
haya maandishi hayasaidii hapa kama wananchi wamechoshwa basi waingie mtaani. Hii ni haki yao ya msingi.

Uko sawa kabisa tatizo la watanzania tunakosa VOLUNTEER WA ku-organize watu na akipatikana itatakiwa kila mkoa apatikane ili maandamano kila mkoa yafanyike siku moja ili Polisi wazidiwe nguvu. Tukifanya Arusha tu watakodisha polisi Moshi, Manyara na Tanga na watatushinda ila tukifanya nchi nzima kwa siku moja na masaa yanayofanana hata magari ya kurusha maji hayatatosha na tutakuwa tumefikisha ujumbe kwamba " YES WE CAN" na hapa discipline itaanza kuonekana.
 


Wananchi tunatakiwa tuunde chombo cha KUTUUNGANISHA AMBACHO HAKINA POLITICAL AFFILIATION kiwe na ofisi kila mkoa ili kuwahamasisha wananchi kudai haki yao haswa katika kipindi hiki ambacho nchi inapeperushwa na upepo badala ya kuongozwa na watu. Katika chombo hiki ni rahisi watu kuhamasishwa kukutana na kutembea kwa miguu wakitoa madai yao kwa njia ya amani kila mkoa na hapa serikali inaweza ikaanza kushtuka.

Kwa sasa nchi iko mikononi mwa wakoloni wa ki-Tanzania na sisi ni watawaliwa hivyo tunatakiwa tudai uhuru wetu
 
Mkuu umeongea kitu ambacho ni cha muhimu sana adimu ambacho wengi bado hatujashtukia na ndiyo maana tunapelekwa sana na wana siasa na kutupeleka kulingana utashi wao Maana mgao sasa umefikia mpaka masaa 30 kitu ambacho huo sio mgawo tena tuambiane u kuwa nchi ipo gizani tutaelewa.Ila mkuu Gerald 2008 umepotea sana na sijui umejichimbia wapi!
 
tumeambiwa tatizo ni mabomba ya songas

walianza na mvua, ikaja matengenezo, ikaja dowans, ikaja IPTL sasa ni mabomba..........

Tulia mwana, wa arusha ni mdogo sana tu kwenye hili sakata la umeme, kama huamini tuulize tuliokua uwanja wa taifa jumapili
 


Mkuu tunacholalamika hapa siyo kuwa mgawo usiwepo ila basi uwe organized kuliko kufanya vituko vya kuwasha umeme kwa dk 5 au saa 1 na kuzima masaa 20.

Mgawo ueleweke unakwendaje na si watu wanasubiri zamu yao then ghafla umeme unawashwa saa 1 unakatwa na hapo zamu yenu inakuwa imeisha. Huu ni uhuni mkubwa tu.
 

Mkuu Derimto nipo in and out ila bado nipo hapa hapa A town ni majukumu yamenikaba tu ndugu yangu. Ni na amini tukiweza kuji-mobilize kama Watanzania ni rahisi kuleta changes zikiwamo za kuwa ondoa watendaji wabovu kama huyu Meneja wa TANESCO Arusha.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…