Gerad2008
JF-Expert Member
- Jun 9, 2009
- 583
- 287
Tangu Jumapili tarehe 10/7/2011 hadi leo Jumatano jioni TANESCO Arusha imeshindwa kuwapatia umeme wakazi walioko maeneo ya Kijenge yote(chini na juu), Kimandolu na maeneo yaliyoko barabara ya Moshi yaani Tengeru, Usa river, Maji ya Chai, Kikatiti, KIA hadi Mererani.
Katika mgawo wa umeme unaoendelea mkoani hapa TANESCO imekuwa ikikata umeme masaa zaidi ya 20 na wanarudishiwa kwa masaa 3, au saa 1 au dakika 5 na kukatwa tena kana kwamba tayari zamu yao ya kupata umeme imepita:
Kwa mfano:
Jumapili 10/7/2011
Maeneo ya Kimandolu tulikuwa tupate umeme kuanzia saa 2 asubuhi hadi saa 12 jioni lakini umeme ulirudi kama ifuatayo:
Kuanzia saa 2:15 asubuhi hadi saa 4:50 na ulikatwa ukarudi saa 7;15 na ukakatwa baada ya dakika 5 then ukarudi saa 9 na ukakatika tena na kurudi saa 10 na ilipofika saa 12 kamili TANESCO walikata umeme rasmi na kuhesabu kuwa zamu ya eneo hilo imepita.
Jumatatu 11/7/2011
Umeme ulirudi saa 9 Usiku na kukatika saa 2 asubuhi: TANESCO ilirudisha umeme saa 12 jioni na kuukata saa 4:30 usiku hadi asubuhi.
Jumanne 12/7/2011
Siku ya jumanne tulikuwa tupate umeme mchana kutwa kuanzia saa 2 asubuhi lakini TANESCO iliwasha umeme saa 2 asubuhi na ikakata umeme saa 3 asubuhi (yaani Kimandolu ilipata umeme saa 1 tu kwa siku nzima kati ya masaa 12).
Jumatano 13/7/2011
Leo Jumatano umeme ulirudishwa saa 9 usiku na ukakatwa saa 2 asubuhi. Kutokana na ratiba leo jioni siku ya Jumatano Kimandolu na maeneo ya hapo juu yalitakiwa yapate umeme kuanzia saa 12 jioni lakini TANESCO imerudisha umeme kwa dakika 5 tu na kuukata (yaani kuanzia saa 12:15 hadi saa 12;20). Hadi ninapoandika haya malalamiko ya umeme hauna mwelekeo wa kurudi.
Nataka Meneja wa TANESCO aelewe kwamba tangu jumapili huku Kimandolu na Kijenge watu hawasagi mahindi, hawakoboi mahindi, hawapasui mbao na wala hakuna grill zimetengenezwa. Cha ajabu maeneo mengine yanapewa umeme kwa upendeleo kama mjini , uzunguni na maeneo wanayoishi hawa jamaa wa TANESCO.
Hivi inakuwaje TANESCO inarudisha umeme kwa saa 1 au dakika 5 tu na kuukata tena kwa masaa 12 bila compensation au kueleza kulikoni wakati maeneo mengine umeme ukiwashwa unakaa masaa 8 hadi 10?. Kwa maelezo hayo hapo juu na tathmini ya kawaida tu inaonyesha MENEJA WA TANESCO ARUSHA AMESHINDWA KAZI NA awe tu muungwana asalimu amri kwa sababu ni dhahiri kazi imemshinda.
Nimwulize swali rahisi tu" HIVI UNAPORUDISHA UMEME SAA 8-10 USIKU NA KUUKATA ASUBUHI WAKATI WATU WAMELALA UNAMSAIDIA NANI?
KWA NINI TANESCO ISIRUDISHE UMEME KUANZIA SAA 1 ASUBUHI THEN WAUKATE SAA 6 MCHANA ILI WATU ANGALAU WAUTUMIE KUFANYA SHUGHULI ZAO ZA UZALISHAJI?
Huyu Meneja akiendelea kuwepo kuna uwezekano wa Kimandolu ,Kijenge na maeneo niliyoyataja kukosa umeme hata wiki nzima bila yeye kujisikia vibaya .