Meneja TANESCO Mlandizi unahujumu juhudi za Rais wetu mpendwa

Meneja TANESCO Mlandizi unahujumu juhudi za Rais wetu mpendwa

Ndugu ama kwa kujua au kwa kuto kujua wewe na wasaidizi wako mna hujumu juhudi za Mhe.rais wetu za kutaka Tanzania kuwa nchi ya viwanda na uchumi wa kati na hasa mnatuumiza sisi watanzania wakawaida tulioitikia kwa vitendo juhudi za rais wetu.Tanesco Mlandizi mna matatzo makuu matatu.

1.KUKATA UMEME HOVYO
Pamoja na Tanesco mahali kwingine kusifiwa kuondoa mgao au kupunguza kabisa tatizo la ukataji umeme hovyo hili kwetu mlandizi bado lipo na ni la hovyo kwa sababu unakatika kwa vipindi vipindi pasipo taarifa karibuni kila siku mlandizI umeme unakatika kwa vipindi vya dk tano tano na kurudi na kunasiku tunaenda masaa 10 mpk 18 bila umeme jambo linalopelekea watu kuunguza vifaa vyao vingi vinavyotumia umeme na kuingia hasara shughuli kama saloon na viwanda ambavyo kwa sasa vipo vingi mnoo mlandiz n changamoto uendeshaji wake kuna tatizo gani mkitupa taarifa kuwa mtakata umeme mbona ofisi zingine wanatoa taarifa kwenye mitandao ya kijamii na kwenye vyombo vya habari kama redio na tv ninyi mlandizi mnatatizo gani ? basi igeni hata wenzenu wa DAWASCO wanaopitaga wakitangaza mitaani na gari zao maana cruiser zenu zinapark tu pale kauli ya bibi mida ya kazI

2.HUDUMA KWA WATEJA PIA NI MBOVU
Nimetembelea ofisi yako karibuni mara 7 nimepata nafasi ya kusign kama mgeni mara moja tena baada ya kugombana sana mnapata wapi reference kwa wateja wanaokuja pata huduma maana mlinzi anakuuliza maswali mengI mnoo na hata mkimaliza ulizana hakupi daftari la kusaini mteja unakosa reference ya hata kwamba ulikuja mara ngapi kueleza tatzo hilo hilo moja ukiingia ndani napo kuna wadada wale wa front office pale nao ni balaa nimemshuhudia mara 2 nzima yule dada mwenye asili ya kiarabu akiwafokea wateja badala ya kuwaeleza na kuna mdada mmoja anapenda kuwa zamu jmosi (natumia neno anapenda maana kila siku ni yeye tu na unamkuta busy na simu) nilimshuhudia akimwambia mzee mmoja kuwa sio muelewa na watu wengi wamekuwa wakiwalalamikia hawa watu wako wa front office.

(b) Takriban ofisi zote kuanzia DAWASCO, TRA hata TANESCO sehemu zingine wanatoa huduma siku ya jumamosi mpk saa sita mchana na huduma huwa ni kama zinazotolewa siku zingine tofauti n muda ila kwa mlandiz mnakuwa na dawati la emergency tu nadhan kuongeza ufanisi mngetoa pia baadhi ya huduma kwa siku ya jumamosi kwa hayo masaa machache wengine wanaweza ninyi mnashindwa wapi ?

3.HARUFU YA RUSHWA
inasemekana kitendo cha wale walinzi kuuliza maswali mengi na kutokutoa daftari la wateja kusign kama wageni ni kuwa baada ya kukuuliza huwa wanashauri uchukue namba za watu flan flan ili mteja akamalizane nao nje ya ofisi (sina hakika ila maswali wanayouliza wale walinzi ni kama wanamaelekezo flani)

Nina tukio ambalo na uhakika nalo kwa wakazi wa kisabi block C ambao walikuwa wapate umeme wa REA kwa mabavu ww na washiriki wako mmeupeleka mradi kijiji cha jirani cha madimla na kisabi block C zimepita tu nguzo huku nyumba kama nne tu wakiwa wamepata na walipokuja ulizia ofisi yako ilijibu hujakabiziwa bado mradi na REA ila kwa wanaitaji umeme kama wale wanne waliopata watengeneze mazingira rafiki ...
Tunaomba TANESCO na TAKUKURU mchunguzeni huyu bwana
Ndugu mpendwa mteja wetu

Tumesoma maelezo yako kwa kina, Awali ya yote tunakuomba radhi kwa adha yeyote uliyodai kupitia.

Uongozi wa TANESCO Makao Makuu umechukua swala hili kwa uzito mkubwa na umepanga kukutana na wewe na kusikiliza upande wa pili kwa lengo la kuboresha zaidi, Hivyo tusaidia namba yako ya simu kwa hatua zaidi

Majibu ya hoja zako

1.Kutotoa taarifa. shirika limejitahidi sana kutoa taarifa za makatizo yaliyopangwa au yatokanayo na hitilafu kupitia vyombo vya habari mbalimbali, magari kupita mtaani na mitandao ya kijamii.Hapa tunaomba namba yako yenye WhatsApp kwa taarifa zaidi

2.Kuhusu daftari la kujaza wateja lipo na hakuna kikwazo kwa mteja kusaini daftari letu kama ipo changamoto uliyokutana nayo basi tupatie kwa hatua za haraka

3.Huduma kwa wateja na muda wa kutoa huduma. Tumekuwa tukitoa huduma muda wote wa kazi na siku za mapumziko pia.Kwa kweli wataalamu wetu haswa uliyemtaja wamekuwa wakifanya vizuri sana na kupokea sifa kem kem kutoka kwa wateja hivyo kama kuna mahali haukuridhika tunaomba tukusikilize kwa hatua zaidi

Hitimisho

Tunaomba kukusikiliza na kukupatia majibu stahiki kwa malalamiko yako yote ili kuboresha mahusiano baina yako na sisi pamona na kuendelea kukuhudumia vizuri zaidi. Tusaidie namba yako ya simu tafadhali

TANESCO HUDUMA KWA WATEJA , MAKAO MAKUU

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Tatizo ni kwamba Tanesco Mlandizi wamewapa walinzi wa Getini mamlaka ya kumsikiliza mteja na kumruhusu kuingia ndani au kutoingia kwa hiyo wateja hawapati nafasi ya kupewa majibu sahihi kutoka kwa wataalam wa Tanesco.

Mimi niliwahi kufika pale mlinzi akaniambia nisiingie ndani maana Manager hayupo, nikamiambia kwa kuwa nilishafika naomba kuwaona hata wafanyakazi wengine wanaweza kunishauri nikakataliwa kabisa.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Je ulipozuiwa ulimuona meneja wa eneo husika?
Sent using Jamii Forums mobile app
TANESCO Malalamiko keshayataja, ni kwamba Meneja wa Mlandizi anakata umeme kwa upendeleo/ ma una post kaelezea Sherehe zilifanyika kwa Mbunge, umeme ulipokatwa simu ilipigwa umeme ukarudishe
  1. Kweli tmemshauri kwanza atoe Malalamiko kwenu kuliko kupitia humu JF, SASA MNAPOMSHAURI AWAPE SIMU YAKE ILI AWASILISHE TENA MAALAMIKO YAKE SI KWELI
  2. HitimishoTunaomba kukusikiliza na kukupatia majibu stahiki kwa malalamiko yako yote ili kuboresha mahusiano baina yako na sisi pamona na kuendelea kukuhudumia vizuri zaidi. Tusaidie namba yako ya simu tafadhali
    TANESCO HUDUMA KWA WATEJA , MAKAO MAKUU
    mnaonaje km mmeshindwa kumfuatilia Mlalamikiwa ambaye ni Meneja wa Chalinze mnaonaje aende kwa Waziri Kalemani moja kwa moja au apitie kwa Mbunge Ridhwani (ambaye yumo humu humu JF
USHAURI msaiedieni kwa kufuatilia km ni Majungu maana naona kaogopa na sisi Member tungependa kupata ukweli
 
TANESCO Malalamiko keshayataja, ni kwamba Meneja wa Mlandizi anakata umeme kwa upendeleo/ ma una post kaelezea Sherehe zilifanyika kwa Mbunge, umeme ulipokatwa simu ilipigwa umeme ukarudishe
  1. Kweli tmemshauri kwanza atoe Malalamiko kwenu kuliko kupitia humu JF, SASA MNAPOMSHAURI AWAPE SIMU YAKE ILI AWASILISHE TENA MAALAMIKO YAKE SI KWELI
  2. mnaonaje km mmeshindwa kumfuatilia Mlalamikiwa ambaye ni Meneja wa Chalinze mnaonaje aende kwa Waziri Kalemani moja kwa moja au apitie kwa Mbunge Ridhwani (ambaye yumo humu humu JF
USHAURI msaiedieni kwa kufuatilia km ni Majungu maana naona kaogopa na sisi Member tungependa kupata ukweli
Kwa taratibu ubapopata lalamiko unawajibika kusikiliza pande zote mbili hivyo tunawaomba uvumilivu wenu wakati tunalifanyia kazi lalamiko husika.Mteja tuneshampigia simu na bado hatua kadhaa tunazichukua

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwa taratibu ubapopata lalamiko unawajibika kusikiliza pande zote mbili hivyo tunawaomba uvumilivu wenu wakati tunalifanyia kazi lalamiko husika.Mteja tuneshampigia simu na bado hatua kadhaa tunazichukua
Kongole kwenu maana ktk Post # 8 tumemshauri awaone kwani ndio salama zaidi na itashughulikiwa kuliko kuifidha JF
siku hzizi kuna watuwasiojulikana wanaweza kumdhuru kupitia TCRA au kwingineko kuisaidia POLISI
Msaidieni mshamba mchangamfu
 
Back
Top Bottom