Meneja TANROADS aelezea ulipofikia mchakato wa Ujenzi wa Barabara ya Mbagala Mzinga - Kongowe - Kisemvule

Meneja TANROADS aelezea ulipofikia mchakato wa Ujenzi wa Barabara ya Mbagala Mzinga - Kongowe - Kisemvule

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Joined
Apr 18, 2017
Posts
3,984
Reaction score
13,760
Baada ya andiko la Mwanachama wa JamiiForums.com aliyedai Barabara inayopita katika Daraja la Mto Mzinga pamoja na Daraja lenyewe maeneo ya Mbagala, Dar es Salaam ni changamoto kutokana na uchakavu na kutoboreshwa kwa muda mrefu, TANROADS imetoa maelezo.

Kusoma alichoandika Mdau bofya hapa ~ Barabara ya Mbagala hadi Kongowe inatesa wananchi Serikali itupie jicho

Akijibu hoja hiyo, Meneja wa Wakala ya Barabara Tanzania (TANROADS), Mhandisi, John Mkumbo amesema “Hiyo barabara na Daraja lake mchakato wake upo kwenye hatua za manunuzi, ikikamilika kila kitu kitaendelea, mchakato wa ujenzi utaanza mara baada ya kusainiwa kwa mkataba ambao ndio utaweka wazi kuhusu ujenzi.”

Screenshot 2024-10-17 142449.png

photo_2024-10-17_13-41-29.jpg

photo_2024-10-17_13-57-15.jpg

Pia soma hapa
~
Barabara ya Kilwa kipande cha Mzinga Kongowe kinatumaliza
~ Hizi barabara mbovu Kigamboni na Chamazi, Serikali imeishiwa hela?
 
huo mchakato usio isha mpaka lini.Hii barabara haiwezi kumaliza mwezi hajafa mtu kwa ajali.Achana na foleni zinazosababishwa na malori kushindwa kupanda hicho kilima
Mimi nimewahi kupata ajali hapo ,lory lilishindwa break likatufata na kutugonga na kutupeleka kwenye mtaro ni vile Mungu tu
Hii barabara sasa hivi ni kiunganishi cha Dsm na mikoa ya pwani huko kwenye viwanda vingi
Hapo ndipo watu tunamkumbuka mzee Magu(R.I.P)
 
katika kitu viongozi wote wa kusini wamefeli ni hii barabara

inanifikirisha W/Mkuu ni wa kusini na anaelewa hii ndio barabara inaunganisha kwao ila ni mbovu nayeye ana nafasi ya kufanya jambo ametulia
morogoro road iko vizuri
bagamoyo road mkeka
ila yeye kipande cha mbagala-vikindu/kisemvule kimemshinda

ajifunze kwetu uchaganj
 
Anatakiwa apambane aufungue mkoa wake wa lindi na mikoa ya jirani kama lindi kwenda morogoro hakuna barabara
 
Anatakiwa apambane aufungue mkoa wake wa lindi na mikoa ya jirani kama lindi kwenda morogoro hakuna barabara
Kuna namna viongozi wa kusini hawaelewi maana ya wao kupata nafasi ya kuwa juu hasa kipindi hiki

nakumbuka kina Mrema,Sumaye,Lowasa walivyokamata nafasi za juu waliifungua sana mikoa yao

ila hawa wa kusini kuna namna vichwa vyao havifikirii umuhimu wa kuifungua mikoa yao
 
huo mchakato usio isha mpaka lini.Hii barabara haiwezi kumaliza mwezi hajafa mtu kwa ajali.Achana na foleni zinazosababishwa na malori kushindwa kupanda hicho kilima
Mimi nimewahi kupata ajali hapo ,lory lilishindwa break likatufata na kutugonga na kutupeleka kwenye mtaro ni vile Mungu tu
Hii barabara sasa hivi ni kiunganishi cha Dsm na mikoa ya pwani huko kwenye viwanda vingi
Hapo ndipo watu tunamkumbuka mzee Magu(R.I.P)
Pole mkuu. Hiyo ajali kama naikumbuka hv, ilitaka kumtoa mke wangu roho hiyo siku, nakumbuka vifo kadhaa vilitokea ma majeruhi wengi sana maana liligonga gari kadhaa za abiria, hadi leo wife ana kovu la ajali ile. Hakika ktk barabara za mjini hapa zinazogawa mateso kwa wana nchi hii inaongoza. Kila mtu amabye ameshaitumia hii barabara n8 lazima atamkumbuka Mr. Mwenda zake pamoja na yote aliyoyafanya katka uongozi wake. Tunaamini angekuwepo hii hali isingekuwepo kabisa hilo naamini. Mungu amuhifadhi.

Kinachokatisha tamaa ni kwamba, hv karibuni nimesafiri hadi Mtwara, nikajionea hali ya hiyo barabara, haaaaaa hapana aisee, hali ni mbaya kupita tunavyofikiri na ma manager wa TANROAD na TARURA pesa hawajaletewa. Anyways niishie tu hapo
 
katika kitu viongozi wote wa kusini wamefeli ni hii barabara

inanifikirisha W/Mkuu ni wa kusini na anaelewa hii ndio barabara inaunganisha kwao ila ni mbovu nayeye ana nafasi ya kufanya jambo ametulia
morogoro road iko vizuri
bagamoyo road mkeka
ila yeye kipande cha mbagala-vikindu/kisemvule kimemshinda

ajifunze kwetu uchaganj
Usiongee vitu usivyo vijua barabara ya kusini sio mbovu

Hiyo sehemu inayosumbua ni kipande na kipo chini ya mkoa wa Dar

Ukimaliza hicho kipande ukikutana na bango linalosema karibu mkoa wa pwani ni mkeka kwenda mbele

Na ukiwa unatokea kusini ukikutana bango karibu Mkoa wa Dar shida ndio inaanzia hapo

Hapo uzembe upo Kwa TANROADS, mkulugenzi wa mkoa wa Dar pamoja na mkulugenzi wa wilaya Temeke
 
Dar mwisho kongowe mkuu

barabara ya kongowe kisemvule bado nayo mbovu tu hakuna cha kusingizia vipande na kutetea upuuzi
 
Back
Top Bottom