''...Meneja amesema mpaka sasa kwa wastani wana hudumia abiria 250 kwa mwezi na ndege za Shirika la ATCL zinatua uwanjani hapo mara 3 kwa wiki...''
Amenukuliwa kwa usahihi? Au namba aliyotoa ni sahihi?
Inawezekanaje ndege itue mara tatu kwa wiki halafu uwe na wastani wa abiria 250 kwa mwezi?
Au huo ni wastani wa wiki?
Maana kwa abiria 250 kwa mwezi hii ina maana kuwa:
1. Kwa wiki ni sawa na abiria 250/4 = 62.5 approx abiria 63
2. Kama kwa wiki kuna safari 3 za ndege kupeleka abiria 63 hii ina maana kuwa 63/3 = abiria 11 kwa safari moja ya ndege.
Meneja atafutwe ili athibitishe hizi namba