Roving Journalist
JF Roving Journalist
- Apr 18, 2017
- 5,352
- 15,876
Meneja wa Uwanja wa CCM Kirumba uliopo jijini Mwanza, Hassan Omar Ali amesema taarifa kuwa uwanja huo una changamoto ya uhaba wa vyoo ilikuwa ni mkakati wa kuchafua sifa iliyopangwa na watu wenye nia hovu juu ya eneo hilo.
Hoja ya awali ~ Uwanja wa CCM Kirumba hali ni mbaya. Watu wajisaidia hovyo, kutokana na vyoo kujaa uchafu
Akifafanua kuhusu video iliyosambaa ikionyesha baadhi ya mashabiki wakijisaidia kwenye chupa na maeneo yasiyo rasmi ndani ya uwanja huo, Meneja Hassan amesema inakuwaje watu hao wanaenda kujisaidia hadharani, tena wakiwemo watu wazima na wanawake, huku uwanja ukiwa na vyoo vya kutosha na vilivyo wazi.
Anasema “Uwanja una mageti 11 ya kuingilia na kila geti lina vyoo sita thabiti na safi, ambavyo vimekuwa vikitumika bila shida kwenye mechi kubwa zilizopita. Mfano mechi kati ya Pamba na Yanga ambayo ilijaza mashabiki wengi zaidi ya 15,000, na hakukuwa na changamoto yoyote ya miundombinu hiyo ikilinganishwa na mechi ya Azam na Yanga ambayo haikuwa na mashabiki wengi kiasi hicho.”
Anaongeza “Tunamsaka aliyetengeneza video ile kwa kuwa ni wazi walipanga na wahusika kwa sababu zao binafsi ili michezo mikubwa isitete Kirumba, video ile imedhalilisha Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kwa kuwa kambali ya mchezo walikagua na kuona kila kitu kipo sawa.
“Kabla ya TFF kuruhusu mechi yoyote kubwa (Big Match) kuchezwa Kirumba, huwa wanatuma barua ya mahitaji na kufanya ukaguzi wa kina wa miundombinu yote ikiwemo vyoo, na kutoa kibali baada ya kujiridhisha kuwa kila kitu kiko sawa.
“Hivyo, Uongozi wa Uwanja wa CCM Kirumba umechukua hatua zifuatazo ili kuzuia hali hiyo isijirudie: Ulinzi na Uangalizi Makini: Kuweka walinzi maalum kwenye maeneo yote ya wazi yanayoweza kupitika ili kuzuia watu kufanya vitendo visivyofaa.
“Kuelekeza Mashabiki: Kuweka utaratibu mzuri wa kuwaelekeza mashabiki, hasa wageni, mahali vyoo vilipo ili wasipotee au kutumia maeneo yasiyohusika.
“Hatua za Kisheria: Suala hilo tayari liko mikononi mwa vyombo vya sheria na mtu aliyetengeneza na kusambaza video hiyo anatafutwa ili athibitishe madai yake.”