Meneja wa Diamond akamatwa tena, aswekwa rumande

barafu

JF-Expert Member
Joined
Apr 28, 2013
Posts
6,739
Reaction score
32,880
Meneja wa mwanamuziki wa kimataifa Diamond Platnumz, Hamis Tale Tale maarufu kwa jina la ‘Babu Tale’ hivi sasa yupo mikononi mwa polisi Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam.

Babu Tale amekamatwa leo na kufikishwa mahakamani hapo ili ajieleze ni kwa nini asifungwe kwa kushindwa kutekeleza hukumu ya Mahakama iliyomwamuru alipe fidia ya Sh250 milioni kwa makosa ya kuvunja sheria ya Hakimiliki.

Babu Tale anatakiwa alipe fedha hizo kutokana na kuvunja mkataba kati yake na Shekhe Mbonde, kwa kuuza na kusambaza nakala za mawaidha (DVDs) bila ridhaa ya shekhe huyo, jambo ambalo ni kinyume na haki miliki.

Chanzo: Mwananchi
 
Babu Tale kakutana na Wazee wa Mji acha ajifunze uungwana
 
Babu Tale amekamatwa leo na kufikishwa mahakamani hapo ili ajieleze ni kwa nini asifungwe kwa kushindwa kutekeleza hukumu ya Mahakama iliyomwamuru alipe fidia ya Sh250 milioni kwa makosa ya kuvunja sheria ya Hakimiliki.

Dar es Salaam Meneja wa mwanamuziki wa kimataifa Diamond Platnumz, Hamis Tale Tale maarufu kwa jina la ‘Babu Tale’ hivi sasa yupo mikononi mwa polisi Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam.

Babu Tale amekamatwa leo na kufikishwa mahakamani hapo ili ajieleze ni kwa nini asifungwe kwa kushindwa kutekeleza hukumu ya Mahakama iliyomwamuru alipe fidia ya Sh250 milioni kwa makosa ya kuvunja sheria ya Hakimiliki.

Babu Tale anatakiwa alipe fedha hizo kutokana na kuvunja mkataba kati yake na Shekhe Mbonde, kwa kuuza na kusambaza nakala za mawaidha (DVDs) bila ridhaa ya shekhe huyo, jambo ambalo ni kinyume na haki miliki.
 
Nakumbuka watu walitoa michango yao ya kisheria.... kama angesikiliza.... Yasingemkuta wallah
 
Pale matajiri wanaposua sua kulipa.....
 
Angemtafuta huyo shekhe njaa nje ya mahakama ampe hata milioni tano wamalizane!!

Sent from my BlackBerry 9320 using JamiiForums
usilete dhihaka kwenye matatizo ya watu. Kumuita mtu shehe njaa pasi kujua ukweli wa mambo ni dharau na kebehi isyokuwa na tija. Ingekuwa wewe ndie unaedai haki yako ungekubali ulipwe pungufu ya stahiki yako kwa vile tu una njaa?
 
Back
Top Bottom