Meneja wa Diamond Platnumz, Babu Tale amjibu Shigongo

Meneja wa Diamond Platnumz, Babu Tale amjibu Shigongo

Huku mwaka ni mwaka wa wasukuma, wanatrend hao kuanza January makonda, mara gwajima tukapumzika kidogo Shigongo, sijui baadaye atakuwa nani. Ila nimekaa nimejiuliza Kuna msemo mmoja wa fid q anasema '' SIKU HIZI HAMNA UHURU WA HABARI, KUNA UHURU WA MWENYE MITAMBO NA MWENYE MALI '' sasa naliamini, sasa subiria reaction ya Shigongo na magazeti yake, atakavyomuandama diamond platnumz na management yake, ila kwa diamond platnumz nina uhakika atashindwa tuu, kwanza hata yeye mwenyewe na magazeti yake hali ni mbaya, instagram, Facebook, Twitter na whatsup zinampa stress na bado kama hana mpango mbadala wa kuiokoa kampuni yake yeye ndio atakuwa wa kwanza kudondoka.
Umemsahau Ney
 
Ushauri amepewa Diamond, Babu Tale povu la nini? Mbona Sallam kakaa kimya? Kinachomuuma Tale ni magazeti ya Shigongo kuandika habari za yeye kumdhulumu shehe na kushtakiwa Mahakamani. Tale hakutaka habari zile ziandikwe, mwanzo alisema magazeti ya udaku waongo, watu wakasubiri siku ya kesi wakaenda kumpiga picha na kurudia stori, hapo ndipo chuki zilipoanza
 
Hivi kwa hii kitu ilivyo kuna kuwa na uhakika gani kuwa hayo maneno ni ya mtu fulani!!?
 
Huwa nachukia sana kauli za "Tulisema, nilisema" ila kwa leo ngoja na mimi niseme kuwa jana nilisema hili ni suala la biashara, Tanzania kuna watu wanapenda sana Kuwatumikisha wengine kama watumwa bila kujali una jina umelitengeneza kwa shilingi na gharama gani na muda. Harmonize was nobody and no body gave a **** abt him leo ametengenezwa amepata jina mtu anajipa MAMLAKA YA UTABIRI kwa kutaka kukutumia BURE tu

- Aiyola (Video + Audio 35M )

- Bado ( Video + Audio 40 )

- Matatizo ( 8M )

- Niambie ( 30M )

Bado kuna gharama za muda, utunzi, kukesha muda na ubunifu, LEO MTU ANATAKA KUKUTUMIA BURE TU na watu wanaoongoza kufanya haya ni SHIGONGO na CLOUDS, Ukibuma ndo WANAKUCHEKA NA HAKUNA ATAKAYEKUJALI
 
ldddmmmmtttatizo wabongo si waelewa hata kidogo. mada ya shigongo ni kuemwelekeza diamond, sasa babu tale kinachomtoa povu ni nini? ukwlei umemuuma? hawasa wasanii wetu wakiwa wanatafuta kutoka wanauitaga shigongo 'broo' wakishafanikiwa wanamwona kama anawachafua. kama si magaeti ya shigongo diamond asingekuwa huyu anayekimbiliwa na akina babu tale leo
 
Nina muda mrefu sana sijasoma magazeti maana taarifa zote na kila kinachojiri nakipata mtandaoni Jamiiforumz,Twitter, Instagram, Facebook, WhatsApp na telegram, habari zote nazipata kwa wakati mpaka wengine huwa wananiuliza napata wapi habari, sisomi magazeti wala sipati muda wa kusikiliza redio, nikiamka tu naingia mtandaoni kidogo baadaye naendelea na mambo mengine nikipata time natupia tena jicho mtandaoni, sasa akina shigongo wana njaa mambo yamebadilika
mbona uingreeza mitandao imeanza miaka mingi lakini bado watu wananunua magazeti, we sema hali ya mfuko wapo si nzuri
 
Shingongo bana akiwa na bifu anataka kila mtu ajue. Kuna kipindi alikuwa na bifu na uwoya kisa wanakijua wao,jamaa akapiga stop kuandika habari za uwoya kwenye magazeti yake huku akijitapa alimpandisha umaarufu na atamshusha. Saiv zamu ya dai na team yake [emoji23] [emoji23] [emoji23] jaman
Bifu lake na songoro mtengeneza meli
 
Umejitahidi kujaribu kubomoa biashara yangu kenye magazeti yako kwa kila aina ya uchafu kuwazushia na kuwaandika wasanii wangu tumekaa kimya. Baada kufeli kuwabomoa wasanii wangu na kuona magazeti yako sasa hayauzi, watu wapo instagram Naona unajitahidi kujaribu kubomoa biashara yangu kupitia instagram yako.

Siku zote nimekuheshimu na sijawai kuku vunjia heshima hata kwa kuteleza, ila unapoelekea Sina budi ya kukupa unacholazimisha kukipata ili kesho ukawaambie vizuri waandishi wa magazeti yako wanitungie kashfa, uongo na kunitukana kama mnavyofanya kwa wasanii wangu, wasanii wwengine na watu mbalimbali.... tafadhali heshimu biashara yangu kama inavyokuheshimu.

Umekazana wiki nzima kuandika vitu vya uongo juu ya Diamond ila sie tumekaa kimya na kujifanya unazunga eti unatushauri. Kweli mtu unasema unampenda unamshauria instagram, ama unamwita ofisi au nyumbani kumshauri?

Mbona sie hatujawai kuingilia biashara yako wala kukupangia bei juu ya kuuza bidhaa yako yoyote labda kusema gazeti uuze kwa shilingi mia au hamsini? Na kuonesha hatukuwa na tatizo kabisa na wewe, juzi tu tumetoka kuongea na wewe kufanya show ya @Harmonize_tz DARLIVE na tukakubaliana asilimia, na hadi kupost tumepost ila baada ya kuona watu wameipokea kwa ukubwa teaser ya show umetubadilikia na kutaka asilimia kuuuubwa wewe, eti sisi tuchukue asilimia ndogo kabisa tukaona tukae tu kimya, na hatujakulalamikia wala kukuandika popote kiubaya juu ya kutaka asilimia kubwa.

Hivi kweli hata kama kuweka wasanii karibu na mashabiki zao hii ndio kuwaeka karibu wasanii na mashabiki zao kama usemavyo ama kuwaibia wananchi wanaodunduliza kuwasapoti wasanii wao na wewe kujifaidisha kwa kuendelea kuwanyonya wasanii na kutajirika wewe mwisho wa siku wasanii waishie kuambulia jina, na kula Madawa yote kutafuta sababu Msanii akikataa ama kudai aongezewe mapato Ukawaamuru watu wako wakamtungie kashfa na skendo za uongo na kweli ili kum'bomoa msanii kupitia magazeti yako.

Tafadhali heshimu heshima yetu kwako. "Mh Magufuli tafadhali Ulipo Kaza legeza, ona Wakubwa wanaanza kutaka kupora hadi watoto vidogo vyao.
mimi sijaona hoja ya babu tale. na kama meneja wa msanii mkubwa anaweza kutoa madai haya ya kikazi kwenye mitandao kuna tatizo kubwa kwa mameneja wa wasanii wetu. ndiyo maana muziki wa Bongo uko levo moja miaka na miaka
 
ldddmmmmtttatizo wabongo si waelewa hata kidogo. mada ya shigongo ni kuemwelekeza diamond, sasa babu tale kinachomtoa povu ni nini? ukwlei umemuuma? hawasa wasanii wetu wakiwa wanatafuta kutoka wanauitaga shigongo 'broo' wakishafanikiwa wanamwona kama anawachafua. kama si magaeti ya shigongo diamond asingekuwa huyu anayekimbiliwa na akina babu tale leo
Tatizo kubwa ni kwamba wewe ndio hujaelewa lakini unalazimisha watu wengine waone kama vile wao ndio hawajaelewa

- Shigongo anamshauri Diamond kuwa atashuka eti kutokana na MAMENEJA Wake, sasa wewe huoni kama Shigongo anataka kuwachonganisha Diamond na Mameneja wake na sababu kubwa Alitaka kumtumia Harmonize kwenye show yake Dar Live wameshtukia. Dunia imebadilika sana kwa sasa kila msanii mjanja muda wa kuburuzana na kutumiana kama cheap labour ushakwisha
 
Shigongo alitengeneza hoja fresh tu kwenda kwa Naseeb Abdul na uongozi wake.

Babu Tale baada ya kujibu hoja kuhusu Diamond yeye kaja kufumua mambo ya Harmonise na show Dar Live mara anayashutumu magazeti ya Shigongo.

Mwanzo sikumuelewa Shigongo na kumuona kavurugwa ila kama haya majibu ya Babu Tale yamenifanya kuona tatizo liko wapi.

Kama Tale angejibu hoja kwanini Diamond anafanya show kwa Milioni 100 angevunja vunja hoja zote za Shigongo ila naona Tale kaamua kupambana kitoto na sio kisomi.
 
[emoji3] [emoji3] naona upo kwenye ubora wa ubashite wako wewe pimbi
We huoni shigongo anataka kitonga, diamond akifanya show za 5000 wakina man fongo na nuh mziwanda so watakufa na njaa
 
Sikuwahi wala sikutaka kuamini kama shigongo nyumbu kiasi hicho kweli magufuli kabana watu biashara zimebuma yani shigongo leo hii ndio unataka kutelezea kwa mondi kweli kua uyaone sio kwa kiki hii umejinyea bro
Umepuyangaaaaaa[emoji57][emoji57][emoji57][emoji57]
hivi mkuu umefuatilia kinachosemwa? mtu akikupa ushauri wa huko uendako ili ujipange kuna tatizo? nyumbu ni nyumbu tu au ulitaka ampe ushauri au amsifie akishakufa?
 
Mbona hajaongelea dau la dola 55,000 .
Maana ndo ushauri alioutoa shigongo...nilitegemea angejibu ushauri huo kwa kusema kwa vipi haitowezekana kushusha dau...badala yake anaongelea vijembe na shutma za kike kike.
naunga mkono hoja
 
Shigongo alitengeneza hoja fresh tu kwenda kwa Naseeb Abdul na uongozi wake.

Babu Tale baada ya kujibu hoja kuhusu Diamond yeye kaja kufumua mambo ya Harmonise na show Dar Live mara anayashutumu magazeti ya Shigongo.

Mwanzo sikumuelewa Shigongo na kumuona kavurugwa ila kama haya majibu ya Babu Tale yamenifanya kuona tatizo liko wapi.

Kama Tale angejibu hoja kwanini Diamond anafanya show kwa Milioni 100 angevunja vunja hoja zote za Shigongo ila naona Tale kaamua kupambana kitoto na sio kisomi.
ni kweli hiyo ndiyo hoja ya msingi, watu wajifunze kujenga hoja waache kukurupuka
 
Babu Tale kapaniki sana why? Alichokieleza Ngosha to some extent kina mashiko, nani asiyejua mameneja ndiyo wanaochangia sana kuwaangusha wasanii wao? Huyu alikuwaga meneja wa Mb Dogg kipindi kile anatamba na Latifa, akaja kuwa meneja wa Keisha na Tip Top at large, tazama maisha ya hao wote aliowahi kuwa-manage, angalau kidogo Madee siku hizi kapata akili anajiongeza kivyake, bosi kahamia Madale hawakumbuki kabisa vijana wake... huyu pia alikuwa meneja wa Rayvan (Raymond) kabla hajatoka, akawa anamsugulisha sana benchi, dogo katusua anamganda kinoma... mind you Dogo Janja naye yupo chini ya himaya yake... lets call a spoon a spoon and a spade a spade! Ana kesi bado mahakamani ya kuiba kazi za sanaa kwa ustaadh mmoja, tena nyimbo za Qaswida... dont fool people na utetezi wa shoo sijui nani kataka nini Dar Live, acha drama
 
Erick atulie, now hatusomi magazeti umbea tunaupata insta lazima apate stress!!

Huwa ana karoho kabaya sana yule baba
Yaani nisimsome warumi humu nihangaike na shigongo? Nitakuwa naumwa sana !
Huwa nachukia sana kauli za "Tulisema, nilisema" ila kwa leo ngoja na mimi niseme kuwa jana nilisema hili ni suala la biashara, Tanzania kuna watu wanapenda sana Kuwatumikisha wengine kama watumwa bila kujali una jina umelitengeneza kwa shilingi na gharama gani na muda. Harmonize was nobody and no body gave a **** abt him leo ametengenezwa amepata jina mtu anajipa MAMLAKA YA UTABIRI kwa kutaka kukutumia BURE tu

- Aiyola (Video + Audio 35M )

- Bado ( Video + Audio 40 )

- Matatizo ( 8M )

Bado kuna gharama za muda, utunzi, kukesha muda na ubunifu, LEO MTU ANATAKA KUKUTUMIA BURE TU na watu wanaoongoza kufanya haya ni SHIGONGO na CLOUDS, Ukibuma ndo WANAKUCHEKA NA HAKUNA ATAKAYEKUJALI
 
mbona uingreeza mitandao imeanza miaka mingi lakini bado watu wananunua magazeti, we sema hali ya mfuko wapo si nzuri

Uingereza gani unasema wewe? Wao wana internet ya uhakika kuliko Bongo, na magazeti yao yote yana websites, Facebook pages na Twitter ambazo ziko busy. Kwa taarifa yako tu, wao hawategemei kuuza copies kama Shigongo ndio wapate pesa. Kuna magazeti mengine yanagawiwa bure asubuhi kwenye vituo vya mabasi na treni. Au mengine unaletewa mpaka mlangoni bila kulipa chochote. Mimi nakubaliana na wadau wanaosema Internet imeua biashara ya magazeti ya udaku hasa Dar es salaam.
 
Babu Tale ndio kaandika hivi? Amelalamika Sana Kama vile siyo meneja wa Diamond.
Ndio jadi yao hiyo sio diamond sio Harmonize hadi mameneja wao kazi yao ni kulalamika tu. Wanapendaga kujifanya masikini wana shida wanatokea familia duni wakati kiukweli time hii wako poa life limewanyookea. ila huyo Shigongo namuonea huruma cause siku hizi watu hawanunui udaku, wanaupata insta tena mubashara. Alijiona mjanja enzi zile watu wananunua udaku akawa anawazidi wenye magazeti ya hard news na uchambuzi. Akaoge alale
 
Back
Top Bottom