Kurzweil
JF-Expert Member
- May 25, 2011
- 6,621
- 8,411
Habari wanaJF,
Meneja wa Simba Robert Richard amefungiwa mwaka mmoja kujihusisha na soka na faini ya Tsh milioni 4, Robert amekutwa na makosa mawili kuihujumu timu ya taifa kwa kutotii maagizo ya TFF na kuchelewesha wachezaji wa Simba kufika kambini Taifa Stars
======
Wachezaji wa Simba waliokuwa wameitwa kwenye kikosi cha timu ya taifa 'Taifa Stars', waliondolewa katika kikosi hicho baada ya kushindwa kuwasili kambini kwa wakati.
Wachezaji hao ni pamoja na John Bocco 'Adebayor', Shiza Kichuya, Jonas Mkude, Erasto Nyoni, Hassan Dilunga na Shomari Kapombe.
Katibu Mkuu wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Wilfred Kidau, alisema Kocha, Emmanuel Amunike, amefanya maamuzi hayo baada ya kushangazwa na jinsi ambavyo wachezaji wa Tanzania wamekuwa wakijivuta wanapoitwa timu ya taifa.
Chanzo: Mwananchi