Mkuu,wananchi sisi ni wajanjawajanja mnoo.Huwa tunalima kiujanjaujanja kama tunapalia nyasi(wanyamwezi wanaita kukela).Kumbe ndiyo kilimo chenyewe.Utakuta tumeshapanda mahindi,mtama,karanga,maharage,kunde nk.
Ukiuliza hilo swali kwamba mamlaka ilikuwa wapi utakwama.Maana kuna "mabalozi",wajumbe wa s/mtaa,mwenyekiti,watendaji wa mitaa,watendaji kata na madiwani tunashinda nao humohumo mitaani.Lakini kuna sababu.
-na wenyewe huwa tunawapiga chenga hivyohivyo kwa kuwazevezya/kuwadanganya tukifanyacho.
-tunawavizia wakati hawapo hasa wikiendi,jioni na sikukuu.
-wengine ni ndugu zetu,marafiki,majamaa,wametuzoea sana au hata wakwe zetu.Hutuonea aibu.Kitanzania hiyo.
-wanatuogopa kwa upole wetu sana,midomo yetu mikali au uchawi.
-uzembe wao kutofuatilia kwa ukaribu.
-wakati mwingine tunawakaribisha "chai".
Ni hayo kwa uchache wake.