PM anaweza kuwa alikuwa sahihi kbs, lkn kutokana na mazoea yetu ya kutotenga bajeti katika kufanya ukarabati wa miundo mbinu chakavu, je hata angekagua pesa ingetolewa ili kufanya ukarabati? Yani Kama tukijaribu kuangalia uhalisia, tunaona kweli hili lingetokea?
Ikiwa tu baadhi ya miradi mipya iwe mikubwa au midogo inasimama kwa kukosa pesa, ije kuwa hili la kutoa pesa ili kukatabati daraja ambalo lilikuwa likionekana liko vzr tu kabla ya kusombwa na maji hiyo juzi?
Sisi hatuna utaratibu madhubuti wa kumaintain assets au miradi mbalimbali tuliyoanzisha, yani inakuwa ikishajengwa ndy ntolee.
Embu chukua mfano wa mradi wa DART, yaani huu mradi hauna kbs muendelezo mzr, hv Sasa hakuna tena ule utaratibu wa kuscan tickets, vituo vyao vimeanza kuharibika baadhi ya maeneo, dustbins zile katika vituo zimen'golewa , utaratibu wa kutangaza vituo hakuna tena, achana na uozo ktk utaratibu wa kupakia abiria ktk mabasi yenyewe n.k lkn ajabu hakuna anaestuka hata kdg.
Nilitarajia ubunifu zaidi ktk huu mradi Kama kuweka Wi-Fi free ktk vituo na mabasi yake(kuonesha wanajali wateja wake), utaratibu mzr wa ticket, utaratibu mzr wa ratiba ya mabasi mfano kuwa na sign board au digital display device itakayoonesha bus la route gani litawasili baada ya muda gani, huu utaratibu wange u integrate na application maalum ambayo mtu hata kabla hayatoka nyumbani anaangalia kwa simu yake na anajua kbs bus atakalopanda litafika baada ya muda gani kituo husika.
Sent using
Jamii Forums mobile app