Meneja wa TANROADS nchini asema daraja la Kiyegeya limekatika kwa uchakavu. Je, Waziri Mkuu kumuondoa Meneja TANROADS-Morogoro alimuonea?

Meneja wa TANROADS nchini asema daraja la Kiyegeya limekatika kwa uchakavu. Je, Waziri Mkuu kumuondoa Meneja TANROADS-Morogoro alimuonea?

Waziri mkuu kamwondia Meneja kwasababu kipenyo kilikua kidogo kwasababu kiliziba kwa mchanga uliojikusanya mvua iliponyesha awali. Sidhani hiyo ndio sababu
 
Kumbe mfugale anajua yalishachoka! Kama unajua hilo maana yke uangalizi unatakiwa kuwa karibu sana.
Mi naona mfugare nibola asingeongea hilo. Hii nikutaka kutuaminisha kuwa ipo cku watu watakufa kwatatizo wanalolijua wataaram wetu!
Ndo maana kule mwanza magu daraja la mto simiyu limeanza kufanyiwa ukarabati kila siku usiku.
Ndo inavyotakiwa siyo baada ya tatizo unasema wanajua.
Masanjaone, naunga mkono hoja
 
Ni sawa ila mbona yote ayajasombwa na maji? Kama waandis wangekagua kuna kitu wangegundua na kuchukia hatua, daraja alisombiti kama gogo, lilianza taratibu.....

Kwani kazi hasa ya ao waandis ni ipi? Ata mimi kazini kwangu kuna vitu baada ya siku mbili lazima nichek, ata usafir wako lazima uuchek kama upo sawa baada ya muda flan.....
Madaraja yote njia hiyo ni chakavu
.hujaelewa nn? Serikali hii haina fedha tu.kwani nchi nzima unajua machakavu yanapungua 100?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wakati meneja wa Tanroads mkoani Morogoro, Godfrey Andalwisye akiondolewa kwa madai ya kutokagua miundombinu, mtendaji mkuu wa taasisi hiyo, Patrick Mfugale amesema barabara ya Morogoro-Dodoma ni chakavu kwa kuwa imejengwa muda mrefu.

Kauli hiyo ya Mfugale imekuja siku moja baada ya Waziri Mkuu Kassim Majaliwa kuagiza Andalwisye arudishwe makao makuu kutokana na kutokagua barabara hiyo ambayo daraja lake la Kiyegeya lililoko wilayani Kilosa lilisombwa na maji.

Waziri Mkuu, ambaye juzi alikuwa ameenda eneo hilo kushuhudia ujenzi wa daraja hilo, alishangaa kuona mkoa wenye wahandisi 12, kushindwa kufanya ukaguzi wa barabara na madaraja.

Lakini jana, Mfugale alisema barabara hiyo ilijengwa miaka 40 iliyopita na hivyo imeshatumika muda mrefu ndio maana kila mara wamekuwa wakiifanyia ukarabati.

Alisema kukatika kwa daraja hilo ni jambo la kawaida kiutaalamu kwa kuwa uhai wa makalavati yanayowekwa si zaidi ya miaka 25.

Alisema tayari Serikali iko katika mchakato wa kuijenga upya barabara hiyo na madaraja yake.
Kama anajua ni kawaida kwanini hawakuchukua hatua ya kuliondoa what if lingekatika gari ikiwa inapita juu yake na watu wakapoteza maisha?
 
Hiyo ni taaluma yake na nikazi yake....
Mpaka daraja linasombwa kulia na wear and tear za muda mrefu ......
Life Span ni 100 yrs lakini kuna kama miaka ,40 toka lijengwe je hapo unamlaumu vipi mtaalam? Suala la kukagua hata kama lipo je anavifaa vya kuonesha ubovu wa daraja au ndo anakagua kwa kuchungulia kwa macho kama polisi wa usalama barabarani wanavyokagua magari?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Sipendi kumuingilia waziri mkuu wakati akitumia mamlaka yake kikatiba kuamua hili ama lile.. Swali hili limenipa kigugumizi na mtanziko mkubwa nafsini mwangu.. But nipende kusema kuwa tungeanza na kuwang'oa wale ambao hawakukagua reli mpaka kipande cha km 120 kikabebwa na maji if we want to be fair na kuepuka double standards... Haki itendeke kwa watu wa makabila yote maana mito iloyoharibu reli ndiyo hii iliyong'oa makalavati.
To be much fair tuchukulie haya kama maafa ama act of God kuliko kuyachukulia kama negligence!
 
Natumaini Mhe Waziri Mkuu angefanya utafiti kwanza kabla ya kumrudisha Meneja wa Tanroads- Morogoro Wizarani.
 
PM yuko sawa licha ya kua limesombwa kwa uchakavu lakin Muhandisi usikanalitakiwa kutoa taarifa kama lilikua kwenye hatari libadilishwe.....

Sent using Jamii Forums mobile app

Daraja la Wami Dakawa,

siku na wakati wowote litatuadhili,

ukiwa pale darajani kwa miguu, Kisha gari likapita huwezi amini macho yako,

daraja linatikisika utafikiri ndiyo mwisho wake.
 
Kumbe mfugale anajua yalishachoka! Kama unajua hilo maana yke uangalizi unatakiwa kuwa karibu sana.
Mi naona mfugare nibola asingeongea hilo. Hii nikutaka kutuaminisha kuwa ipo cku watu watakufa kwatatizo wanalolijua wataaram wetu!
Ndo maana kule mwanza magu daraja la mto simiyu limeanza kufanyiwa ukarabati kila siku usiku.
Ndo inavyotakiwa siyo baada ya tatizo unasema wanajua.

Ubovu wa hilo daraja ulikuwa unajulikana,

na siyo Hilo TU yapo mengi tu.

Kama daraja la Ruaha Mkuu pale Ruaha Mbuyuni lilikatika na hakuna aliyeadhibiwa.

Maji ni mengi kuliko uwezo wa daraja = Mvua NI kubwa kuliko makisio ya Wajenzi wa daraja.

Engineer Mfugale mtetee Huyo Mhandisi, mbali ya madaraja Kuna MASHIMO HATARISHI na mengi yalishasababisha ajali nyingi tu, si kwamba hakuna taarifa ya kuwepo kwake.

Mhandisi anaomba hela, ombi linakaa kwenye droo.

Hata ajali ya AZAM TV kule Shelui chanzo ni mashimo barabarani.
 
Wakati meneja wa Tanroads mkoani Morogoro, Godfrey Andalwisye akiondolewa kwa madai ya kutokagua miundombinu, mtendaji mkuu wa taasisi hiyo, Patrick Mfugale amesema barabara ya Morogoro-Dodoma ni chakavu kwa kuwa imejengwa muda mrefu.

Kauli hiyo ya Mfugale imekuja siku moja baada ya Waziri Mkuu Kassim Majaliwa kuagiza Andalwisye arudishwe makao makuu kutokana na kutokagua barabara hiyo ambayo daraja lake la Kiyegeya lililoko wilayani Kilosa lilisombwa na maji.

Waziri Mkuu, ambaye juzi alikuwa ameenda eneo hilo kushuhudia ujenzi wa daraja hilo, alishangaa kuona mkoa wenye wahandisi 12, kushindwa kufanya ukaguzi wa barabara na madaraja.

Lakini jana, Mfugale alisema barabara hiyo ilijengwa miaka 40 iliyopita na hivyo imeshatumika muda mrefu ndio maana kila mara wamekuwa wakiifanyia ukarabati.

Alisema kukatika kwa daraja hilo ni jambo la kawaida kiutaalamu kwa kuwa uhai wa makalavati yanayowekwa si zaidi ya miaka 25.

Alisema tayari Serikali iko katika mchakato wa kuijenga upya barabara hiyo na madaraja yake.
Majaliwa namuona kama kilaza asiyejiamini anayeiga ukali wa boss wake kama kick.Kila anakopitia yeye ni kusimamisha watu kazi ili aonekane yuko serious
 
Back
Top Bottom