DodomaTZ
Senior Member
- May 20, 2022
- 197
- 233
Akizungumza jambo hilo, Prosper alisema kuwa hatua ya Mbunge huyo imekuja wakati muafaka na inalenga kubadilisha kabisa hali ya miundombinu ambayo kwa muda mrefu imekuwa changamoto kwa wakazi wa Buchosa.
“Mheshimiwa Mbunge ameleta mitambo kwa ajili ya matengenezo ya barabara, barabara ambazo ni muhimu kwa huduma za kijamii na shughuli za uchumi katika halmashauri yetu ya Buchosa. Sisi TARURA tumejipanga – tumeandaa mafuta na mipango ya utekelezaji iko tayari. Tumeweka mkakati wa kufungua barabara nyingi iwezekanavyo,” amesema Mhandisi Prosper.
Ameongeza kuwa mitambo hiyo, iliyotolewa kwa jitihada binafsi za Mbunge, itatumika kufungua na kuboresha barabara ambazo hazijawahi kufikika kwa urahisi, huku TARURA wakihakikisha kuwa kila hatua ya utekelezaji inazingatia ubora na usalama wa watumiaji wa miundombinu hiyo.
Kwa upande wake, Mbunge Eric Shigongo alisisitiza kuwa lengo kuu ni kuhakikisha kila mwananchi ananufaika na fursa za maendeleo kwa kupata huduma muhimu kama elimu, afya, na biashara kupitia upatikanaji wa barabara bora.