Inasikitisha sana suala kama hili linapotokea na uhai wa binadamu mwenzetu unakuwa upo hatarini,ila mimi nakubaliana na mchangia hoja hapo juu kuwa chaguzi nyingi za nchi zetu za kiafrika zimetawaliwa na sitofahamu kubwa,why we always complicates things wakati kama uchaguzi ni wa huru kwa nini damu imwagike?nimeshughudia uchaguzi mkuu ndani ya nchi mojawapo ya SADC,ni salama na huru ;mpiga kura anajiandikisha kupiga kura kwa kutumia life book yake kweny eneo atakalapigia kura,then siku ya kura unakwenda pale wana scan life book yako kuthibitisha kama ulijiandikisha pale,then unapiga kura yako,baada ya upigaji kura kuisha na wawakilishi wote wa viama vilivyoshiriki kuafiki hili,kura zinahesabiwa pale pale kituoni,baada ya kukubaliana wote wanasaini kuafiki zile kura,then msimamizi wa uchaguzi from IEC anaziingiza zile kura kwenye mtandao wa ukusanyaji kura na zinakwenda moja kwa moja kwenye kituo mama cha ukusanyaji wa matokeo ambacho kina screen kubwa na kila mtu anaona matokeo moja kwa moja,kwa hili linaepusha matokeo kwenda kwa mtu mmoja au kikundi cha watu before mass wajue.democracy kwenye nchi zetu ni ndoto na nina wasiwasi kama itatokea kweny life time yangu.