Orodha ya watu wanaogombana na Mengi ilikuwapo kwa muda mrefu kutokana na umiliki wake wa vyombo vya habari (TV, radio na magazeti). Watu wengi tu, kwa namna moja au nyingine, walikuwa wanaguswa (ki-ubaya) na vyombo vyake hivyo na mara ya kwanza kabisa Mengi alikosana na mfanyabiashara mmoja wa Kiasia aliyekuwa anamiliki CTN (nimemsahau jina lake) kuhusu hakimiliki ya kutangaza mechi za World Cup mwaka 1994 kupitia ITV, wakati tu kituo hicho kinaanzishwa.
Mfanyibiashara huyo kumbe alikuwa fisadi maana baadaye alitoroka nchini na fedha nyingi za wafanyabiashara wengine aliowatapeli.
Orodha ya watu wanaogombana na Mengi imeongezeka kwa haraka baada ya vyombo vyake vya habari kuanza kupiga vita ufisadi kwa nguvu zote. Mimi sioni sababu nyingine.
[Chanzo cha vita hii labda kinatokana na yeye kukosa kuuziwa Hoteli ya Kilimanjaro, kwa kile alichokielezea mchezo mchafu uliofanyika akimaananisha milungula ilitembea. Katika tukio hilo Masilingi (akiwa waziri wa mambo ya usalama wa taifa) alimtisha Mengi kwa kutamka Vyombo vya dola vitamshughulikia. (Miaka kadha baadaye waziri Masha alirudia kauli kama hiyo dhidi ya Mengi.)]
Kila mtu ana orodha ya watu anaogombana nao, na umaarafu wa watu hawa unategemea na umaarufu wa yule wanaogombana naye.
Manji, kwa mfano, anao maadui wake wengine wengi tu (ukiacha Mengi) lakini hawa hawajulikani kwani Manji si maarufu sana kama Mengi (kwa mtazamo wa jamii) na pia si mmiliki wa vyombo vya habari ambavyo angeweza kuvitumia kikamilifu kukabiliana nao.
Na ni kweli kabisa idadi kubwa ya wale waliomo kwenye orodha ya Mengi ni watu wachafu, au wapambe wao. Kuna wengine wamechomekwa tu kwenye orodha ili ionekane ndefu sana.
Aidha nakubaliana na wale wanaosema thread hii ni mojawapo ya zile ambazo huanzishwa kwa lengo la kuwatakasa mafisadi eti kwa kujaribu kuelezea kuwa Mengi naye fisadi tu.
Lakini hili wanashindwa kabisa kuthibitisha hatujapata uthabiti, hata wa kimazingira wa kumfunga Mengi na ufisadi wa kuchota mapesa ya umma kama vile yale ya EPA, Deep Green, Twin Towers, Meremeta n.k.
Wanabakia kusemasema tu mambo yasio na msingi kabisa na diyo maana hata vyombo vya dola havimgusi. Inawezekana alikopa fedha kwenye mabenki (inasemekana alikopa fedha nyingi NBC, wakati benki hiyo ikiwa bado ya umma), lakini kukopa si ufisadi, aliomba, akapewa mkopo, na kama hajarudisha basi hilo ni suala la mdai na mdaiwa na si jinai kamwe.
Kwa kuangalia tu posts hadi sasa, thread hii inaonekana imekwama -- majority wanapinga ufisadi -- na habari ndo hiyo.