Mengi: Kwanini nimemuoa K-lynn

Kwa umri wa huyu baba na uwezo wake kipesa, usitegemee akaoa mke ili wasaidiane kazi. kwa uwezo wake nina imani 200% ya matumizi ya ndani ni juu yake, sasa unataka afue pia wakati mwanamke hata chumvi hununui..!!! Ujanja ujanga wa wanaume wa sasa ndio unapelekea kusema kua maisha sasa hivi ni kusaidiana. Iliandikwa kwenye maandiko yapi kua tusaidiane? mwenyezi mungu alimpa kila mmoja laana yake. Mwanamme ule kwa jasho na familia yako na mwanamke uzae kwa uchungu. Wapi alisema kuna kusaidiana. Msilazimishe kitu ambacho hakipo sababu ya kukimbia majukumu.
Duh kumbe bado anapenda usultani, dunia ya leo bado anahamasisha kufuliwa nguo kupikiwa? raha ya mapenzi kusaidiana na katika hili yeye anaeeza kumfulia pichu yfu wake wakati mwenzake anampikia.
 
Yaani wewe mdada umeongea vizuri mno. ningetamani nikupe like 100 hivi lakini ndio siwezi. waeleze wale ambao wanadhani hsegal ndio kila kitu maana eti wote mnaamka asubuhi kwenda kazini hivyo unachoka. Hivi unawezaje kuchoka kumhangaikia mumeo na watoto wako? sipati picha. Eti wengine humu wanasema Mengi kasahau kua maisha ni kusaidiana. Yaani baba wa watu umri ule aingie jikoni au afue maana mnasaidiana...? ukisikia wanasema hivyo ambao wengi ni wababa, ujue issue hapa ni kukwepa majukumu. baba lisha familia yako, mama tunza familia yako, ndio mpango mzima. mawazo potofu ya kusaidiana achaneni nayo maana labour naingia mwenyewe na kugugumia maumivu mwenyewe kama mwenyezi mungu alivyoelekeza. Nakusaidia kipesa nikiamua lakini si wajibu wako kuanza kulazimisha. Thank you tena mdada.
 
hivi jamani mi naona chenga tu.mnaweza kunitajia jina la mke aliepita wa mengi?na waliachana kwa kisa gani? mbona kimyakimya?na kuna process za kupeana talaka mahakamani walizifuata au?
 

ni ukweli usiopingika kwamba mama ni mlezi/mtunzaji wa familia baba ni mwangalizi na mlishaj wa familia............usalama wa wanafamilia uko mikononi mwa baba, wale nini, wavae nini watibiwe wapi na walale wapi...............kazi ya mama ni kuhakikisha wamekula kilicholetwa, wamevaa vilivyoletwa, wamelaal palipoandaliwa, na wanafya zilizokusudiwa...............

majukumu ya mama katika kutekeleza hayo ndio yanayotufanya tufue, tupike, tudeki, tuoshe vyombo tuogeshe watoto nk.............mie ikiwa kama mume utanisaida basi nisaidie kwamba umependa lkn sio kwamba nimekuomba ama siwez kuzifanya......................binti wa kazi wee ni msaidiz kwangu pale ninapohitaj tu huo msaada ..........

i fell proud familia yangu, kula chakula nilichopika mimi, kuvaa nguo nilizofua mimi, kulala niliposafisha mimi...................ni mtazamo w akizaman lakin kwangu unafanya kazi sana na nimeshauzoe sion shida

Lakin Da Asia kwa yule ambaye hajazooea haya mambo ni ngumu sana kuweza kuyafanya so aina ya makuzi mtu aliyoyapata yana mchango mkubwa sana kwenye hili.

mie mama yangu mpaka leo tukienda nyumban huwa ndo mpish wa chakula anachokula baba, na ndo mfuaji wa nguo za baba yaani ata umwambie mama nikusaidie hatak wla hatak umfulie nguo yake. na yeye huwa haelewi ukimpa mtu nguo yako akufulie kiukweli. sasa fikiria mama ambaye she is 70 anapika chakula cha kula watoto wake na mumewe why not me?
 
Last edited by a moderator:
hivi jamani mi naona chenga tu.mnaweza kunitajia jina la mke aliepita wa mengi?na waliachana kwa kisa gani? mbona kimyakimya?na kuna process za kupeana talaka mahakamani walizifuata au?

Mengi hajawah kumtaliki mkewe Mercy. Bado ni mume na mke, ila zipo sabbu kwann Mengi ameamua kuoa huyu na sio kwamba mercy hajaridhia
 
Tatizo lako unafikiri kazi za nyumbani ni za wake vilaza.., usifanye mchezo na kazi ya kutunza nyumba, kutunza watoto, kupika chakula kizuri, kufua na hapo hapo abaki kuwa mwanamke mzuri...
nani wanafanya hizo kazi za kufua na kupiga na ku baby seat watoto duniani kama sio unskilled women?


hata Faiza ni mkorofi, lakini yaelekea ni mke mwema..., kama Klyn...
Faiza anakujaje hapa, umeshindwa kumuanjia kwenye ma pm huko umeamua kumchomeka hapa? Kama unamwogopa kwenye ma one on one ya pm huko achana nae, kwanza ni religious bigot moja kubwa sana, mimi lilisha ni turn off siku nyingi wala silisomi for the most part.
 
Mengi hajawah kumtaliki mkewe Mercy. Bado ni mume na mke, ila zipo sabbu kwann Mengi ameamua kuoa huyu na sio kwamba mercy hajaridhia

kama hajamtaliki ana uhalali gani wa kuoana na huyu dada wakat ndoa yake ni halali?
 
Mwenye kumwongelea vibaya mwandani wake basi ni punguani...
Kutunziana siri ndo mapenzi....
Na siri za ndani ya ndoa ya mtu waja mwazitakiani.!!!!??
 
Jmn mapenzi ni upofu. Mapenzi ni ujinga na mapenzi ni kila aina ya kituko. Kyln jmn katika akili ya kawaida kuna vijana wangapi saiz yake na walipropose na wakataka kumtuliza. Mbona hakuwaona hao na kuamua kusacrifise happiness yake na Uhuru wake wote kwa mengi a man enough to be her dad. Ni hela jmn. Hata mm Leo hapa kingunge atangaze ndoa nitaolewa jmn. Halafu nitafanya kila anachotaka ilimradi nipate ushuru wote Wa stand ya mabasi ya mkoani. Na vitega uchumu vingine ambavyo nkiwa fresh vitakuwa vinamiminika tuuu. So kyln lazima ajishughulishe ajinyenyekeze ajipretendishe afanye ufake wote mpk mzee aseme kwingine siendi
 
Koz mengi ni type ya mwanaume ambaye ana hela rafiki Mkubwa Wa mwanamke. So anaitumia. So mwanamke ampi shida akizingua anakudelete halafu mwanamke kuachwa na mengi lzma ujutie hiyo chance uliyoipata ukaichezea. So kyln alishaambiwa how huyu mtu alivyo soooo lzma ajitulize na awe mpole. Mapenzi anayabembeleza yeye na ndo anajua nn anataka kwa hiyo atapretend mpk mengi azidi kudata kashaolewa unategemea nn. Na pale kyln kashaona kuwa ndoa sio kila kitu. Koz hata mwanzo mwenzie kaachwa. So inabidi akazane kuitunza ndoa ile isiyumbe. Muombeeni jmn koz saiv ndo yupo kwenye hard tym tena sana. One mistake of she goes pesa itamleta mwingine
 
Hongera K-lyn kwa kuonesha upendo wa dhati toka moyoni
na si ule upendo wa "hapendwi mtu ila pochi"
 
Duh kumbe bado anapenda usultani, dunia ya leo bado anahamasisha kufuliwa nguo kupikiwa? raha ya mapenzi kusaidiana na katika hili yeye anaeeza kumfulia pichu yfu wake wakati mwenzake anampikia.
Uanawake upo pale pale yle ya upande wako kama mwanamke wapaswa kuyatimiza kwa asilimia mia moja
 
Vipi tena haya yote yanatokana na nini?
Kuna mtu kamuulize huyu mzee kuwa kapenda nini kwa huyo kisura!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…