Mengi na Uanachama wake CCM

Kwa maneno mengine Mengi ataacha biashara, aingie kwenye siasa? Hizo ndo sera za JK, au mmesahau?
 
Labda huku kuhamishia uanachama nYUMBANI ndo ule mwanzo wa dalili za ndugu zetu hawa kurudi NCHI YA AHADI (Wanavyoiita wenyewe) pale anapoanza kuzeeka. Ila kama anadhima ya ubunge hapo ndo atapokua anachemka maana Ndesa kifua kipana na si rahisi kumuondolea imani alokwisha kujijengea kwa wananchi wa moshi Mjini hasa kinamama ambao ndio wapigakura wakubwa. Hai nako (Jimbo analozaliwa) nalo si rahisi kivile maana hakubaliki kihivyo hasa ukizingatia amekua na mafanikio muda mrefu bila kuwekeza sana nyumbani. Si miongoni mwa watu wanaokubalika sana Hai na hasa machame anakotoka (Ingawa huku ndiko anakoweza leta upinzani zaidi). So si tishio saana kwa siasa za kilimanjaro.

Angalizo: Mzee huyu anabusara na anahisi anahitaji kulitumikia taifa, sitaki kuamini kama anatamani ubunge maana atakua anajipunguzia himaya. Nataka niamini kwamba, kama anadhima ya kisiasa basi amerudi kujijenga nyumbani ili aweze kuukwaa urais akiungwa mkono kwa karibu na wapambanaji.

Hatukawii kusikia hapa ooh wazee wameniomba maana nchi inaangamia.

Yetu Macho
 
Mengi ashakataa kujiingiza katika siasa, na mpaka juzi hivi alirudia tena kauli hizo wakati akimjibu Sofia. Please mods get rid of this!

Kukataa tu, wala isikupe shida mkuu, labda tafuta defensive point nyingine!! wengi walishakataa lakini baadae wakakifanya kile kile walichokikataa!!! nakumbuka mwanasiasa pekee ambae alikuwa na ujasiri wa kuweka ndoto zake hadharani ni Idd Simba, wengine wote hamna ki2!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…