Kuna mjumbe mmoja mpya wa kamati ya bunge ambayo zamani ilikuwa ujenzi, na sasa ni Miundombinu, anasema kuwa huko kuna ushahidi wa kutosha kuwafunga maisha mzee Mkapa pamoja na Magufuli, kwa hiyo pole pole utaona vitu vinatolewa mapaka atoke!
Kwa vile FMES ni shabiki mkubwa wa JSM (na AKM?) shutuma zake dhidi ya Jaji Waryoba hazishangazi sana. Labda nisaidiwe tu, Waryoba na Malecela walipishana wapi?
Mkulu FMES,
Mzee Mkapa alikukosea nini?kila muda lazima umuandike??au ndiyo hasira za Mzee Butiku na wewe zimekutawala?
FMES,
Jaji Waryoba na Balozi Mahalu walianzisha lini ile firm yao ya UWAKILI?
FMES,
Jaji Waryoba si mmoja wa mafisadi wa NCHI hii. Kama ni urafiki na mafisadi hilo kila mtu kwa wakati fulani kalifanya maana ni vigumu mno kuwajua mafisadi, wezi, wabadhirifu hasa hawa wenye nafasi kubwa katika jamii yetu. Jiulize tu kidogo, kwa nini Malecela mara zote mbili hakufika angalau kwenye tano bora.
FMES,
Jaji Waryoba si mmoja wa mafisadi wa NCHI hii. Kama ni urafiki na mafisadi hilo kila mtu kwa wakati fulani kalifanya maana ni vigumu mno kuwajua mafisadi, wezi, wabadhirifu hasa hawa wenye nafasi kubwa katika jamii yetu. Jiulize tu kidogo, kwa nini Malecela mara zote mbili hakufika angalau kwenye tano bora.
Mkulu FMES,- Wow! wow! now wait a minute wewe Mkulu wangu Gembe, kweli unaona furaha masikini kina Mramba, Yona, na Mgonja wakisota rumande huku Mkapa aliyekua akiwatuma anatesa tu nje kama sio yeye na kujficha nyuma ya immunity ambayo kwanza haipo anyways!
- Sasa unasema na mimi nilikuwa ninatafuta mlo kwa Mkapa kama Butiku? Is that so? Dr. Slaa naye alikuwa anatafuta mlo kwa Mkapa? Mbunge Kimaro naye alikuwa anatafuta mlo kwa Mkapa? Pinda aliyesema Mkapa haogopwi na serikali yake naye alikuwa anatafuta mlo kwa Mkapa?
Mkulu Gembe, hivi vita vya ufisadi naona vinaanza kuku-wear out, wewe tuachie sisi wengine tutaendelea navyo mpaka kieleweke, huwezi ongelea kusafisha mafisadi bila kukamata Mkapa na kumburuza Kisutu, lakini milango iko wazi kama kuna mafisadi tuliowasahau muwataje hapa tule nao sahani moja!
- Mkuu Wildcard labda ufungue topic ya Malecela na kugombea urais hii ni topic ya Mengi VS Warioba, au?
- Mimi hapa nitaendelea na Warioba tu na Mengi, sasa naomba kukuuliza swali vipi hii kesi vipi Warioba mbona hajaifungua dhidi ya Mengi aliyedai amemuharibia jina na yeye sio fisadi?
Mkapa hana Hatia,Kosa lake alikurupuka kujiunga na watu wezi!Vita dhidi ya Mafisadi nipo na wewe mkuu mzee wa sauti ya Umeme mpaka kieleweke!
- Mkuu Kigoma, kwa kawaida huwa ninakuaminia sana, ila kwenye hili inaonekana huna uhakika na unachokisema, maana ungekua na uhakika ungekua unajua kua Warioba ni mbia na Fisadi Mahalu, kwenye law firm, halafu ungekuwa unajua kua kwenye uchunguzi wa kamati yake ya rushwa hakuenda kumchunguza Mahalu kule Elimu na Sayansi,
- Mkuu wangu hivi umeyasikia ya Mwananchi Gold na Warioba au unakurupuka tu ndugu yangu? Hivi unafikiri ni kwa nini mtoto wake wa kike aliyekua akisoma majuu alirudi ghafla bila kumaliza shule?
Pole pole ndugu yangu kama huyajui ni kuuliza, hivi umesikia aliyoyafanya baada ya Yona na Mramba kutinga Kisutu, akihofia na yeye kutinga huko? Hana lolote mgombea wake Salim aliposhindwa urais akatukana sana kuwa rushwa imezidi, lakini Dr. Slaa alipotoa ile list ya aibu akasema ni kuligawa taifa, hana lolote huyu filimbi nyingi lakini na yeye Warioba ni fisadi aliyeshitukia wakati hana nafasi!