- Mkuu Kigoma, kwa kawaida huwa ninakuaminia sana, ila kwenye hili inaonekana huna uhakika na unachokisema, maana ungekua na uhakika ungekua unajua kua Warioba ni mbia na Fisadi Mahalu, kwenye law firm, halafu ungekuwa unajua kua kwenye uchunguzi wa kamati yake ya rushwa hakuenda kumchunguza Mahalu kule Elimu na Sayansi,
- Mkuu wangu hivi umeyasikia ya Mwananchi Gold na Warioba au unakurupuka tu ndugu yangu? Hivi unafikiri ni kwa nini mtoto wake wa kike aliyekua akisoma majuu alirudi ghafla bila kumaliza shule?
Pole pole ndugu yangu kama huyajui ni kuuliza, hivi umesikia aliyoyafanya baada ya Yona na Mramba kutinga Kisutu, akihofia na yeye kutinga huko? Hana lolote mgombea wake Salim aliposhindwa urais akatukana sana kuwa rushwa imezidi, lakini Dr. Slaa alipotoa ile list ya aibu akasema ni kuligawa taifa, hana lolote huyu filimbi nyingi lakini na yeye Warioba ni fisadi aliyeshitukia wakati hana nafasi!