Mengi yaibuka kiwango cha Simba kwenye mashindano ya kombe la Mapinduzi

zanzibar kuna ligi ya ajabu sana nadhani ni yakipekee duniani

kila siku ligi inachezwa tena mechi zinaanza saa mbili asubuh mpaka jion

zawadi za bigwa wa ligi ni sawa na zawadi anayopewa mchezaji bora ligi kuu bara[emoji16][emoji16][emoji16]
 
kawaida timu nzuri inapocheza na timu mbovu lazima ionyeshe kiwango kibovu kiwango cha simba utakijua vizuri pale watakapokutana na timu nzuri
 
Daah! Yanga tunawaza club bingwa bara Africa simba wanawaza namna ya kurudi toka Zanzibar kwa aibu kubwa
 
Kundi la Simba lina timu tano, la Yanga lina timu nne. Kwa hiyo pamoja na kuongoza kwa pointi saba, Simba bado hajapata tiketi ya kucheza nusu fainali
 
Mkuu sishangai kuona wanayanga hawapendi simba ashinde ila nashangaa mnavyotokwa mapovu kuonyesha kuwa simba anabebwa.. Hivi kwa hapa bongo kuna timu inayobebwa kama vyura fc? Kuna maamuzi mabaya ya refa ya kumfikia mwamuzi wa yanga na simba walipokuta au yanga na castal union pale tanga? Kuna timu inayopenda point za mezani kama yanga? Hata kama mnaona mkifungwa mnadhalilisha chama ila msizidishe kununua matokeo... Kama mngekuwa na timu ya maana basi kule caf mngetolewa kwa idadi ya magoli ya nyumbani na ugenini... Simba ni kweli haichezi kwa kiwango kizuri ila si kwamba ndo ukatae magoli halali kisa simba kashinda.. Mbona husemi penat mnazowekewa na mnakosa ingekuwa simba sijui mngesemaje
Mi naona unatokwa bovu tu halafu unatemea wenzio.

Simba ingekuwa timu bora ingekuwa msindikizaji kwenye vpl? Bora hata azam wajitape kuliko nyinyi , kazi yenu kipiga mayowe wenzenu twaa ma makombe kila uchao...chezea yanga wewe
 
Usijali mkuu maana najua kauli mbiu yenu vyura fc ni lazima uwe mbishi kiasi cha kuweza kubishana na radio so sikushangai komaa mkuu utajulikana tu
 
Kuendelea kucheza kwa kiwango cha chini kwenye mashindano ya Kombe la Mapinduzi yanayoendela Zanzibar kwa mabingwa zamani wa mashindano hayo kumeibua mambo mengi kutoka kwa baadhi ya wadau wa mchezo huo hapa nchini.

Licha ya kuchezesha kikosi cha kwanza kinachojumuisha wachezaji wao wa kimataifa team hiyo imekuwa ikishindwa kuonyesha kiwango kizuri na matokeo yake kupata ushindi kiduchu kwenye michezo yake.

Simba imeteremka mara 2 kwenye mashindano hayo na kushinda 2-1 na 1-0 dhidi ya team dhaifu za Taifa Jang'ombe na KVZ respectively, huku ushindi wa jana dhidi ya KVZ ukilalamikiwa kuwa haukuwa halali kwakuwa walifunga goli la Offside.

Mdau mmoja wa mchezo huyo ambaye amekuwa akihudhuria match zote za mashindano hayo alisikika akiuliza inakuwaje Simba inayocheza kiwango kibovu hivyo kuongoza Ligi kuu ya Bara ambayo Zanzibar nzima wanaijua kuwa ni ngumu.

Bwana Mohamed Fakhi wa Kibandamaiti naye alisikika akilalamika kutomuona mchezaji anayeongoza kwa kuzifumania nyavu kwenye ligi kuu bara, na kulaumu team hizi kubwa za Bara kwa kudharau haya mashindano na kuwaacha wachezaji mihimili Dar. Hata hivyo alipothibitishiwa kuwa mfungaji huyo muongozaji anayekwenda kwa jina la Shiza Kichuya yupo na amecheza match zote alipigwa na mshangao mkubwa kwa kutoona vitu vyake ambavyo amekuwa akivisikia anavifanya huko kwenye Ligi ya Bara.

Aidha wadau wengine walifika mbali na kuzitaka mamlaka husika kufuatilia mwenendo wa team hiyo kwenye ligi kuu ya mwaka huu Bara wakitilia mashaka matokeo ambayo wamekuwa wakiyapata ambayo kihalisia hayafanani na kiwango chao halisi cha uwanjani, "kwa namna Simba walivyopania kumaliza ukame wa kutwaa ubingwa wa Bara,huenda wakawa wanatumia mbinu mbadala za kuwawezesha kufanikisha hilo.

Haiwezekani team ikawa na kiwango duni hivyo kama inavyothibitika uwanjani hlf ikawa inaongoza Ligi" alisikika akilalamika mdau mwingine ambaye hoja yake iliungwa mkono na Mshabiki mmoja aliyejitambulisha kwa jina 1 la Ahmed ambaye alisema kwa kiwango hiki hata Simba ingekuwa inashiriki ligi kuu ya Zanzibar inayojulikana kuwa ni nyepesi isingeweza kuwa hata kwenye Top 3.

Naomba kuwasilisha.
Sema sasa mbona leo hujasema kiwango chenu.......kazi kujadili timu za wenzenu..nyambafuiu
 
Hao wanaitwa makozimeni. Kazi yao kuchungulia na kusema mambo ya wengine. Wakipigwa huwaoni na uchunguzi wa timu yao na mienendo yake lakini wepesi wa kuizungumzia Simba.
Mleta mada mvimba macho leo sijui yuko wapi atupe tathimini ya timu yake.
 
c3a4affa2cd1f832f7ce8b598d5d3987.jpg
 
Kuendelea kucheza kwa kiwango cha chini kwenye mashindano ya Kombe la Mapinduzi yanayoendela Zanzibar kwa mabingwa zamani wa mashindano hayo kumeibua mambo mengi kutoka kwa baadhi ya wadau wa mchezo huo hapa nchini.

Licha ya kuchezesha kikosi cha kwanza kinachojumuisha wachezaji wao wa kimataifa team hiyo imekuwa ikishindwa kuonyesha kiwango kizuri na matokeo yake kupata ushindi kiduchu kwenye michezo yake.

Simba imeteremka mara 2 kwenye mashindano hayo na kushinda 2-1 na 1-0 dhidi ya team dhaifu za Taifa Jang'ombe na KVZ respectively, huku ushindi wa jana dhidi ya KVZ ukilalamikiwa kuwa haukuwa halali kwakuwa walifunga goli la Offside.

Mdau mmoja wa mchezo huyo ambaye amekuwa akihudhuria match zote za mashindano hayo alisikika akiuliza inakuwaje Simba inayocheza kiwango kibovu hivyo kuongoza Ligi kuu ya Bara ambayo Zanzibar nzima wanaijua kuwa ni ngumu.

Bwana Mohamed Fakhi wa Kibandamaiti naye alisikika akilalamika kutomuona mchezaji anayeongoza kwa kuzifumania nyavu kwenye ligi kuu bara, na kulaumu team hizi kubwa za Bara kwa kudharau haya mashindano na kuwaacha wachezaji mihimili Dar. Hata hivyo alipothibitishiwa kuwa mfungaji huyo muongozaji anayekwenda kwa jina la Shiza Kichuya yupo na amecheza match zote alipigwa na mshangao mkubwa kwa kutoona vitu vyake ambavyo amekuwa akivisikia anavifanya huko kwenye Ligi ya Bara.

Aidha wadau wengine walifika mbali na kuzitaka mamlaka husika kufuatilia mwenendo wa team hiyo kwenye ligi kuu ya mwaka huu Bara wakitilia mashaka matokeo ambayo wamekuwa wakiyapata ambayo kihalisia hayafanani na kiwango chao halisi cha uwanjani, "kwa namna Simba walivyopania kumaliza ukame wa kutwaa ubingwa wa Bara,huenda wakawa wanatumia mbinu mbadala za kuwawezesha kufanikisha hilo.

Haiwezekani team ikawa na kiwango duni hivyo kama inavyothibitika uwanjani hlf ikawa inaongoza Ligi" alisikika akilalamika mdau mwingine ambaye hoja yake iliungwa mkono na Mshabiki mmoja aliyejitambulisha kwa jina 1 la Ahmed ambaye alisema kwa kiwango hiki hata Simba ingekuwa inashiriki ligi kuu ya Zanzibar inayojulikana kuwa ni nyepesi isingeweza kuwa hata kwenye Top 3.

Naomba kuwasilisha.
af0833cfa13b8639031a9d6347cf83fd.jpg
 
Unawasilisha nn sasa? Hujaeleweka, tutoe bac maan n point zako tu znatutoa hapa
 
Halafu KVZ wamesema wao ni timu changa na kuingizwa mapinduzi cup ni kama kujenga uzoefu (mazoezi) mechi zao mapinduzi cup ni kama bonanza, simba wameshindwa kuifunga hata goal moja la halali, inamaana firimbi ingepulizwa wangetoka suluhu.
Yanga walivocheza na simba ligi kuu je?
 
Back
Top Bottom