Angalizo: mimi sio daktari wa wanawake na wala sio mtaalamu wa kiswahili
Hii ni maada ambayo haiongelewi kwa upana wake nchini, yawezekana ni sababu ya kukosa maarifa, au watu wanaona kawaida na kuishi na maumivu yao kama nyakati ambazo hakukua na suluhu au wengi wa wanawake hawapitii hayo katika jamii ya watanzania
Mimi kama mwanamke ambaye ni mkoma hedhi ajaye, ningependa wenzetu ambao wamepita huko na wapo huko wanamudu vipi kuendelea kuishi maisha yao kila siku
Hapa naongelea ambao ukomo wa hedhi umetokea kwa sababu ya umri wa kibaolojia ( sio wale ambao imetokea sababu ya operation au dawa)
Kwa ufupi mpaka kufikia ukomo wa hedhi wa kudumu kuna mabadiliko yanatokea
Peri menopause (kabla ya uko wa hedhi)
Haya ni maandalizi kabla ya ukomo wa hedhi, kwa wengi inawatokea miaka 7-14 kabla ya ukomo wa hedhi.
Inatokea sana kwa wanawake walio 40s na baadhi inaanza 35+
Mara nyingi hali hii inaambatana na baadhi ya mambo yafuatayo (provided maisha yako hayajabadilika kwa kiasi kikubwa)
1. Hedhi kupoteza mtiririko
2. Joto kali (hot flashes)
3. Maumivu makali ya mwili especially joints (aches)
4. Uke kuwa mkavu sana, kupoteza hamu ya tendo
5. Magonjwa ya njia ya mkojo ya kujirudia rudia (UTI)
6. Sonona, kusahau sahau, kukosa umakini, kukosa mental clarity
7. Kuongezeka uzito kupitiliza
Menopause:
Ukomo wa hedhi kwa mwaka mmoja mfululizo
Post Menopause:
Mara nyingi miaka 50-55
Hii ni kwa maisha yako yote yaliyobaki bila hedhi. Wapo ambao wanabahatika maisha yanaendelea kama kawaida na maudhi machache ya hapa na pale.
Pia wapo ambao mambo yanakua magumu kiasi kwamba maisha ya kawaida inakua ni afadhali ya jana.
1. Wenzetu ambao mnapitia na mmepitia huko mmewezaje na mnawezaje maisha yenu ya kila siku?
2. Mngependa kitu gani kifanyike cha tofauti kwa sisi ambao tupo kuelekea safari hiyo?
3. Mnawezaje kumudu mabadiliko haya kwenye mahusiano yenu ya ndoa au uchumba sugu???
4. Kwa wanaume au mabinti ambao bado, una uzoefu na mtu wako wa karibu alivyobadilika kipindi hichi? Ilikuwaje?
Kwa elimu zaidi mnaweza pitia links hapa chini
View: https://youtu.be/Cgo2mD4Pc54?si=mvtPl4hH9PpKm9VE
View: https://youtu.be/oQqcnYcKx68?si=78J5YjSA2B_jBDQm
Nakaribisha wadau, mods naomba mpin huu uzi sababu ni kitu endelevu wengine ukifika wakati wetu tungependa kuchagua