Men’s essentials

Men’s essentials

Nyani Ngabu

Platinum Member
Joined
May 15, 2006
Posts
94,296
Reaction score
122,540
Sijui ni wangapi mnajua kuhusu hii bidhaa.

Bidhaa yenyewe ni ‘body powder spray’.

Ni poda [powder] ambayo unajipulizia mwilini: kwenye mabega, mgongoni, kifuani, chini ya makwapa, na kadhalika.

Kazi yake kuu ni kufyonza/ kukata jasho.

Kwa vile huja kwa aina za manukato mbalimbali, pia huufanya mwili unukie vizuri.

Body powder spray siyo mbadala wa kiondoa harufu za kwapani, yaani deodorant na antiperspirant deodorant.

Body powder spray hutumika kama kitu cha ziada kwa hivyo viondoa harufu.

Zipo za wanawake na za wanaume. Hapa nazungumzia za wanaume.

Kama hujawahi kutumia hii bidhaa, nakushauri ujaribu siku moja. Hususan kama upo eneo lenye joto na jua kali kama Dar, Mtwara, Lindi, na kwingineko.

4C36F129-A16A-42E2-884C-0A9C9E8BD688.jpeg
118BE42A-FBEA-4EE9-AD99-D6AAC5780079.jpeg
 
Nadhani nimewahi kuiona ila sikuwahi kuichukulia seriously, ngoja nitainunua...
 
Ukijipulizia haupauki kama poda ya kawaida?
 
Ukijipulizia haupauki kama poda ya kawaida?

Unapauka.

Lakini hii ni ya kujipaka/ pulizia sehemu ambazo hazionekani, kama vile mgongoni, kwenye mapumbuuu, tumboni, ubavuni, na sehemu zinginezo kama hizo.

Mwili ukishapata moisture kidogo tu huko kupauka kunapotea na jasho unakuwa hutoki kivile.
 
Inafaa sana kwakwel..
Ngoja nijaribu kutafuta kama ntapata
Unapauka.

Lakini hii ni ya kujipaka/ pulizia sehemu ambazo hazionekani, kama vile mgongoni, kwenye mapumbuuu, tumboni, ubavuni, na sehemu zinginezo kama hizo.

Mwili ukishapata moisture kidogo tu huko kupauka kunapotea na jasho unakuwa hutoki kivile.
 
Zipo za wanawake na za wanaume. Hapa nazungumzia za wanaume.

Kama hujawahi kutumia hii bidhaa, nakushauri ujaribu siku moja. Hususan kama upo eneo lenye joto na jua kali kama Dar, Mtwara, Lindi, na kwingineko.

View attachment 959849View attachment 959850

Ooh kumbe ziko za kike pia, nilijua ni mambo ya kiumeni tuu.

Ulishawahi kupigwa na jua na joto la Lindi na Mtwara?

Ila harufu ya kikwapa taaamuuuu.... 😛😛😉

K' Matata.
 
Ooh kumbe ziko za kike pia, nilijua ni mambo ya kiumeni tuu.

Ulishawahi kupigwa na jua na joto la Lindi na Mtwara?

Ila harufu ya kikwapa taaamuuuu.... 😛😛😉

K' Matata.

Mtwara ndiko nyumbani. Pande za Ligula pale..
 
Hivi nivea hawana hii kitu kweli!

Niliwahi kununua spray ya nivea nikispray inakua kama powder,
Nikajua ime expire
 
Back
Top Bottom