Mercedes Benz C Class (W205) hii chuma Wajerumani walituliza vichwa. Hadi sasa naamini ndio the best katika segment yake

Mercedes Benz C Class (W205) hii chuma Wajerumani walituliza vichwa. Hadi sasa naamini ndio the best katika segment yake

Mad Max

JF-Expert Member
Joined
Oct 21, 2010
Posts
26,961
Reaction score
77,890
Wakuu.

Katika segment ya compact executive cars tunakutana na wakali wengi sana, mfano BMW 3 series, Mercedes Benz C Class, Audi A4, Volvo S60, Genesis G70, Lexus IS nk.
IMG_0215.jpeg

Yote tisa, hii generation ya nne ya Mercedes Benz C Class, W205, iliyoanza mwaka 2014 hadi 2021 ni namba nyingine kabisa.
IMG_0223.jpeg
IMG_0224.jpeg

Wengi wamekua wanaipambanisha na BMW F30 ila tukiacha mapenzi pembeni, muonekano wa F30 ni improvement ndogo sana kutoka E90, ila muonekano wa W205 ni improvement kubwa sana kutoka generation iliotangulia W204.
IMG_0216.jpeg


Improvement haijaishia kwenye muonekano tu, ila ata handling, technology, efficiency na power za hii W205 ni upgrade kubwa sana.
IMG_0217.jpeg

Kingine nnachowapendea Benz wametoa aina nyingi sana za engine kwenye hii class, kuanzia Diesel, Petrol hadi Hybrid.
Kwa mfano, hapa una selection ya engine ziguatazo:

Petrol:
  • 1.5 L M264 turbo I4
  • 1.6 L M270 turbo I4
  • 2.0 L M274 turbo I4
  • 3.0 L M276 twin-turbo V6
  • 4.0 L M177 twin-turbo V8
Petrol hybrid:
  • 1.5 L M264 Mild-Hybrid turbo (EQ Boost) I4
  • 2.0 L M139 Mild-Hybrid turbo (EQ Boost) I4
  • 2.0 L M264 Mild-Hybrid turbo (EQ Boost) I4
  • 2.0 L M274 PHEV turbo I4
Diesel:
  • 2.1 L OM651 turbo I4 & Bluetec Hybrid
  • 1.6 L OM626 turbo I4 & Bluetec
  • 1.6–2.0 L OM654 turbo I4
Diesel hybrid:
  • 2.0 L OM654 turbo I4 PHEV.
IMG_0225.jpeg
Kama utakua makini, kumbuka kuanzia miaka hii ya 2014 BMW wanatoa F30 generation, walikua wameacha kutengeneza engine za V8 katika hii class, ila Benz aliendeleza kutuletea Mercedes Benz AMG C63, 4.0L V8.
IMG_0221.jpeg

Tunapishana nazo mjini, tatizo TRA ndio wanaweka vikwazo, kwani entry level C200 ya 2014 unalipia ushuru Mil 12, wakati ukiitaka kutoka JP utatakiwa kutuma $6,000 minimum.

Kuna Watanzania wanaziuza, either showroom au walizotumia ila jiandae kupasuka Mil 50 kuendelea kwenye mashowroom.
IMG_0214.jpeg

Kuna baadhi namba E inamanaisha zimetumika kidogo kuanzia 2023 maybe hapa, naona zipo kwenye 30 - 40 Million.
IMG_0226.jpeg

Kwa miaka ya 2010 hadi 2020 naamini hii ndio best car katika segment yake.
 
I4
2.0 L M274 turbo I4
3.0 L M276 twin-turbo V6
4.0 L M177 twin-turbo V8
Petrol hybrid:
1.5 L M264 Mild-Hybrid turbo (EQ Boost) I4
2.0 L M139 Mild-Hybrid turbo (EQ Boost) I4
2.0 L M264 Mild-Hybrid turbo (EQ Boost) I4
2.0 L M274 PHEV turbo

Wajerumani huwambii kitu bila kutumia turbocharger hawa jamaa magari Yao yote ni kutunisha misuli tu
 
Uliitupa wapi nkaokote bro....
Ni mwezi uliopita naona kwa sasa imeisha chunwa na kuuzwa kiti peke yake ila noana imeushatafunwa na chuma huko scrap yard
Niliwapigia simu wakaja kuibeba
Ilikuwa haina thamani tena maana kuitenheneza ingekuwa gharama kubwa kama 3m ya bongo
Acha iende tu, ila kwa Africa nawaaminia wangeweka hata gearbox ya Honda
 
Hiyo classic. Ukimpata mtaalamu akaitengeneza unaiuza safi
Mkuu ni hapa UK nimeipeleka kwa fundi wa kwanza akaniambia hizi A class za miaka ya nyuma gearbox zake walichemsha
Kuitengeneza anaweza ila itanigharimu kama £900 akashauri niachane nayo.
Wa pili alipo diagnosed akasema baba itupe tu haina thamani tena
Nikaamua kuwapigia watu wa scrap yard waibebe kwa laki 7 sh
 
I4
2.0 L M274 turbo I4
3.0 L M276 twin-turbo V6
4.0 L M177 twin-turbo V8
Petrol hybrid:
1.5 L M264 Mild-Hybrid turbo (EQ Boost) I4
2.0 L M139 Mild-Hybrid turbo (EQ Boost) I4
2.0 L M264 Mild-Hybrid turbo (EQ Boost) I4
2.0 L M274 PHEV turbo

Wajerumani huwambii kitu bila kutumia turbocharger hawa jamaa magari Yao yote ni kutunisha misuli tu
Ni hatari hao hadi L 1.3 usishangae kukuta turbo
 
Back
Top Bottom