JanguKamaJangu
JF-Expert Member
- Feb 7, 2022
- 2,780
- 6,607
Kampuni ya Mercedes-Benz, Ijumaa ya Mei 20, 2022 iliweka rekodi ya kuuza gari la gharama zaidi Duniani, ambalo ni Mercedes-Benz 300 SLR ‘Uhlenhaut Coupe’ ya mwaka 1956 kwa kiasi cha dola milioni 142.7 sawa na Tsh. bilioni 330.
Kabla ya hapo gari aina ya Ferrari 250 GTO ya mwaka 1963 ndilo lilikuwa gari la gharama zaidi, mwaka 2018 liliuzwa kwa kiasi cha dola milioni 70 sawa na Tsh. bilioni 162.
Gari hilo limeuzwa katika mnada ambao waliokaribishwa katika manunuzi yam nada huo ni watu 10 pekee. Mnunuaji hajawekwa wazi lakini amekubali taarifa hizo ziwekwe hadharani
Pesa zilizopatikana katika mauzo ya gari hii zitatumika kuanzisha mfuko wa Mercedes Benz kwa ajili kusaidia ya wanafunzi katika masomo ulimwenguni.
Source: Supercarblondie