Meremeta 00:00:00. EXTRA

Status
Not open for further replies.


Mkuu FMEs, shilingi 30,000 ni robo ya mshahara wa mfanyakazi wa serikali na baadhi ya taasisi binafsi nyingi tu hapa nchini hivyo siyo fedha kidogo. Mwanakijiji ameuza ripoti ya Meremeta kwa bei ya kulangua
 

Hakika umenena
 


UKWELI NI KWAMBA KILA MMOJA ANAJIPANGA NAMNA YA KUJIBU. Wakati wa media kupick hili bado na pengine wahariri ni wavivu wa kusoma kama ilivyo kawaida yetu tulio wengi. Hata hivyo ni risk kubwa kwa media kwa sababu serikali inaweza kuamua kufa naye atakayejitokeza adherani na hii riport kwa kisingizio cha wizi wa nyaraka za siri za serikali. Kila mmoja anatahadhari ya kivyake. Nimefurahishwa na jibu hili

Kwanini ulitegemea hivyo? Mimi sikutegemea hivyo. just FYI wengi wao waliniuliza kama wangeweza kuirusha... jibu langu limezuia hiyo.

Tuna haraka sana, ukitaka haraka unabeba bunduki yako unaenda kwenye kikao cha kamati kuu ya sisiem na unafanya vitu vyako ndipo utapata majibu ya haraka. Harakati zenye hekima kama hizi za mwanakijiji zinahitaji subira kubwa na wote wenye busara wanafahamu hili.
 

Ndugu yangu Dar es salaam, Wasema kweli daima huonekana wakorofi. japo Mwanakijiji na timu yake wanataka tuunge mkono tu na kuwapamba lakini mwitikio kidogo wa vyombo vya habari ni ishara tosha kuwa ripoti imeonekana kuwa siyo ya uchunguzi wa kina. Ilidaiwa kuwa ripoti itakuwa na ushahidi mzito na vielelezo ambatisho, mmmmmh mimi sijakutana navyo kama tulivyoelezwa awali na Mwanakijiji kabla ya kuilipia, lakini zaidi aliikweza sana ripoti hii na hadi kufikia kuiuza
 


Dah!!!!!!!!!!!!!!!!!
 

Wewe ulitegemea kukutana na vielelezo gani? Wabongo mbona mnapenda ku-criticize sana?
 

Kwa hali hii kweli Tanzania tunamwendo mrefu wa kuleta mageuzi,kuna watu wanamacho lakini hawaoni,wanamasikio lakini hawasikii.Sasa kama kilichopo kwenye ripoti hakitoshelezi wewe mchango wako ni upi ili ripoti ijitosheleze.

Tusiwe wepesi wa kukritisize tutoe michango ya mawazo na vitendo kuboresha juhudi za kumkomboa mtanzania toka kwenye kongwe la ukandamizaji.Binafsi nimeiona ripoti na on the balance of probabilities kama shutuma zilizopo ndani hazijibiwi kwa ufasaha,serikali iliyopo madarakani itabidi iwajibike kwa kuukalia uvundo huu.
 


Wadau baada ya Meremeta, tuanza kuwakama watoto wa mafisadi ili warudishe hela zetu. tumechoka kweli tena. Kidnapping will solve the matter
 
Wadau baada ya Meremeta, tuanza kuwakama watoto wa mafisadi ili warudishe hela zetu. tumechoka kweli tena. Kidnapping will solve the matter

that will not solve the issue. Hela zimeshakwenda na kuliwa. All we can do is start with a new clean slate. Bila hilo, tutabaki tukiumizana tu. Tuige mfano wa Mandela. Wewe unadhani angeamua kulipa injustices zote, leo SA kungekalika? Sometimes you have to be the bigger person, and say we forgive you. Turudishe tunachoweza...mfano kuvunja mikataba hovyo, lakini kudai personally sio sawa. Hata ukisilikiza audio ya MWJJ inasema hatutaki mali zao, bali tunataka resources zetu. Tukianza kudai katika personal level, itakuwa ngumu kuwatoa hapo.
 
Sorry Mkjj kuuliza

Hatupati kabisa hii kitu sie akina hohe hahe? maana nilijua eventually watu wakipata na sie tupewe walau na sie tupate hoja au somo hilo la wizi wa kodi zetu ambazo wengine zinatufanya hata kununua kopi hii inakuwa shida au inakuwaje maana tunahitaji uhasishaji kama huu ingawa wakati mwingine majukumu yanakuwa yamebana kiasi chake au watu 150 bado au badi una list ingine tena ya kuongeza may waombaji wameongezeka?.

I appreciate you all effort man
 
Bandugu,

Hii ripoti ya Meremeta kupitia Cheche bado inapatikana? Kivipi?
 
wakuu si mshaisoma......wekeni torrent au rapidshare tuinyonye....
 
Huwa tunapata doc za ufisadi kwa namna tofati leo hii haipatikani kabisa; mwanakijiji achia kidogo basi; au umewapiga ganzi hata wale walio lipia tayari? inakuwaje; nataka kusambaza ujumbe ila sina documents mkuu
 
Huwa tunapata doc za ufisadi kwa namna tofati leo hii haipatikani kabisa; mwanakijiji achia kidogo basi; au umewapiga ganzi hata wale walio lipia tayari? inakuwaje; nataka kusambaza ujumbe ila sina documents mkuu


duh.. wenzio wameanza kudownload hapa masaa kadhaa yaliyopita. Angalia threads za hapa..
 
Status
Not open for further replies.
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…