Tunawashukuru kwa mwitikio wenu lakini kwa hakika mmetupa kibarua kipya kabisa na kazi imekuwa ngumu katika hiyo ripoti. Kutokana na ongezeko kubwa la watu wapya ambao wangependa kupata ripoti hii hasa wale ambao ndio wamepata tu taarifa zake tumeamua kuongeza nakala 50 tu hadi hii Ijumaa.
Maelezo ni yale yale na utaratibu ni ule ule wa kupata.
Pamoja na hilo, jana nilizungumzia kwanini tumefanya hili tulilolifanya na tunasukumwa na kitu gani ili kusiwe na utata wowote.
Sikiliza:
juuyameremeta.MP3 - Bonyeza
Inapatikana hivi:
Ripoti inapatikana kwa njia ya pre-ordering (yaani order zikishatimia zote zinatolewa kwa wakati mmoja) kwa wale ambao watachangia dola 30 au shilingi elfu thelathini tu au zaidi kwa njia zifuatazo:
- Kupitia Mtandao wa http://www.mwanakijiji.com kuna kitufye cha kuchangia upande wa juu kulia (Donate Button) cha Paypal Inc., kwenye ukurasa wa mbele (homepage - siyo ukurasa wa forum). Hapo tunaweza kupokea malipo ya kadi za kibenki katika njia ya usalama wa hali ya juu na wachangiaji wote wanamakia sirini (rekodi yetu ya miaka mitatu hatujawahi kuvujisha jina la mchangiaji yeyote yule!).Kadi za Visa, MasterCard, Express zinapokelewa.
- Kwa taasisi au watumishi wa umma (VIPs) ambao kwa sababu za wazi wangependa kutojulikana wasiliana nami kwa email au Private Message na utapata maelezo ya kuwasiliana na Mwandishi wa Habari Mchunguzi wa gazeti la kiingereza la kila siku la nchini aliyepo Tanzania ambaye atapokea fedha hiyo pamoja na email yako ambayo tutakutumia nakala hiyo katika usiri mkubwa. Yeye pia anaweza kupokea kwa njia ya Western Union kwa wale ambao wangependa kutumia njia hiyo.
- Kwa mtu mwingine yeyote tuma fedha kwa njia ya recharge vouchers kwenda namba: 0713444649. Vouchers ziwe ni za tiGO, Zain au Zantel.
Kama mipango yote itakwenda ilivyo, basi tunatarajia kutuma nakala hizo 100 siku ya Jumatano wiki hii kwa wale waliochangia. Hivyo ina maana watu wana siku tano za kukamilisha oda zao. Pamoja na ripoti hiyo, tumeambatanisha pia ripoti yetu ya 2006 juu ya Tracing Reports of Tanzanias role in arms trafficking.
Oda nakala yako mapema kwani tutafanya kwa mtindo wa aliyewahi mpe
first come, first serve.
NB: -
Email moja kwa nakala moja.
- Hakuna nakala itakayotangulia mchango; na hakuna mtu atakayepata nakala kabla ya watu wengine. Watu wote watakaokuwa wamechangia watapata nakala zao Jumatano. NO EXCEPTION.
Shukrani
M. M. Mwanakijiji
Consortium of Concerned Tanzanians Intl.
+ 1 248-556-6748
unaweza kwenye email ya
mwanakijiji ati jamiiforums dot com
[/CENTER]