Meremeta 00:00:00. EXTRA

Status
Not open for further replies.
Nani alisema misemo ya wahenga huanguka! Si imesemwa " Ukweli hata ukiuzika chini kiasi gani, bado utatafuta njia ya kuibuka" (No matter how deep you bury the truth, it will always manage to surface), sasa ndio wakati wa ukweli kuibuka, hongera mzee mwanakijiji na Jopo zima la Cheche za Kifikra!
 
Mwanakijiji,
Kama ulivyokwisha eleza mapema, haya malipo ni walau yaweze ku-subsidize gharama za kazi kubwa mliyoifanya. Kama ndivyo, kwa nini uwawekee limitation (100 copies) watu ambao wako tayari kulipa ili wapate ripoti hiyo? Nitakuwaje na uhakika kuwa nikilipa hizo sh 30,000/= nitakuwa miongoni mwa hao 100 watakaopata nakala?
 
MMJ,
hongera sana mzee kwa kazi unazozifanya za kuonyesha udharimu wa utawala wetu, ila tu mimi nina wasiwasi kidogo na upatikanaji wa hii document, nataka niweke wazi kwamba 99.99% ya wachangiaji humu kwenye forum siwajui akiwemo MMJ na hili ndilo limewapa ujasiri mkubwa wengi wetu ku-dare to speak their mind...leo hii huu utaratibu liowekwa unaendana kabisa na kureveal our identity..tukumbuke hivi karibuni kuna mtu alileta thread ikimuelezea MMJ kuwa ni mtu gani, sitaki kuipinga sana ile thread wala kuikubali lakini inanipa wasiwasi kidogo katika kusubmit our details while tring to buy the document, suala la gharama it is reasonable lakini wasiwasi wangu ni upatikanaju wake........ni dukuduku langu tu otherwise kama ingepatikana namna ya kumwaga hadharani hiyo ishu hapa ingekuwa ni fresh...

wazo langu la mwisho...Jamii forum inunue haki za hiyo document kutoka kwa MMJ kwa michango ya wanachama, kwakuwa kutoka na MMJ watatoa copy 100 kwa 30$ this is equal to 3000$, na hapa ndani kuna watu wangapi ambao hata tukichangia $5 kila mmoja zinafika hizo na kuipa jamii forum uwezo wa kununu hiyo document halafu ikaweka hapa na ikawa limited tu kwa few users, i am sure this can be arranged...
 
Ni kweli
 
Mwanakijiji,

Mimi dola 30 zangu ziko njiani (hewani) kuja kwako. Nataka niwe miongoni mwa wale wenye copy hii. Ikifikia hatua ya kuisambaza bure pale jangwani na mnazi mmoja, nitakuwa miongoni mwa paper nuts......IYWI
 

Good idea but it will take time to organise. Nataka by kesho niwe nimeisoma
 
Na pia kuhakikisha linafanyiwa shughuli, nilikuwa napendekeza nakala za bure kwa wabunge. Mnaonaje?

bure kwa wabunge!? tena hawa ingebidi wachangie zaidi maana tumefanya kile ambacho wao wameogopa kukifanya (ukiondoa wachache wao).
 

hii isiwe shaka; hakuna mtu atakayechangia ifikapo J'tano ijayo ambayo hatapata nakala. Tumeweka hiyo limitations ya 100 kutupungizia mzigo wa kuserialize na kuprotect kila document.
 

Katika maisha kuna risk taking; We took the risk to do what we are doing, somebody else has to take some risk. Without taking risks hakuna mabadiliko ya kweli.


Wazo hili zuri lakini hizo haki haziuzwi, sorry.
 
Mkuu MKJJ,

hakuna "sneak-peek" angalau ya a couple of paragraphs?
Mimi nakala yangu itabidi unishushie mtaani ukipiga raundi...$ thelathini
yako inakusubiri.

Big ups to what you are doing bro!

Mwalimu.. I have put some excerpts kwenye post ya kwanza kuwadokeza tu sehemu ya uhondo uliomo..
 

i also salute you brother
 
Ka"nzi" kamechoka baada ya kukaa kwa madiba karibu wiki nzima!
Mkuu MKJJ,
Kumbe ka 'nzi' kalikuwa huku bondeni kwa karibu wiki nzima, ningejua kanakuja ningekatuma "kauleth' umushini wami"; hehe!
Hongera kwa kazi nzuri ya kuipigania nchi yetu.
 
Mkuu MKJJ,
Kumbe ka 'nzi' kalikuwa huku bondeni kwa karibu wiki nzima, ningejua kanakuja ningekatuma "kauleth' umushini wami"; hehe!
Hongera kwa kazi nzuri ya kuipigania nchi yetu.

wakati mwingine kanishtua kuwa kako mitaa fulani..
 
'I think the reason why people don't vote is because the politicians are all so central now, it doesn't seem to matter who you vote for
 
Mwanakijiji iwapo taarifa zimefahamika kwa nini watu tununue hizo taarifa na tusipewe bure?

Je Watanzania wasioweza kuchangia hizo dola 30 lakini wanataka kufahamu huo uozo wa meremeta wafanyeje? ilhali kuna watanzania wanaufahamu huo uozo lakini wanauza hata taarifa?.

Mimi ninapinga kwa nguvu zote, hatua hii ya mwanakijiji kuuza hizi taarifa muhimu, taarifa za kuwakomboa watanzania lakini zinageuzwa kuwa za kuuzwa instead.

Kwa jinsi hizi taarifa zilivyo muhimu, thamani yake ni kubwa sana kiasi kwamba hizi dola 30 zitakwamisha lengo la kumkomboa Mtanzania aliye masikini ajabu (dola 30 kwake ni mshahara wa mwezi).

sana sana kinachofanyika kwa hizi dola 30 ni kutugawa Watanzania katika kundi la walionacho na wasionacho linapokuja suala muhimu la kukomboana sisi kwa sisi, kwa sababu hakuna ushahidi kwamba mwenye hizo dola 30 ndo mwenye brain muscle, au patriotism kubwa, au uwezo wa kuleta mabadiliko ya kweli katika ile nchi kuliko mlalahoi, mshinda njaa, ambaye hana kitu lakini anaumia kweli kweli kutokana na madudu haya yaliyomo kwenye MereMeta.

Mwanakijiji fikiria mara mbili kabla hujatuuzia hizi taarifa.
 

I asked him the same question...anasema someone has to cover the cost - which is understandable. Lakini kinachonishangaza ni hizo cost zimekuja kufumuka kwenye habari inayosadikika kuwa na umuhimu mkubwa.
Wengine wakadai kuwa Watanzania wanapenda vya bure....sasa sijui how imaginary borders zinawezaje ku-affect mindset ya watu.
 
Mwanakijiji iwapo taarifa zimefahamika kwa nini watu tununue hizo taarifa na tusipewe bure?

Kwa sababu kuna gharama katika kujua.

Je Watanzania wasioweza kuchangia hizo dola 30 lakini wanataka kufahamu huo uozo wa meremeta wafanyeje? ilhali kuna watanzania wanaufahamu huo uozo lakini wanauza hata taarifa?.

Inabidi wawabane wabunge wao ili wafanye uchunguzi na kutoa ripoti ya bure.

Mimi ninapinga kwa nguvu zote, hatua hii ya mwanakijiji kuuza hizi taarifa muhimu, taarifa za kuwakomboa watanzania lakini zinageuzwa kuwa za kuuzwa instead.

Ni vizuri kujitahidi kupinga.

Kwa jinsi hizi taarifa zilivyo muhimu, thamani yake ni kubwa sana kiasi kwamba hizi dola 30 zitakwamisha lengo la kumkomboa Mtanzania aliye masikini ajabu (dola 30 kwake ni mshahara wa mwezi).

Lengo la ripoti hii siyo kumkombia Mtanzania.

Kuna ukweli hapo.


wanakijiji fikiria mara mbili kabla hujatuuzia hizi taarifa.

Kwa kweli nimefikiria mara nyingi sana. Na uamuzi haujabadilika. Wale watakaopata wanaweza kuwadokeza.

Swali kwako: Kama hii kazi ingefanywa na timu au kamati inayolipiwa na walipa kodi unafikiri ingegarimu kiasi gani? Unafikiri kweli ripoti nzito ya namna hii nani anailipia au mimi nina kisima cha utajiri wa kugharimia haya yote kwa vile nina nini ambacho wengine hawana na mimi ni mtoto wa maskini kama wengine tu?
 
I asked him the same question...anasema someone has to cover the cost - which is understandable.

I dont think it is understandable! Hivi mmeona picha za Dowans HQ kule Costa Rica hivi unafikiri kanzi kanasafiri kwa ungo?
Lakini kinachonishangaza ni hizo cost zimekuja kufumuka kwenye habari inayosadikika kuwa na umuhimu mkubwa.

kweli ukinitaka nicharge kwa kila info ambayo napata nafasi ya kutoa kweli tutafika?

Wengine wakadai kuwa Watanzania wanapenda vya bure....sasa sijui how imaginary borders zinawezaje ku-affect mindset ya watu.

Wandugu.. ni watu 100 tu wanaweza kuchangia gharama ya haya. Mnataka itoke bure ili kiwe nini? Na hao waliotumia masaa kibao kufanya na kufuatilia habari ambazo zinatosha kabisa "kuitwa kufichua siri za serikali" kikiwaungulia mtawalipia wanasheria? au mtasema wajitolee kwa sababu ni kazi ya kujitolea?
 
Status
Not open for further replies.
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…