ripoti ya kijarida cha cheche za fikra juu ya meremeta imekamilika. Ina kurasa karibu 50 ikiambatanishwa na vielelezo lukuki ambavyo kwa wengi itakuwa ni mara ya kwanza kuviona hadharani, vielelezo ambavyo serikali yetu na baadhi ya wanasiasa mafisadi imefanya jitihada kubwa kuhakikisha havioni nuru ya siku kwa muda mrefu.
Ndani ya ripoti hii maswali kadhaa yanajibiwa kwa kina (mengine kwa kupita tu). Yanajibiwa si kwa ufundi wa hoja na uzuri wa ushawishi wa maneno bali kwa ushahidi mzito na vielelezo ambavyo vyenyewe peke yake vinatosha kabisa kufunga mjadala huu.
Tunaamini kuwa kama sisi watanzania hatutasimama na kupinga mambo ya uovu yanayofanywa kwa jina letu basi watawala wetu wataendelea kufanya maovu kwa jina letu. Tunafuata mfano wa wamarekani waliofichua na kukasirishwa na ab ghraib au waisraeli waliojitokeza kupinga vitendo vya jeshi lao dhidi ya wapalestina. Tunaamini kwenye uovu, hakuna uzalendo wala undugu – there is no patriotism in the presence of evil!
Baadhi ya maswali yanayojibiwa:
- meremeta ilianzishwa kwa ajili ya shughuli gani hasa?
- ni kampuni gani iliingia mkataba na serikali kuunda meremeta ile august 17, 1997? Ukijibu triennex basi huna budi kuipata ripoti hii kwani utakuwa umekosea.
- je tanzania inahusika vipi katika usafirishaji wa silaha haramu katika eneo la maziwa mazuu na ni kina nani wanahusika (majina yanatajwa!).
- je yule mfanyabiashara ya kifo victor bout amewahi kutumia tanzania kama njia ya kusafirisha silaha haramu kwenda kwenye nchi zenye machafuko? Angalia picha uamue mwenyewe! Vipi kuhusu dr. K.m?
- kwanini meremeta ilianzishwa 1997 na si mwaka mwingine wowote?
- unamkumbuka mzee wa "vijisenti"? Kwanini tunaamini sfo walikosea kuhusisha fedha za chenge na rada.
- kwanini waziri mkuu mmoja wa zamani aliita mambo ya meremeta ni ya "aibu" na kujulikana kwake "kungesababisha wafadhili watunyime misaada"?
- barua ya ccti kuelekea the hague, eu, us na taasisi za kimataifa za haki za binadamu.
- n.k!!
excerpts:
[1] tume ya ukweli na upatanisho, juzuu ya 2, 2003 uk. 39
jinsi ya kuipata:
kutokana na unyeti wa taarifa hii na madai mazito ambayo yametulazimu kutoa tumetengeneza nakala 100 tu. Kila nakala ina namba yake (serialized) na ina ufunguo wake (password protected). Kuna sababu mbili za kufanya hivi: Kwanza, kuhakikisha kuwa ni wale tu ambao wanataka kujua ili watende ndio watapata. Lengo letu siyo kutoa taarifa au kufurahisha genge bali tunataka kuhakikisha hatua muafaka zinachukuliwa. Sababu ya pili ili tulinde kuenea kwake, kwa ajili ya usalama wetu na usalama wa wale waliotusaidia kufanikisha kutolewa kwake, mwezi mmoja baada ya ahadi na ombi letu kwa waziri mkuu pinda ambalo limeenda bila kujibiwa.
inapatikana hivi:
ripoti inapatikana kwa njia ya pre-ordering (yaani order zikishatimia zote zinatolewa kwa wakati mmoja) kwa wale ambao watachangia dola 30 au shilingi elfu thelathini tu au zaidi kwa njia zifuatazo:
- kupitia mtandao wa http://www.mwanakijiji.com kuna kitufye cha kuchangia (donate button) cha paypal inc., kwenye ukurasa wa mbele (homepage - siyo ukurasa wa forum). Hapo tunaweza kupokea malipo ya kadi za kibenki katika njia ya usalama wa hali ya juu na wachangiaji wote wanamakia sirini (rekodi yetu ya miaka mitatu hatujawahi kuvujisha jina la mchangiaji yeyote yule!).kadi za visa, mastercard, express zinapokelewa.
- kwa taasisi au watumishi wa umma (vips) ambao kwa sababu za wazi wangependa kutojulikana wasiliana nami kwa email au private message na utapata maelezo ya kuwasiliana na mwandishi wa habari mchunguzi wa gazeti la kiingereza la kila siku la nchini aliyepo tanzania ambaye atapokea fedha hiyo pamoja na email yako ambayo tutakutumia nakala hiyo katika usiri mkubwa. Yeye pia anaweza kupokea kwa njia ya western union kwa wale ambao wangependa kutumia njia hiyo.
- kwa mtu mwingine yeyote tuma fedha kwa njia yarecharge vouchers kwenda namba: 0713444649. Vouchers ziwe ni za tigo, zain au zantel.
kama mipango yote itakwenda ilivyo, basi tunatarajia kutuma nakala hizo 100 siku ya jumatano wiki ijayo kwa wale waliochangia. Hivyo ina maana watu wana siku tano za kukamilisha oda zao. Pamoja na ripoti hiyo, tumeambatanisha pia ripoti yetu ya 2006 juu ya "tracing reports of tanzania's role in arms trafficking".
Oda nakala yako mapema kwani tutafanya kwa mtindo wa "aliyewahi mpe" –
first come, first serve.
nb: -
email moja kwa nakala moja.
- hakuna nakala itakayotangulia mchango; na hakuna mtu atakayepata nakala kabla ya watu wengine. Watu wote watakaokuwa wamechangia watapata nakala zao jumatano. No exception.
m. M. Mwanakijiji
consortium of concerned tanzanians intl.
+ 1 248-556-6748